Golden Dome: Jinsi mfumo mpya wa ulinzi wa makombora wa Marekani utakavyofanya kazi?

Chanzo cha picha, EPA
Mfumo mpya wa ulinzi wa makombora wa Golden Dome ambao Marekani inatengeneza utafanana kimawazo na mpango wa Strategic Defense Initiative (SDI), ambao rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan alianzisha mwaka wa 1983.
Hata hivyo, kile ambacho Reagan alishindwa kuafikia, Trump anaweza kufaulu. Angalau, hivyo ndivyo utawala wake unavyoamini.
Wazo la programu zote mbili ni rahisi sana: kuzuia makombora ya masafa marefu wakati injini zinatoa miale ya moto inayoonekana wazi, wakati kombora lenyewe halijapata kasi, au katikati ya safari yao angani.
Njia rahisi zaidi ya kufanya hivyo ni kuweka vizuizi kwenye mzunguko wa Dunia.
Katika miaka ya 1980, hii haikuweza kuafikiwa kwa sababu ya kutokamilika kwa teknolojia, kwani SDI ilifikiria kuhusu mifumo ya kigeni - kama vile leza za atomiki, na mengi zaidi.
Hata risasi za kinetic, yaani, risasi zinazoharibu shabaha, zilikuwa na umbo la ajabu la mwavuli.
Setlaiti

Chanzo cha picha, Getty
Kanuni ya uendeshaji wa mfumo mpya wa ulinzi wa makombora ilielezewa wakati wa muhula wa kwanza wa urais wa Donald Trump, mnamo 2019 wakati Idara ya Ulinzi ya Marekani ilipochapisha Mapitio ya Ulinzi wa Kombora la 2019.
Ilisema kuwa mtandao wa vyombo vya angani utawekwa angani ili kutumika kama mfumo wa onyo wa kurusha kombora. Vizuizi vitawekwa huko.
Tayari mnamo 2019, kulikuwa na mazungumzo kwamba mfumo huo ungeharibu makombora katika hatua ya kuongeza kasi linaposafiri kwa kutumia njia za kinetic na zisizo za kinetic, kama vile leza.
Hili liliwezekana kutokana na ujio wa satelaiti za gharama ya chini za obiti ambazo zinaweza kurushwa angani kwa wingi, na hivyo kuunda mtandao wa vyombo vya angani ambavyo vinaweza pia kufuatilia kurushwa kwa makombora.
Mbali na teknolojia mpya ambazo zimefanya uundaji wa vyombo vya anga vya juu kuwa nafuu zaidi, fursa mpya zimeibuka za kuvirusha kwenye obiti - kutokana na ujio wa roketi za kuingia tena, gharama ya kurusha vyombo hivyo imeshuka kwa kiasi kikubwa.
Ugumu hapa ni kwamba tutahitaji sio tu satelaiti za uchunguzi wa Dunia ambazo zitafuatilia vitu vilivyo ardhini, kama vile nyambizi au virutubishi vya rununu, lakini pia satelaiti ambazo zitafuatilia makombora ya masafa marefu (ICBMs) yakiruka na kutoa maelezo ya kuyashambulia.
Vizuizi
Kinasa cha kinetic ni kombora ambalo huharibu lengo kwa kuligonga kombora kwa kasi. Kwa kuwa tunazungumza juu ya kasi ya kweli, kwa kasi zaidi kuliko kasi ya sauti, athari itakuwa na mshindo, na nishati ya kinetic iliyotolewa itakuwa ya kutosha kuharibu lengo.
Hivi ndivyo, kwa mfano, roketi ya kizazi cha PAC-3 ya tata ya Patriot inavyofanya kazi. Hatahivyo ni vigumu kuzindua kombira hilo kwenye obiti. Roketi moja ya familia hii ina uzito zaidi ya kilo 300.
Ili kugonga lengo, unahitaji makombora mengi zaidi ya moja, na kwa hisabati tu, ikizingatiwa kwamba italazimika kuwekwa juu ya eneo kubwa sana, itakuwa vigumu sana .

