Mbappe mdogo atokeza kwenye kivuli cha kaka yake

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Wakati mwingine si rahisi kuwa ndugu mdogo wa mwanasoka wa kulipwa - hata zaidi wakati kaka yako ni mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani.
Ethan Mbappe, mwenye umri wa miaka 18, ni kaka wa nyota wa Real Madrid Kylian, mwenye umri wa miaka minane.
Wachezaji wote wawili walikuwa Paris St-Germain kwa wakati mmoja, lakini wakati Kylian alipoamua kuwaacha wababe hao wa Ufaransa mwishoni mwa kandarasi yake na kujiunga na Real Madrid msimu uliopita wa joto, mkataba wa Ethan pia haukuongezwa upya katika klabu hiyo.
Sasa akiwa Lille na ambapo bado hajafunga bao lake la kwanza katika klabu hiyo, Ethan anatarajiwa kumenyana na PSG siku ya Jumapili, na ana matumaini ya kuwa katika vichwa vya habari dhidi ya klabu ambayo alianza soka yake.
Kufuata nyayo za Kylian Mbappe
Mabao hugonga vichwa vya habari, hivyo kutokana na nafasi ya Ethan kuwa kiungo hawezi kumzidi kaka yake kwenye idara hiyo.
Lakini kijana huyo anaonekana kuwa na kipaji cha kusisimua katika haki yake mwenyewe.
Mawazo yake yalisifiwa alipotoka kwenye mfumo wa vijana wa PSG, akionekana kumudu vyema matarajio ambayo yalikuja na kuwa Mbappe.
Laurent Glaize, mkuu wa zamani wa kuajiri vijana huko Caen, alitumia miaka mitatu kumfuatilia Kylian mchanga na kuwa karibu na familia ya Mbappe wakati huo.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Akiongea kuhusu Ethan mnamo 2022, aliiambia TNT Sports: "Yeye ni mtoto mwenye usawa, aliyesoma vizuri ambaye ana heshima hata ikiwa ni wazi yuko kwenye kivuli cha kaka yake, suala ambalo sio rahisi kwake.
"Lakini naona ametulia na mwenye utu wa kweli, naona anaimudu presha hii vizuri, hakosei pale alipo kwenye mechi, hata kama tayari anaombwa autographs zaidi kwa ajili ya jina lake, kuliko alichofanya, kwa sababu bado ni mdogo."
Akisifiwa kwa akili yake ya soka, utulivu kwenye mpira na uwezo wa kupiga pasi, Ethan aliwavutia makocha wa PSG na akapewa mechi yake ya kwanza ya ligi akiwa na umri wa miaka 16 tu, akitokea kama mchezaji wa akiba katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Metz, huku Kylian akifunga mabao mawili kati ya hayo.
"Ethan ni mchezaji wa kuvutia sana ambaye anaweza kucheza katika nafasi kadhaa," bosi wa PSG Luis Enrique alisema baada ya mchezo huo.
"Nina uhakika atacheza tena. Ana jina la ukoo la kifahari, ambalo ni vigumu kuliishi."
Kwa jumla, alicheza mechi tano PSG kabla ya kuondoka mwishoni mwa kandarasi yake msimu uliopita wa joto, ingawa kulikuwa na utata kuhusu kuondoka kwake.
Kylian hapo awali alidokeza, nje kwamba Ethan kutopata mkataba mpya PSG kulihusishwa na uamuzi wake wa kuondoka na kujiunga na Real Madrid, na alikuwa tayari kusalia katika miamba hiyo ya Ufaransa ikiwa na maana kwamba kaka yake amepata mkataba mpya huko pia.
"Ni jambo ambalo liliniathiri zaidi," Kylian alisema.
"Yeye [Ethan], hakuuliza chochote. Real Madrid yake ilikuwa PSG. Nini Real ilimaanisha kwangu, ndoto yake ya utotoni, ilikuwa PSG.
"Wakati mmoja, hata nilimwambia: 'Ikiwa unataka, nitaongeza [mkataba wangu] na unaweza kubaki, tutabaki hapa.' Ningeacha ndoto yangu ya Madrid na kubaki kwa ajili yake.
"Ethan aliniambia... 'Sitaki kukaa hapa, walichokufanyia, walichonifanyia si kawaida. Kama angeniambia, 'Kylian, ndicho ninachotaka', ningeachana na ndoto yangu ya Madrid na kubaki kwa ajili yake."
Kujiundia njia yake ya soka

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Msimu wa kwanza wa Ethan akiwa Lille ulitatizwa na majeraha, ambayo yalimnyima fursa ya kukabiliana na kaka yake katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Septemba mwaka jana.
"Ndoto yangu ya kukutana na kaka yangu kwenye Ligi ya Mabingwa iko mbali, lakini haijatoweka," Ethan alisema kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuondolewa kwenye mechi hiyo.
Ethan alicheza mechi chache tu za kikosi cha kwanza msimu uliopita lakini sasa hana jeraha, atakuwa na matumaini ya kujiimarisha katika kikosi cha kwanza .
Tayari amefikia hatua muhimu kwa kufunga bao lake la kwanza akiwa na Lille mapema mwezi huu - bao la dakika za majeruhi na kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Toulouse.
Mshindi huyo wa kipekee aliiweka Lille kileleni mwa Ligue 1 kwa muda mfupi na ingawa wameshuka hadi nafasi ya sita, Ethan anaendelea kujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza, baada ya kucheza mechi mbili zaidi za ligi.
Huku Lille wakishiriki Ligi ya Europa msimu huu, hakutakuwa na nafasi kwa Ethan kutimiza ndoto yake ya kukutana na kaka yake kwenye mechi ya ushindani kwa sasa, lakini hilo linamuacha na fursa ya kujikita katika kujitengenezea jina kwa njia yake mwenyewe.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












