Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 25.08.2022

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea huenda itamnunua mlinzi wa Manchester United na Uingereza Harry Maguire, 29, ikiwa hawataweza kumsajili mlinzi wa kati wa Ufaransa Wesley Fofana, 21, kutoka Leicester. (Evening Standard)
Newcastle United wameweka rekodi ya klabu kutenga kitita cha £60m kumnunua mshambuliaji wa Real Sociedad mwenye umri wa miaka 22 Alexander Isak. (Mail)
The Magpies hatimaye wanaweza kulipa zaidi ya £60m kwa Isak. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Ajax wanashikilia pauni milioni 84 kumnunua winga wa Brazil Antony, 22, ambaye amedhamiria kuhamia Manchester United. Wawakilishi wake wanasalia Uingereza kusaidia kufanikisha mpango huo. (Telegraph)
Antony aliwasilisha ombi la uhamisho Jumatano ili kufanikisha nia yake ya kuondoka rasmi. (Mirror)
Liverpool wametoa ofa kwa Barcelona kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25. (Futbol Total, via Forbes)

Chanzo cha picha, Getty Images
West Ham wamekuwa na ofa ya euro 50m (£42.2m) kwa kiungo wa kati wa Brazil Lucas Paqueta, 24, iliyokataliwa na Lyon. (L'Equipe, via Metro)
Arsenal haitarajiwi kumnunua Paqueta licha ya ripoti kuwa wanamtaka. (Express)
West Ham wamepewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Ainsley Maitland-Niles, 24, katika wiki za mwisho za dirisha la uhamisho. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wamefanya mazungumzo na Newcastle United kuhusu kumsajili mlinda mlango wa Slovakia Martin Dubravka, 33. (Mail)
Klabu hizo bado hazijafikia makubaliano lakini Manchester United wamewasilisha ofa ya mkopo kwa Dubravka. (Athletic)
Mtendaji Mkuu wa Manchester City Ferran Soriano amefutilia mbali uwezekano wa kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva, 28, kuihama klabu hiyo msimu huu wa joto. (SER Catalunya, via 90min)

Chanzo cha picha, Getty Images
Aston Villa wameshusha dau kwa mlinzi Frederic Guilbert huku wakitafuta kumuuza Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 27. (L'Equipe, via BirminghamLive)
Nottingham Forest wana nia ya kumsajili mlinzi wa kulia wa Ivory Coast Serge Aurier, 29, ambaye anapatikana kwa uhamisho wa bila malipo baada ya kuondoka Villarreal. (Sun)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Callum Hudson-Odoi mwenye umri wa miaka 21 yuko tayari kujiunga na Bayer Leverkusen kwa mkopo. (Guardian)
Everton wako kwenye mazungumzo na Manchester United kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati wa Uingereza James Garner, 21. (Athletic)












