Magenge yanavyotumia 'Miongozo ya ngono' kwa ulaghai katika mitandao ya kijamii, BBC imegundua

Wahalifu wanauza miongozo kwenye mitandao ya kijamii kuhusu jinsi ya kuwalaghai watu kutuma picha au video zao za utupu ambazo walaghai huzitumia kuwatishia waathiriwa kuzitangaza iwapo watakataa kutekeleza matakwa yao, Habari za BBC zimebaini.
Miongozo hiyo inawaonyesha watu jinsi ya kujifanya kama wanawake wachanga mtandaoni, kumrubuni muathiriwa kutuma picha za ngono au video na kisha kumtishia kuzichapisha au kuushirikisha umma iwapo atasindwa kutimiza matakwa yao.
Siku ya Jumanne, Olamide Shanu alifikishwa mahakamani mjini London. Anaaminika kuwa miongoni mwa genge lililopata £2m kutokana na kuwalaghai watu wazima na watoto mtandaoni kwa kutumia picha na video zao za utupu.
Mwezi uliopita Shirika la Kitaifa la Uhalifu lilitoa tahadhari kwa shule kote Uingereza , kuonya dhidi ya hatari ya unyanyasaji wa ngono wa walaghai wanaotumia mitandao ya kijamii.

Wataalamu wanasema pia kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wanaokumbwa na ulawiti unaofanywa na magenge ya watu wanaoishi katika mataifa ya Afrika Magharibi, hasa Nigeria.
Nchini Uingereza, vijana wawili wa Uingereza wametambuliwa kujiua tangu Oktoba 2022 baada ya kuwa waathiriwa wa ngono.
Paul Raffile, mtaalamu wa ujasusi na mtaalam wa ngono, anaelezea jambo hilo kama "tisho kubwa" kwa watoto.
"Walaghai wa mtandao katika miaka hii miwili iliyopita wamegundua kuwa wanaweza kutajirika haraka sana kwa kulaghai soko ambalo halijatumiwa.
"Na hao ni vijana," alisema.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Bw Raffile alisema kuwa watu wazima wamekuwa walengwa wa matumizi ya picha zaa za utupu kwa miaka mingi - na sasa wavulana walio katika umri wa kubalekhe ni miongoni mwa walio hatarini zaidi.
"Wanatafuta waathiriwa wao kwa kwenda kwenye mitandao ya kijamii na kutafuta shule za upili (sekondari) na timu za michezo ya vijana, na kisha 'kuwafuata' au 'kufanya urafiki nao'," alisema.
BBC News iligundua miongozo ya jinsi ya kutekeleza uhalifu huo inauzwa wazi katika video zilizochapishwa mtandaoni.
Imefafanuliwa kwa kina jinsi ya kusajiri nambari za simu zisizoweza kupatikana, kuunda wasifu bandia wa mitandao ya kijamii na kutumia njia salama za malipo.
Wengine wanajivunia idadi ya watu waliowashawishi - mmoja aliandika kwamba muathiriwa alimlipa mara kwa mara, "kila Ijumaa".
Mtoto wa kiume wa Lucy mwenye umri wa miaka 14 alijipata katika mtego wa ulaghai wa genge mwaka huu.
Ingawa hakuwa ametuma picha zozote yeye mwenyewe, walaghai hao walitumia waliihariri picha yake wakaiweka katika hali ya utupu na katika maandishi wakamtishia kuishirikisha kwa umma.
"Ulikuwa ujumbe, kimsingi ukisema, 'usitufunge. Usipotutumia pesa ndani ya saa 24, tutatuma picha kwa watu unaowasiliana nao,” alisema.
"Alishtuka sana. Na alikuwa anatetemeka kimwili."
Kijana huyo tayari alikuwa amewalipa wafanyabiashara hao pauni 100, lakini kwa usaidizi wa wazazi wake alifunga akaunti na simu. Hakuwahi kubata mawasiliano kutoka kwa walaghai hao tena.
"Kama asingekuwa nyumbani asubuhi hiyo, na nisingekuwa jikoni, na kama asingezungumza nami, sijui ingekuwaje kwake," alisema Lucy.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 33 anasakwa katika jimbo la Idaho kwa tuhuma za ulaghai wa picha za utupu, utakatishaji fedha na udukuzi mtandaoni.
Mashtaka hayo yanawahusu waathiriwa wanne, mmoja wao akiwa mtoto.
Wachunguzi wanaamini kuwa kunaweza kuwa na mamia ya waathiriwa katika kipindi cha miaka mitatu.

Bw Raffile anasema Makampuni makubwa ya Teknolojia hayafanyi juhudi za kutosha kukomesha ulaghai wa ulaghai wa picha za kingono.
"Uhalifu huu umeshamiri sana kwenye Instagram na Snapchat katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ... majukwaa haya yanahitaji kuwafuata wahalifu hawa kwa ukali," alisema.
Snapchat aliiambia BBC: "Tumekuwa tukiongeza juhudi zetu za kukabiliana nayo ikiwa ni pamoja na chaguo la kuripoti hasa vitisho vya kuvuja kwa maudhui ya ngono, na elimu ya ndani ya programu kwa vijana."
Katika taarifa Meta, ambayo inamiliki Instagram, ilisema ilitoa "chaguo maalum la kuripoti ili watu waweze kuripoti mtu yeyote anayetishia kushiriki picha za kibinafsi".
"Sisi vijana walio chini ya umri wa miaka 18 nchini Uingereza huingia kwenye akaunti za kibinafsi za Instagram wakati wa kujiandikisha, ambayo huficha wafuasi wao na orodha zinazofuata, na katika mipangilio mikali ya utumaji ujumbe," iliongeza.
TikTok ilisema jukwaa hilo lilibuniwa "kutokuwa na ukarimu kwa wale wanaokusudia kusababisha madhara kwa vijana na hatuvumilii maudhui yoyote au tabia inayokuza unyanyasaji wa ngono".
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












