"Walinivua nguo, wakanikalisha kwenye kiti na kuipiga miguu yangu kwa umeme ."

Ramani
Maelezo ya picha, Maelfu ya vijana wa kiume na wa kike kutoka , Afrika Mashariki, ni miongoni mwa waliolaghaiwa na kufanyia kazi mitandao kulingana na Interpol

Maelfu ya vijana wa kiume na wa kike kutoka Asia, Afrika Mashariki, Amerika Kusini na Ulaya Magharibi waliahidiwa kazi inayohusiana na kompyuta lakini badala yake walilaghaiwa na kufanyia kazi bustani za uhalifu wa mtandaoni, Interpol ilisema.

Wale waliokataa kutii amri walipigwa, kuteswa au kubakwa.

"Walinivua nguo, wakanikalisha kwenye kiti na kuipiga miguu yangu kwa umeme. Nilidhani huu ndio mwisho wa maisha yangu."

Ravi (si jina lake halisi) alikwenda Thailand akitarajia kupata kazi katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano (IT), lakini badala ya kukaa katika jengo la ghorofa kubwa huko Bangkok na kufanya kazi hii kama alivyotarajia ,Kijana Msri Lanka mwenye umri wa miaka 24 alijikuta amenaswa katika jiji kubwa huko Myanmar.

Alitekwa nyara karibu na mji wa mpaka wa Thailand wa Mae Sot na kusafirishwa kwa njia haramu na kuvuka mto.

Huko, alisema, aliuzwa kwa chuo kinachodhibitiwa na genge la utapeli mtandaoni linalotumia lugha ya Kichina. Wanalazimisha watu wanaosafirishwa kama Ravi kushiriki katika ulaghai wa muda mrefu, wakitumia utambulisho wa uwongo kuiga wanawake mtandaoni na kuwalaghai wanaume ambao hawana wake katika nchi za Marekani na Ulaya.

Huwashawishi watu wanaowalaghai kuwekeza kiasi kikubwa cha pesa kwenye mifumo ghushi ya biashara na kuwaahidi mapato ya haraka.

‘’Utumwa wa mtandao’’ ambao Ravi alijipata ndani yake unapatikana ndani kabisa ya msitu wa Myawaddy, nchini Myanmar. Eneo hilo haliko chini ya udhibiti wa moja kwa moja wa utawala wa kijeshi wa Myanmar.

"Nilifungwa kwa siku 16 kwa sababu nilikaidi maagizo yao. Walinipa tu maji yaliyochanganywa na misokoto ya sigara na majivu ," Ravi aliambia BBC.

"Siku yangu ya tano au sita katika mahabusu, wasichana wawili walipelekwa kwenye mahabusu jirani wakabakwa na wanaume 17 mbele ya macho yangu," aliongeza.

"Mmoja wa wasichana hao ni Mfilipino. Sijui uraia wa muathiriwa mwingine."

Waathiriwa ni akina nani?

f
Maelezo ya picha, Ravi alisema alidhulumiwa na kuteswa kwa siku 16.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa mnamo Agosti 2023, zaidi ya watu 120,000 nchini Myanmar na zaidi ya watu 100,000 nchini Kambodia wanalazimishwa kujihusisha na ulaghai huu wa mtandaoni, pamoja na ulaghai mwingine kuanzia uchezaji kamari haramu hadi ulaghai wa sarafu ya mtandaoni (cryptocurrency).

Ripoti ya Interpol mwaka jana iligundua kuwa Laos, Ufilipino, Malaysia, Thailand na (kwa kiasi kidogo) Vietnam zote zina maeneo ya ulaghai mtandaoni.

Msemaji wa Interpol aliiambia BBC kwamba hali hiyo imebadilika kutoka tatizo la kikanda hadi tishio la usalama duniani, huku nchi nyingine nyingi pia zikihusika, na kuwa maeneo ya ulaghai, nchi za kupita au nchi chanzo cha wahanga waliosafirishwa kwa ajili ya biashara hiyo haramu.

Serikali ya India ilitangaza mapema mwezi huu kwamba hadi sasa imeokoa raia 250 wa India ambao walikuwa wamesafirishwa kwenda Kambodia, huku Machi, Uchina ikiwarudisha mamia ya raia wake kutoka kwa eneo la utapeli huko Myanmar.

Serikali ya China pia imekuwa ikitoa shinikizo kwa serikali ya kijeshi ya Myanmar na makundi yenye silaha kufunga mbuga hizo za udanganyifu.