Chanzo cha picha, Reuters
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wakati huo huo, kulingana na Fred Kennedy, mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Maendeleo ya Anga la Marekani na mkuu wa Ofisi ya Teknolojia ya Mbinu ya DARPA, Marekani tayari ina uwezo wa kutengeneza makombora ya kinetic ya kupenyeza angani yenye uzito wa kilo 80.
"Weka vipokezi sita katika sehemu ya obiti inayolingana na kifaa cha kurusha kombora kutoka ardhini cha MLRS na uiambatanishe na setilaiti ndogo kichwani mwake.
Rusha kati ya vibebaji hivi 21 kwenye roketi moja ya Falcon 9 (au roketi ya washindani sawa). Rudia hii mara 13 na utapata vizuizi 273 . Vipokezi sita vinaweza kuwa na uzito wa kilo 750 pekee - hiyo ni sawa na uzito wa satelaiti ya Starlink ya kizazi cha pili,".
Kwa upande mwingine, kama mhariri wa kijeshi wa Economist Shashank Joshi alivyobainisha katika mahojiano na BBC, kwa vile vizuizi vitakuwa katika obiti ya chini, watakuwa na masafa mafupi na muda mchache sana wa kufikia malengo yao.
"Utakuwa na dakika chache sana, kulingana na jinsi roketi inavyowaka kwa kasi. Na ikiwa unataka kusimamia eneo la ukubwa, tuseme, Korea Kaskazini na maeneo yake yote ya kurusha, bado utahitaji mamia na mamia ya satelaiti zenye vizuizi," alisema.
Upnade wa Urusi, idadi yao itakuwa kubwa zaidi.
Gharama
Trump alisema Jumanne mpango huo utahitaji uwekezaji wa awali wa dola bilioni 25 na utagharimu dola bilioni 175.
Dola bilioni 25 za awali, alisema, tayari zimejumuishwa kwenye "One Big Beautiful Bill on Taxes," ambayo bado haijapitishwa.
$175 bilioni ni makadirio rasmi ya gharama ya mpango huo, lakini Ofisi ya Bajeti ya Congress inakadiria kuwa mfumo wa kulinda anga wa Golden Dome unaweza kugharimu $524 bilioni kwa miaka 20.
Lakini hata kiasi hiki cha awali kinaweza kugeuka kuwa kidogo sana kuliko cha mwisho, kwani mifumo mingi bado inahitaji kuendelezwa.
Kukosa udhibiti
Ulinzi wa makombora wa Trump huenda ukavuruga mfumo uliopo wa kimkakati wa kuzuia nyuklia (SND).
Ni mkakati ambao umiliki wa silaha za nyuklia hutumika kama njia ya kuzuia shambulio la adui anayeweza kutokea.
Kanuni ya msingi ni uharibifu unaohakikishiwa pande zote mbili: ikiwa upande mmoja utatekeleza shambulio la nyuklia, upande mwingine utaweza kujibu kwa uharibifu kiasi kwamba gharama ya uchokozi inakuwa isiyokubalika.
Kwa miongo kadhaa, hii ilizuia USSR na USA, nguvu kubwa zaidi za nyuklia, kutoka kwa vita. Na kutokuwepo kwa vita, kwa msingi wa nguvu za kimkakati za nyuklia, kunaitwa utulivu wa kimkakati.

Chanzo cha picha, Getty
Utulivu huu ulihakikishwa sio tu na vikosi vya kimkakati vya nyuklia, lakini pia na mambo mengine mengi, pamoja na kupunguza mvutano na kuongezeka kwa joto la uhusiano kati ya USSR, na kisha Urusi na USA.
Na utulivu huu unavurugwa na mambo mengine, ikiwa ni pamoja na vita ambavyo Urusi inaendesha huko Ukraine, kuibuka kwa aina mpya za kimkakati za silaha, kama zile ambazo Vladimir Putin alizungumzia mnamo 2018.
Wakati wa Vita Baridi, programu za ulinzi wa makombora zilizingatiwa kuwa moja ya sababu za kudhoofisha utulivu wa kimataifa. Ukweli ni kwamba nchi iliyo na mfumo mzuri wa ulinzi wa makombora inaweza kutaka kuwa ya kwanza kushambulia , ikitegemea kwamba majibu dhaifu hayatashinda ulinzi wake. Adui atajaribu kushambulia kwanza ili kudhoofisha uwezo wa mfumo ya ulinzi.
Majibu ya Urusi
Urusi ilijibu hotuba ya Trump kwa kujizuia. Katibu wa vyombo vya habari wa rais wa Urusi Dmitry Peskov alisema kwamba uundaji wa mfumo wa ulinzi wa makombora wa Golden Dome ni biashara huru ya Marekani: "Ikiwa Marekani inaamini kuwa kuna tishio la kombora, basi, bila shaka, wanaunda mifumo ya ulinzi wa makombora."
Je, Urusi itajibu?
Moscow hakika itajaribu kujibu hatua za programu, na kuna fursa nyingi za hili.
Kwanza, idadi ya makombora ya masafa marefu ICBM inaweza kuongezwa. Hii ilizuiwa na mkataba wa START, ambao sasa umesitishwa.
Haijalishi ni vizuizi vingapi vilivyowekwa angani, kila kombora la ziada litahitaji ongezeko kubwa la idadi yao.
Hakuna mfumo uliopo wa ulinzi wa kombora ulimwenguni unaoweza kuzuia mashambulizi makubwa ya nyuklia, na kwa hivyo ni busara kudhani kwamba Urusi itajaribu, kwanza kabisa, kuongeza idadi ya wabebaji makombora
Kwa kuwa tunazungumza juu ya hatua ya awali, inawezekana kujenga sio tu makombora na vichwa vya nyuklia, lakini pia malengo ya uwongo - kutakuwa na wakati mdogo sana wa kuwatambua.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












