Tazama kilichotokea baada ya ndege za kivita za China na Marekani kukutana angani

Jeshi la Marekani limetoa video inayoonyesha ndege ya kivita ya China iliyogongana na ndege ya kivita ya Jeshi la Anga la Marekani.

Rubani wa ndege ya kivita ya China alifikia mita 121, ambayo ilikuwa karibu sana na ile ya Marekani.

Ndege ya kivita ya Marekani ilipogundua kuwa ndege hii ya China ilikuwa karibu sana, ilisababisha kuyumba.

Vikosi vya Marekani katika eneo la Indo-Pacifiki vilisema kwenye taarifa yake ya pamoja kwamba marubani wa Marekani walikuwa katika anga ya kimataifa wakati huo.

Wiki chache baada ya Rais wa Marekani kutuma onyo kwa China kuhusu Taiwan, serikali ya Beijing ilitoa jibu kali zaidi kuwahi kutokea.

Marekani na China zina mivutano ya kisiasa hasa kuhusu Taiwan ambayo Marekani inaiunga mkono.

Uchina inaitambua Taiwan kama sehemu yake lakini Taiwan imetangaza uhuru na inataka kuwa nchi huru inayotambuliwa na ulimwengu.

Marekani na China mara nyingi zimebadilishana vita vya maneno na vitisho vikali.

Tazama kilichotokea kati ya ndege hizo mbili za kivita:

Marekani

Marekani ina jumla ya wanajeshi milioni 1.4. Wakati jeshi la wanamaji linasemekana kuwa 346,200.

Jeshi la Wanamaji la Marekani lina nyambizi 51 zinazobeba vichwa vya nyuklia na meli za kivita 11. Kwa jumla, Jeshi la Wanamaji la Marekani lina meli za kivita 296.

Jeshi la Anga la Marekani lina utaalam wa vita vya anga.

Ilianzishwa mnamo Septemba 1947, chini ya Sheria ya Usalama wa Kitaifa ya 1947, na wakati huo ilikuwa moja ya vikosi vipya vya jeshi la Marekani.

Ndege nyingi za Jeshi la Anga ni F-16C Falcons, nambari 783.

Jeshi la anga la Marekani lilikuwa na ndege 4,100 zilizo tayari kupambana.

Kwa kuongezea, Jeshi la Anga la Marekani lina makombora 400 ya balestiki ya mabara.

Idadi ya wafanyikazi wa akiba katika Idara ya Ulinzi ya Marekani imebaki thabiti tangu 1995. Mnamo 2020, kikosi cha akiba kilikuwa 795,955.

China

Tathmini iliyofanywa na gazeti la Businessinsider linalonukuu tovuti ya Statista mwaka 2022 ilisema kuwa China ndiyo nchi yenye wanajeshi wengi zaidi duniani, huku wanajeshi wake wakifikia milioni 2.18.

Mnamo Oktoba 2019, China ilifanya mazoezi yake ya hivi karibuni ya kijeshi.

Ilikabidhiwa jeshi la askari 15,000, zana za kijeshi 580 na ndege 160 za kivita.

China ni nchi ya pili kwa matumizi makubwa ya kijeshi, inatumia dola bilioni 261 kila mwaka, kulingana na Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Kimataifa ya Stockholm.

China ni nchi ya tatu kwa ukubwa kwa uwezo wa ndege za kivita, ikiwa na ndege 3,210.

China has 3,200 tanks and 33,000 armored vehicles, according to data published by Global Firepower, a website that compares the military strength of countries around the world.

China ina vifaru 3,200 na magari 33,000 ya kivita, kulingana na data iliyochapishwa na Global Firepower, tovuti ambayo inalinganisha nguvu za kijeshi za nchi duniani kote.

China ina mifumo ya kurusha roketi kwenye makombora 2,650. Kwa upande wa nguvu za majini, China ina vyombo vya majini 777 vya aina mbalimbali, manowari 74 na meli za kivita maarufu kama destroyer, 36.