‘Studio ya ngono ilituajiri tukiwa wasichana wa shule’

- Author, Sofia Bettiza
- Nafasi, BBC
- Muda wa kusoma: Dakika 5
Alasiri moja, Isabella alipokuwa akitoka shuleni, mtu mmoja alimpa kikaratasi mkononi mwake. "Je! Unataka kupata pesa na uzuri wako?" kulikuwa na swali.
Anasema studio inayotafuta wanamitindo ilionekana kuwalenga wanafunzi wadogo katika eneo lake huko Bogotá, mji mkuu wa Colombia.
Akiwa na umri wa miaka 17, na mtoto wa miaka miwili wa kumlea, alihitaji pesa sana, kwa hiyo alikwenda pamoja na mtu huyo ili kujua zaidi.
Anasema alipofika, ilikuwa ni studio ya ngono, inayoendeshwa na wanandoa katika nyumba - ilikuwa na vyumba vinane vilivyopambwa.
Wanamitindo hufanya vitendo vya ngono ambavyo vinatiririshwa kwa watazamaji kote ulimwenguni mubashara, wanatuma ujumbe na kutuma maombi kupitia ujumbe.
Siku iliyofuata Isabella, ambaye jina lake halisi hatulitumii, alianza kazi - ingawa ni kinyume cha sheria nchini Colombia kwa studio kuajiri wanamitindo wa ngono walio na umri wa chini ya miaka 18.
Isabella anasema kisha walimwambie arikodi mubashara akiwa shuleni, kwa hivyo wanafunzi wenzake walipokuwa wakijifunza Kiingereza, alitoa simu yake kimya kimya na kuanza kujirekodi chini ya meza yake.
Anaeleza jinsi watazamaji walivyoanza kumwomba afanye vitendo maalum vya ngono, kwa hiyo alimwomba mwalimu ruhusa ya kwenda kwenye choo, akiwa amejifungia, alifanya kile ambacho wateja walikuwa wameomba.
Mwalimu wake hakujua kinachoendelea. Kwa hivyo nilianza kufanya hivyo darasani", anasema Isabella. 'Ni kwa ajili ya mtoto wangu. Ninafanya hivyo kwa ajili yake."
Biashara ya ngono

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Idadi ya watazamaji kila mwezi katika majukwaa ya kuonyesha ngono mubashara ulimwenguni imeongezeka zaidi ya mara tatu tangu 2017, na kufikia karibu bilioni 1.3, hadi Aprili 2025, kulingana na kampuni ya uchanganuzi ya Semrush.
Colombia inakadiriwa kuwa na wanamitindo zaidi kuliko nchi nyingine yoyote - 400,000 - na studio 12,000, kulingana na Fenalweb, shirika linalosimamia ngono za mubashara.
Wanamitindo wengi wanaofanya kazi katika studio hufanya hivyo kwa sababu hawana maeneo, vifaa au intaneti nyumbani - mara nyingi ikiwa ni maskini au wadogo na bado wanaishi na wazazi.
Waigizaji hao waliambia BBC kwamba studio hizo mara nyingi hujaribu kuwavutia kwa ahadi ya kupata pesa kwa urahisi katika nchi ambayo theluthi moja ya watu wanaishi katika umaskini.
Washiriki walieleza kuwa ingawa baadhi ya studio zinaendeshwa vyema na kuwapa waigizaji usaidizi wa kiufundi ila nyingine unyanyasaji umeenea kutoka kwa waendeshaji wasio waaminifu.
Naye Rais wa Colombia, Gustavo Petro, amewataja wamiliki wa studio kama "mabwana watumwa" ambao huwalaghai wanawake na wasichana, kama Isabella, kuamini kuwa wanaweza kupata pesa nzuri.
Wanamitindo wengine ambao BBC ilizungumza nao wanasema walipewa vitambulisho bandia na studio hizo ili kurikodi mubashara wakiwa na umri wa chini ya miaka 18.
Watazamaji wanapenda wasichana

Keiny sasa ana umri wa miaka 20 na anafanya kazi akiwa chumbani kwake nyumbani huko Medellín. Anasema watazamaji "hupenda sana unapoonekana mdogo. Wakati mwingine nadhani hilo ni tatizo."
Anasema aliingia katika biashara hiyo ili kusaidia familia yake kifedha baada ya wazazi wake kuamua kuachana.
Baba yake anajua anachofanya na anasema anamuunga mkono.
Akikumbuka nyuma, Keiny anadhani alikuwa mdogo sana alipoanza akiwa na umri wa miaka 17, lakini hata hivyo, yeye hawakosoi waajiri wake wa zamani.
Badala yake, anaamini walimsaidia katika kazi ambayo anasema sasa inamletea takriban dola $2,000 (£1,500) kwa mwezi - zaidi ya mshahara wa chini kabisa nchini Colombia, ambao ni takriban $300 (£225) kwa mwezi.
"Shukrani kwa kazi hii, ninasaidia mama yangu, baba yangu, na dada yangu - familia yangu yote," anasema.
Mtazamo huo unaungwa mkono na studio - ambazo baadhi zinapenda kuonyesha kuwa zinawajali wasanii wao.
Maumivu na udhilali
Lakini kama rais wa nchi hiyo alivyodokeza, si kila mwigizaji anatendewa vyema au anapata pesa nzuri.
Wanamitindo wanasema studio ada zinazolipwa na watazamaji, wengine hupewa 20-30%.
Hii inamaanisha kuwa ikiwa onyesho litatengeneza $100 (£75), mwanamitindo huyo kwa kawaida atapata kati ya $20 (£15) na $30 (£22). Walieza studio mara nyingi huchukua pesa zaidi.
Wanamitindo wanasema kumekuwa na nyakati ambapo walikuwa mubashara kwa masaa nane na kupata dola $5 (£4) - jambo ambalo linaweza kutokea ikiwa onyesho halina watazamaji wengi.
Wengine wanasema wameshinikizwa kuwa mubashara kwa hadi masaa 18 bila mapumziko na kutozwa faini kwa kwenda kula au kwenda chooni.
Ripoti ya Human Rights Watch, iliyochapishwa Desemba 2024. Mwandishi, Erin Kilbride, ambaye alifanya utafiti, aligundua baadhi ya watu walikuwa wakirekodiwa kwenye vyumba vichafu vilivyojaa kunguni na mende na wakilazimishwa kufanya vitendo vya ngono vinavyoumiza na kudhalilisha.
'Walinidanganya'
Baada ya miezi miwili, Isabella anasema alikuwa na hamu ya kupokea malipo yake ya kwanza. Isabella anaeleza kuwa alilipwa dola $42; £31) - chini sana kuliko alivyotarajia. Anaamini kuwa studio ilimlipa asilimia ndogo kuliko makubaliano.
Pesa hizo zilikuwa duni, anasema, alitumia kununua maziwa na nepi. Anasema "walinidanganya."
Isabella, ambaye bado yuko shuleni, baada ya miezi michache aliacha kazi hiyo.
Yeye na wafanyakazi wengine sita wa zamani wa studio hiyo wamekusanyika kuwasilisha malalamiko rasmi kwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali.
Kwa pamoja, wameishutumu studio hiyo kwa unyonyaji wa watoto, unyonyaji wa wafanyakazi na unyanyasaji wa kiuchumi.















