Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Everton wanamnyemelea Kalvin Phillips Manchester City

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton wanachunguza kwa makini uwezekano wa kumtia mkononi kiungo wa Manchester City Kalvin Phillips ,29, mwezi Januari. (Football insider)
Liverpool ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya ligi kuu ya premier vilivyo na ari ya kumsajili kiungo wa kati wa Crystal Palace Adam Wharton ,21, kutoka Crystal Palace. (Mail )
Brentford haina azma ya kumpa mkataba Michail Antonio raia wa Jamaica aliye na umri wa miaka ,35, licha ya aliyekuwa mshambuliaji huyo wa West Ham kufanya nao mazoezi. (Bees)
Manchester United wanaendelea na kufanya mazungumzo na Harry Maguire ,32, kuhusu mkataba mpya na maafisa wa klabu wameshakutana ana kwa ana na wawakilishi wa mlinzi huyo wa England ambaye mkataba wake unafikia tamati msimu ujao wa majira ya joto. (Fabrizio Romano)
Manchester United wako katika pilka pilka za kuwapa Juventus pauni milioni 78 kumunua mshambuliaji wa Uturuki Kenan Yildiz ,20, ambaye pia anawindwa na Chelsea. (Caught offside)
Wakiwa na lengo kuu la kumsajili kiungo mpya wa kati msimu ujao wa majira ya joto, Manchester United sasa wanafikiria kuwafukuzia Carlos Baleba wa Brighton na Cameroon,21, na Elliot Anderson wa England,na Nottingham Forest , 22.(Sky sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
Crystal Palace washakubali kuachana na Marc Guehi, na wanapanga kumtoa katika uhamisho wa Januari majira ama majira yajayo ya joto huku Liverpool, Barcelona na Real Madrid zikiwa miongoni mwa vilabu vinavopigana vikumbo kumsajili beki huyo wa England. (Express )
Napoli hawapati usingizi kwa kuitafuta saini ya kiungo wa Manchester United Kobe Mainoo wakati wa uhamisho wa Januari licha ya awali kutaka kumsajili kiungo huyo wa England msimu wa uhamisho wa majira ya joto. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Beki kisiki wa kati wa Nottingham Forest na Brazil Murillo, 23,ni jina moja ambalo liko namba moja katika orodha ya wachezaji wanaowindwa na Chelsea inapopanga kuimarisha safu yake ya ulinzi.(Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
March Guiu ,19, wa Chelsea na Uhispania anaazimia kurejea klabu ya Sunderland wakati wa uhamisho wa Januari licha ya chipukizi huyo kurejeshwa darajani kutoka Sunderland mwezi agosti alipokuwa kwa mkopo
Imetafsiriwa na Ahmed Bahajj na kuhaririwa na Ambia Hirsi












