Je, haya ni mapinduzi? Prigozhin anafanya nini nchini Urusi?

 Picha ya maktaba ya Yevgeny Prigozhin akiwa na mamluki nchini Ukraini

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Picha ya maktaba ya Yevgeny Prigozhin akiwa na mamluki nchini Ukraini

Huu ni wakati muhimu katika vita vya miezi 16 vya Urusi nchini Ukraine na pengine changamoto kwa Vladimir Putin kung'ang'ania madaraka.

Ruis huyo wa Urusi amemshutumu kiongozi wa mamluki wa Wagner Yevgeny Prigozhin kwa uhaini, kuanzisha uasi wa kutumia silaha na "usaliti wa nchi yetu".

Prigozhin ambaye ni mmoja wa watu muhimu zaidi nchini Urusi, anasema lengo lake si "mapinduzi ya kijeshi lakini ni kupigania haki".

Nini kinaendelea?

Kwa miezi kadhaa Prigozhin imekuwa na jukumu muhimu katika operesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine, akiandikisha maelfu ya watu kwa kundi lake la mamluki la Wagner, hususan kutoka jela za Urusi.

Kwa muda mrefu amekuwa katika ugomvi wa wazi na wakuu wa kijeshi wanaoendesha vita, lakini sasa hilo limegeuka kuwa uasi.

Vikosi vya Wagner vimevuka kutoka mashariki mwa Ukraine inayokaliwa kwa mabavu na kuingia katika mji mkubwa wa Rostov-on-Don, kusini mwa Urusi, na kudai kuwa vimedhibiti vituo vyake vya kijeshi.

Rais Putin anasema hali ni ngumu lakini ameahidi kufanya kila awezalo kuitetea Urusi.

Je, haya ni mapinduzi?

Madai yote ya mapinduzi ya kijeshi ni upuuzi, anadai Prigozhin.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Lakini kile kilichoanza kama mzozo juu ya jeshi kushindwa kuwapa mamluki wake vifaa vya kutosha na risasi sasa kimeguka kuwa uhasama wa moja kwa moja kati ya watu wawili wanaosimamia vita vya Ukraine - Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na mkuu wa vikosi vya jeshi Valery Gerasimov.

Haya si mapinduzi, kwani hakujawa na jiribio lolote la kunyakua mamlaka kutoka kwa serikali. Lakini ni jaribio la kuwang'oa madarakani wakuu wa jeshi la Urusi na hivyo kuwa changamoto kwa mamlaka ya rais.

Jiji zima la Moscow limewekwa katika hali ya tahadhari chini ya "utawala wa operesheni ya kukabiliana na ugaidi" na matukio makubwa yameshuhudiwa kufuatia hatua hiyo.

"Kuna 25,000 kati yetu," Prigozhin alidai. "Kila mtu anayetaka, ajiunge nasi." Wito huo hautoshi kumtishia rais lakini ni changamoto kwa uongozi wa kijeshi.

Amehamasisha vikosi vyake kuvuka mpaka hadi Rostov, anaonekana kuzunguka makao makuu ya jeshi kutoka mahali ambapo vita vinaendeshwa, na anadai waziri na mkuu wa majeshi wamekimbia.

Ramani ya Urusi

Jinsi hali ilivyofikia hapa

Prigozhin kwa muda mrefu amekuwa mshirika wa karibu wa Rais Putin na amestawi chini yake, kwanza akiwa mfanyabiashara tajiri na kisha kama mkuu wa kundi la mamluki.

Wapiganaji wa Wagner wamekufa kwa wingi katika makabiliano makali ya kuiteka Bakhmut mashariki mwa Ukraine, ambayo ilidumu kwa miezi kadhaa na hayakufanikiwa kikamilifu.

Prigozhin alilaumu wakuu wa kijeshi kwa uhaba wa makombora, akiweka mitandaoni video za zinazofichua mapungufu ya jeshi la Urusi nchini Ukraine.

Hakuelekeza moja kwa moja hasira yake kwa rais, lakini kauli yake ya kejeli kwa "babu mwenye furaha" yalionekana kama ukosoaji usio wa moja kwa moja.

Mwezi uliopita aliuliza jinsi Urusi inaweza kushinda ikiwa "huyu mwasisi hana maana kabisa"

CONCORD PRESS SERVICE

Chanzo cha picha, CONCORD PRESS SERVICE

Na hapo jana Juni 23, aliwaambia Warusi kwamba vita vyao havina msingi wowowte na kwamba ilikuwa uongo na kisingizio tu cha "kundi dogo la wahuni" kujitangaza na kudanganya umma na rais.

Tangu wakati huo hali imeendelea kubadili kwa haraka sana.

Prigozhin alishutumu jeshi kwa kuwashambulia watu wake huko Ukraine, lakini jeshi lilikanusha na hanjatoa ushahidi wowote kama anavyofanya mara kwa mara.

Mwishoni mwa Ijumaa alitangaza "hatua yake ya kupigania haki" yalikuwa yanaendelea. Wapiganaji wake 25,000 ni "akiba ya kimkakati" tu na jeshi lote na nchi nzima itakuwa hifadhi yao ya kimkakati.

Jenerali Sergei Surovikin, naibu kamanda wa vikosi vya Ukraine, alimwomba arudi nyuma na kutii mamlaka ya Rais Putin.

Lakini kufikia asubuhi wapiganaji wa Prigozhin walikuwa wamefika Rostov: "Tuko ndani ya makao makuu ya [kijeshi]."

Wakati wa changamoto kwa Putin na Urusi

Hatua hii sio changamoto ya moja kwa moja dhidi ya vita vya Urusi nchini Ukraine au uongozi wa rais.

Lakini ni jambo kubwa kiasi cha kumfanya kiongozi huyo wa Urusi kutoa hotuba kwa taifa kwa dakika tano.

Prigozhin ametishia sio tu kuweka kambi huko Rostov, lakini kuelekea Moscow ikiwa matakwa yake ya kijeshi hayatatekelezwa.

Amekuwa akizozana na uongozi wa kijeshi juu ya uhaba wa silaha, sasa amechukua uongozi wenyewe.

Prigozhin ana uungwaji mkono mkubwa wa umma nchini Urusi na, hata kama juhudi yake itasambaratika, huu si wakati wa jeshi kuingia kwenye mgogoro na mamluki wanaotegemea nchini Ukraine.

Lakini huu pia ni wakati muhimu kwa uongozi wa Putin na wito wa muamko kwa Warusi. Ni mapema sana kusema mzozo huuu utaishia wapi.