Utapeli wa ustadi wa juu duniani unaojumuisha Wanigeria kwa kuzimiwa simu tu

Chanzo cha picha, Getty Images
‘’Nambari ya simu ya kampuni yangu imeunganishwa na akaunti ya benki ya kampuni yangu na simu hii ilizimwa ghafla jioni moja. Siku iliyofuata niliangalia akaunti ya benki na nikagundua kuwa mamilioni ya rupia zimehamishwa usiku mmoja kutoka kwa akaunti ya kampuni yetu hadi benki tofauti na akaunti yetu ya benki imesazwa bila chochote.’’
Kalpesh Shah ambaye anamiliki kampuni ya kibinafsi anaelezea utapeli aliofanyiwa kupitia kampuni yake yenye kutoa mamilioni ya pesa kila mwezi kulipa wafanyakazi.
Kalpesh Shah pamoja na kaka zake watatu wanaendesha kiwanda katika eneo linaloitwa Himmatnagar Garhoda nchini India.
Kalpesh Shah, 52, ambaye aliwasilisha malalamishi kutokana na wizi wa kimtandao aliofanyiwa, aliiambia BBC kwamba kampuni yake ilikuwa na nambari ya simu maalum kwa ajili ya kusimamia akaunti za benki na shughuli nyinginezo.
Nambari hii ya simu imesajiliwa kwa jina la kampuni kwa miaka 20.
Afisa anayechunguza kisa hicho katika Idara ya Uhalifu wa Mtandao aliambia BBC kuhusu kundi lililohusika katika ulaghai huo.
"Wakati mtu anayeshughulikia akaunti alipofungua barua pepe, aliona kirusi kinachofahamika kama 'Trojan bug' kimewekwa kwenye kompyuta. Kisha genge hilo la wadukuzi hufuatilia kila kitu.’’
Alisema wadukuzi hupata taarifa kama vile mifumo ya bili lakini mmiliki wa kampuni hajui chochote kuhusu hilo.
'Kwa msaada wa kirusi cha Trojan, genge linapata kwa urahisi nenosiri na kitambulisho cha kampuni.
Je, wizi huo hutokeaje?

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kalpesh Shah anasema, "Kampuni yetu ina pesa za mishahara za kuwalipa wafanyikazi.
Mnamo Mei 31, nambari ya simu iliyounganishwa na akaunti ya benki ilizimwa ghafla. Mtandao pamoja na huduma zinazotolewa pia ziliathirika na kuzima."
Anaongeza kuwa, "Niliwasiliana na mhasibu wangu Chetan Mistry ili awashe simu haraka, nikapata ujumbe kutoka kwa simu ya kampuni kwamba baada ya kupokea barua pepe kutoka kwa kampuni, simu imezimwa. Ikiomba nipige tena na tukawasha simu ili kuwezesha kadi ya siku ya zamani. Kisha mnamo Juni 1, tuliangalia akaunti yetu ya benki na tukagundua kuwa mamilioni ya rupia zimetolewa usiku na asubuhi."
Afisa anayechunguza kesi hiyo alisema, "Genge lililopangwa sasa linafanya kazi ya kupora pesa kutoka kwa makampuni kupitia kubadilisha kadi ya simu.
Magenge haya yanaendeshwa na Wanigeria.
Wameunda genge la wadukuzi huko India Magharibi Bengal, Delhi na Bihar."
Kulingana na polisi, genge hilo linalenga zaidi wamiliki wa kampuni walio na umri wa zaidi ya miaka 50 kwani watu wa umri huu mara nyingi hawafahamu sana teknolojia.
Wadukuzi hawa hutuma bili za kodi ya mapato kwa watu kama hao kwenye barua pepe zao rasmi ambayo kwa hakika ndio chanzo cha ulaghai na ufikiaji wa taarifa muhimu.
Pesa inatoka benki bila hata mmiliki wa kampuni kujua

Chanzo cha picha, BHARGAV PARIKH
Kulingana na afisa anayeshughulikia kesi hiyo, 'kuanzia kwa malipo ya pesa za kampuni hadi pesa zinazoingia kwenye kampuni, wadukuzi hupata maelezo yote muhimu.'
"Akaunti ya benki ya kampuni inapoanza kupata pesa nyingi, magenge haya hutumia kitambulisho rasmi cha barua pepe kuomba kampuni ya simu kuzuia nambari iliyounganishwa na akaunti ya benki na kupata nambari mpya na kutuma barua pepe nyingine kuijulisha benki namba mpya kwa ajili ya shughuli za miamala kwa kutumia barua pepe rasmi ya kampuni.
"Kwa sababu ya kirusi Trojan, wanapata nywila au password rasmi ya barua cha kampuni."
Aliendelea kusema, ‘’Wakati genge hili linaomba kampuni ya simu kuzima simu ya kawaida, simu inazimwa na watu ambao hawajazoea utapeli wa aina hiyo wanadhani kuna tatizo kwenye mtandao wa simu na kuanza kuzima na kuwasha tena simu.’’
Wakati huo huo, genge hilo huhamisha pesa kutoka benki kwenda kwa akaunti tofauti.
Pia simu inasimbwa na inafanya shughuli ya ulaghai wa pesa isionekane wala kujulikana.
Kitambo hili linaanza kugundulika, pesa tayari zimeshahamishwa kutoka kwenye akaunti ya benki ya kampuni.
Uhusiano wa Nigeria wa wizi wa kimtandao
Afisa anayechunguza kesi hiyo anasema kwamba genge hili lina genge jingine wanaloshirikiana nalo.
Genge hilo hukusanya watu maskini kutoka vijijini ili kufungua akaunti za benki na kudhibiti maelezo yote ya akaunti ikiwemo password au neno siri na kadi za ATM kisha wanahamisha pesa za kampuni wanayolenga kwenye akaunti hizi na baadaye pesa hizo hutolewa mara moja.
Genge hili linatoa pesa na kuziweka kwenye akaunti kuu. Mwenye akaunti hiyo ambaye sasa anatoa pesa zilizoibwa hulipwa asilimia kumi ya pesa zote kwa kubadilishana na kufanya kazi na kundi la Nigeria.
Na mkuu wa genge hubadilisha pesa hizo hadi Bitcoin au sarafu ya kidijitali na kuzituma Nigeria na kisha anapata 30% ya pesa zote.
“Operesheni nzima hii nafanyika mtandaoni kupitia mtandao wa WhatsApp, kwa hiyo mtuhumiwa mmoja hana mawasiliano ya moja kwa moja na mwenzake. Baada ya kufanya utapeli, watu hao wanabadilisha kadi ya simu lakini tumewafuatilia na kuwabaini. Tumefanikiwa kumpata mkuu wa genge anayetoa pesa kutoka benki na tunaimani wengine wote tutawabaini hivi karibuni," afisa huyo amesema.