Mamlaka ya Sri Lanka imegundua kuwa takriban raia 56 wa Sri Lanka wamenaswa katika maeneo manne tofauti nchini Myanmar. Hata hivyo, balozi wa Sri Lanka nchini Myanmar, Janaka Bandara, aliiambia BBC kwamba wanane kati yao waliokolewa hivi majuzi kwa usaidizi wa mamlaka ya Myanmar.

Kwa wale wanaoendesha mbuga, lengo lao ni mtiririko thabiti wa wafanyakazi wahamiaji wanaotafuta nafasi za kazi.

w

Chanzo cha picha, TOM HUMBERSTONE

Maelezo ya picha, Kila mwaka, mamia ya maelfu ya wahandisi, madaktari, wauguzi na wataalamu waTehama kutoka Asia Kusini huhamia nje ya nchi kutafuta kazi

Kila mwaka, mamia ya maelfu ya wahandisi, madaktari, wauguzi na wataalamu wa Tehama kutoka Asia Kusini huhamia nje ya nchi kutafuta kazi

Mtaalamu wa kompyuta Ravi alipogundua kwamba kampuni ya kuajiri ya Thailand ilikuwa ikitoa kazi za kuingiza data huko Bangkok, alikuwa na hamu ya kuondoka Sri Lanka kuuepuka mzozo wa kiuchumi.

Muajiri huyo na mfanyakazi mwenzake kutoka Dubai walimhakikishia kwamba kampuni hiyo ingemlipa mshahara wa msingi wa rupia 370,000 -pesa za Sri Lanka (takriban dola za Marekani 1,200).

Wakiwa wanandoa wapya , Ravi na mke wake walikuwa na ndoto kwamba kazi yao mpya ingewawawezesha kumiliki nyumba yao wenyewe, kwa hiyo walichukua mikopo mbalimbali ili kuliwapa mawakala wa ndani.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Kutoka Thailand hadi Myanmar

Mapema mwaka wa 2023, Ravi na kikundi cha Wasri Lanka walipelekwa kwanza Bangkok na kisha Mae Sot, jiji lililo magharibi mwa Thailand.

"Tulipelekwa kwenye hoteli lakini punde tukakabidhiwa kwa watu wawili wenye silaha. Walituvusha mto hadi Myanmar," Ravi alisema.

Kisha walihamishwa hadi chuo kikuu kinachodhibitiwa na washiriki wa genge wanaozungumza Kichina na kupewa maagizo ya wazi ya kutopiga picha.

"Tuliogopa sana. Takriban vijana 40 wa kiume na wa kike, wakiwemo watu kutoka Sri Lanka, Pakistan, India, Bangladesh na nchi za Afrika, walizuiliwa kwa nguvu katika hifadhi hii," alisema.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Old Street, mji mdogo wa Myanmar karibu na mpaka wa China na Myanmar, umekuwa kitovu cha kamari, uuzaji wa dawa za kulevya na ulaghai wa mawasiliano ya simu.

Ravi alisema kuwa kuta ndefu na waya wenye miinuko huzuia watu kutoroka kutoka kwenye bustani hiyo, na watu wenye silaha hulinda lango la bustani hiyo mchana na usiku.

Ravi anasema yeye na wengine walilazimika kufanya kazi hadi saa 22 kwa siku na walipewa siku moja tu ya mapumziko kwa mwezi.

Wale wanaokaidi amri hukabiliwa na mateso isipokuwa pale wanapoweza kulipa pesa tu ndio wanapoweza kuondoka.

Mnamo Agosti 2022, Neel Vijay, mwanamume mwenye umri wa miaka 21 kutoka Maharashtra magharibi mwa India, alisafirishwa hadi Myanmar pamoja na wanaume wengine watano wa Kihindi na wanawake wawili wa Ufilipino. Vijay alichagua kulipa na kutoroka.

"Kuna makampuni kadhaa ambayo yanaendeshwa na watu wanaozungumza Kichina. Ni matapeli. Tuliuzwa kwa kampuni hizo," Neal alisema.

"Tulipofika huko, nilipoteza matumaini. Kama mama yangu asingewalipa fidia, ningeteswa sawa na wengine."

Familia ya Neil ililipa fidia ya rupia 600,000 za India (takriban $7,190) ili aachiliwe baada ya kukataa kushiriki katika ulaghai huo. Lakini kabla ya hapo, alishuhudia adhabu ya kikatili iliyokuwa ikitolewa kwa wale ambao walishindwa kufikia malengo yao au hawakuweza kulipa fidia.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi