Wasiwasi waongezeka juu ya Akili Mnemba (AI) katika biashara ya ngono

Chanzo cha picha, Cybothel
- Author, Nicola K Smith
- Nafasi, BBC
Baadaye mwezi huu, watu wa Berlin, Ujerumani wataweza kuagiza mdoli wa ngono wa akili bandi kwa matumizi ya saa moja katika danguro la kwanza duniani la mtandaoni litakapoanza kutoa huduma hiyo kufuatia awamu ya majaribio.
Wateja wataweza kufanya mapenzi wakizungumza na mwanasesere na kuingiliana nae kimwili.
"Watu wengi hujisikia bora kufanya mambo yao binafsi na mashine kwa sababu haiwahukumu," anasema Philipp Fussenegger, mwanzilishi na mmiliki wa danguro la Cybrothel.
Hiyo ni mojawapo tu ya njia nyingi ambapo akili bandi katika biashara ya ngono za mtandaoni imeanza kufanya kazi.
Ripoti ya SplitMetrics ilibaini kuwa programu za akili bandi zimepakuliwa mara milioni 225 kwenye mtandao wa Google Play.
“Midoli ya mapenzi ya akili bandi inaweza kuwa na faida kubwa,” anasema Misha Rykov, mtafiti wa mambo ya faragha kutoka Mozilla.
Wasiwasi uliopo

Chanzo cha picha, Jason Sheldon
Dkt. Kerry McInerney, mtafiti katika Kituo cha Leverhulme for the Future of Intelligence, kutoka chuo cha Cambridge anasema: “Kuna hatari ya uraibu.”
Anasema, "mawasiliano ya kutumia akili bandia mara nyingi huwalenga watu wapweke, haswa wanaume."
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Nyingi za kurasa za kuandikiana na akili bandia (chatbots) tulizozikagua zina uwezekano mkubwa wa kuleta uraibu na madhara kadhaa, haswa kwa watumiaji walio na changamoto za afya ya akili."
Mozilla imeweka maonyo katika kurasa hizo "tunapogundua mada za unyanyasaji, vurugu na uhusiano wa watoto," anasema Rykov.
Pia alizungumzia suala la faragha. Kurasa za kuandikiana zimeundwa kukusanya "idadi kubwa ya taarifa binafsi za watu".
Rykov anaongeza kuwa 90% ya programu zilizokaguliwa na Mozilla "zinaweza kutoa taarifa au kuuza taarifa binafsi," wakati zaidi ya nusu ya programu hizo haziruhusu watumiaji kufuta taarifa zao binafsi.
Tamara Hoyton, mshauri mkuu katika huduma ya ushauri nasaha Relate, anasema: "Baadhi ya matatizo yanaweza kutokea ikiwa matukio mabaya yatatokea katika program hizo ikiwa matukio hayo hayalingani na mahitaji ya watumiaji wa ponografia za akili bandia."
Bi Hoyton anaongeza kuwa, katika baadhi ya matukio, ponografia za akili bandia zinaweza kumpeleka mtumiaji katika maeneo hatari.

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Kampuni zinazotumia akili bandia katika tasnia ya burudani za ngono zinakubali kwamba kuna haja ya kuwa na tahadhari, lakini akili bandia zina umuhimu mkubwa.
Philipp Hamburger, mkuu wa masuala ya akili bandia huko Lovehoney, anasema kampuni hiyo inalenga "kuboresha mambo ya ngono kwa wateja wake, badala ya kuyaondosha."
Wengine wanaamini akili bandia itakuwa na athari chanya kwenye sekta hiyo. Ruben Cruz ni mwanzilishi mwenza wa The Clueless Agency yenye makao yake Barcelona, ambayo iliunda akili bandia ya mwanzo ya mtu mwenye ushawishi, Aitana Lopez.
Anasema kuwa tasnia ya ngono itakuwepo kila wakati, na akili bandi inaweza kusaidia kupunguza wasiwasi wa maadili kwa kuhakikisha kuwa yaliyomo hayajaundwa kwa kutumia watu halisi.
"Mabadiliko haya yanalenga kuhakikisha kuwa hakuna mtu, mwanamume au mwanamke, ambaye atalazimishwa kujamiiana katika siku zijazo."
Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Yusuf Jumah












