Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Je, Man Utd kumsajili kipa wa New Castle?

Nick Pope

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester United ina mpango wa kumsajili kipa wa England Nick Pope, 33, endapo Newcastle itakamilisha dili la kumsajili mlinda lango wa Southampton 27 Aaron Ramsdale, 27. (Sportsport)

Newcastle imekubaliana na Southampton kumsajili Ramsdale kwa mkopo na chaguo la kufanya mkataba huo kuwa wa kudumu mwishoni mwa msimu huu. (Athletic - usajili unahitajika)

Manchester United pia ina nia ya kumsajili mlinda lango wa Paris St-Germain na Italia Gianluigi Donnarumma, lakini inasita kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na Manchester City . (Sun)

Arsenal bado inamtaka winga wa Uingereza Eberechi Eze, 27, lakini haiko tayari kutimiza masharti ya kulipa ada ya zaidi ya £60m hadi Crystal Palace itakapopunguza bei ya mchezaji huyo. (Athletic - michango inahitajika),

Manchester City imekataa dau la pauni milioni 25 lililowasilishwa na Nottingham Forest kumsajili kiungo wa Uingereza James McAtee, 22. (Sky Sports)

Paris St-Germain imepiga hatua katika juhudi za kufikia mkataba na Bournemouth kumsajili beki wa Ukraine Illia Zabarnyi, 22. (Fabrizio Romano)

Borussia Dortmund inafuatilia hali ya winga wa Arsenal Leandro Trossard, 30, lakini mshambuliaji huyo wa Ubelgijy pia anasakwa na vilabu viwili vya Ligi ya Premia. (Sky Sports Germanu)

Leandro Trossard

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Borussia Dortmund inamnyatia winga wa Arsenal Leandro Trossard

Klabu ya Lyon ya Ufaransa inavutiwa na kiungo wa Uingereza Tyler Morton, 22, na tayari imewasiliana na Liverpool. (Times)

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Manchester United iko tayari kukubali punguzo la ada ya £17m kwa Jadon Sancho, 25, huku klabu za Borussia Dortmund na Juventus zikimuwania winga huyo wa Uingereza. (Mail)

United imesitisha mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Nicolas Jackson, 24, kwa sababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal anataka mshahara mkubwa kupita kiasi. (Mirror)

Napoli inamtaka kiungo wa kati wa Manchester City Jack Grealish, 29, lakini inakabiliwa na changamoto ya kufikia mshahara ikizingatia orodha ya wachezaji inaowalenga kama winga wa Chelsea na Uingereza Raheem Sterling, 30, na mshambuliaji wa Manchester United wa Argentina Alejandro Garnacho, 21. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

United wanataka kumtoa Garnacho na wamezungumza na Aston Villa na Chelsea kuhusu uwezekano wa kufanya makubaliano. (Kujitegemea), nje

Everton imepatia kipaumbele usajili wa kiungo wa kati wa Juventus na Brazil Douglas Luiz, 27, kabla ya kushughulikia mpango wa kumsajili Grealish. (GiveMeSport)

Ollie Watkins wa Aston Villa, 29, anaongoza orodha ya wachezaji wawili wanaosakwa na klabu ya Manchester United huku mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sekso, 22, akiwa chaguo la pili. (Sun)

Imetafsiriwa na Ambai Hirsi