'Safari yangu kutoka unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi hadi kuwa tajiri wa nyumba'

Chanzo cha picha, A&O STUDIO
Na Dougal Shaw
BBC News
Sanmi Adegoke hakuwa na mawasiliano yoyote katika ulimwengu wa sekta ya ujenzi wa nyumba. Katika tasnia ambayo kuna Wakurugenzi Wakuu wachache sana weusi, alipata mafanikio kama mgeni kwa kutumia mawasiliano ya kipekee aliyokuwa nayo, wakati akijenga kampuni yake mwenyewe tangu mwanzo.
Alipowasili Uingereza kutoka Nigeria akiwa kijana na wazazi wake katika miaka ya mapema ya 2000, Sanmi Adegoke alikumbana na ubaguzi wa rangi mapema.
Katika kazi yake ya kwanza, akifanya kazi katika kampuni ya vyakula vya haraka ya McDonald's kusini mwa jiji la London, anasema baadhi ya watu wangemjia na kutumia lugha za kibaguzi dhidi yake.
“Au nyakati fulani wangesema, ‘Hapana, sitaki unihudumie’” anakumbuka. "Na ilinibidi kuishi na hali hiyo."
McDonald's ilikuwa haiwavumilii wateja hawa, lakini imani yake ya Kikristo ndiyo iliyompa nguvu ya kukabiliana na unyanyasaji huo. "Ningewaambia watu hawa, 'Yesu anampenda kila mtu - ninyi ni wajinga tu."
Bw Adegoke alifanya kazi McDonald's, hadi kufikia wadhifa wa usimamizi.
Mfanyakazi mwenzake, ambaye alijua kwamba alikuwa mjasiriamali, alimpa kitabu ambacho kilikuwa na athari ya kudumu kwake. Rich Dad, Poor Dad by Robert T Kiyosaki , ninachozungumzia kuwekeza katika mali kama vile mali isiyohama ili kupata maendeleo katika jamii.
Kitabu hicho kilimtia hamasa na baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, alianza kuwekeza katika soko la nyumba nchini Uingereza, kununua na kuuza gorofa ambazo zinapangwa kuuzwa (kabla ya kujengwa).
Ingawa alipata mafanikio makubwa wakati wa msukosuko wa kifedha wa 2008, kufikia 2013 alikuwa amepata pesa za kutosha kuanzisha biashara yake ya Rehoboth Property Group.

Chanzo cha picha, SANMI ADEGOKE
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Lakini biashara ya nyumba inategemea sana ni nani unayemjua.
"Ni vigumu kuingia ikiwa huna wa kukuunganisha," anaelezea Priya Aggarwal-Shah, mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika la BAME in Property. "Fursa za mtandao huja kwa urahisi zaidi kwa wale kutoka asili fulani, wanaopenda gofu, na raga, kuteleza kwenye barafu na kunywa pombe, kwa mfano."
Kwa kuwa bado hakuwa na mawasiliano yoyote katika ulimwengu wa biashara ya nyumba, Bw Adegoke aliamua kutumia mawasiliano hayo aliyokuwa nayo - katika ulimwengu wa jumuiya za kidini za watu weusi za London.
Huko Nigeria alikuwa mshirika wa kikundi cha kanisa tangu akiwa na umri wa miaka mitano, na alipokuja London alijiunga na kusanyiko la kidini linalofanana na lake.
Kumekuwa na kupungua kwa kasi kwa kwa idadi ya watu wanaohudhuria ibada mkanisa nchini Uingereza katika miongo michache iliyopita. Kanisa la la Kianglikana limeuza mali zake nyingi pole pole , mkiwemo makanisa.
Lakini kusini mwa London watu bado watu wanasali, hasa kwa sababu ya wahamiaji kama Bw Adegoke. Yinakadiriwa kuwa kuna makanisa 250 yanayohudhuriwa na watu weusi kusini mwa London huku maelfu ya watu wakiabudu kila Jumapili.
Bw Adegoke aliendeleza biashara yake kwa kukarabati maeneo ya zamani ya burudani yaliyojengwa baada ya vita, na kuyageuza kuwa mahali pa kuabudu.

Miradi ya awali ilijumuisha kugeuzwa - kwa jumba la bingo huko Camberwell, London kusini, na Mahakama ya Woolwich, kuwa sehemu za vikundi vya kidini.
Kisha alipanua himaya yake ya umiliki wa utaalam katika kupanga upya na kukarabati mchanganyiko tofauti zaidi wa majengo, akageuza maeneo kama vile baa na vituo vya polisi vya zamani kuwa mahala pa kufanya kazi pamoja, kumbi za jumuiya na kumbi za matukio.
Kikundi chake cha Rehoboth sasa kimefanya miradi mikubwa zaidi ya 20 ya ukarabati na kina mali ya thamani ya pauni milioni £35 chini ya usimamizi wake, na zaidi ya wafanyakazi 20.
Mafanikio ya Bw Adegoke kama Mkurugenzi Mtendaji wa mali yanamfanya kuwa kitu cha nje. Kwa miaka mingi tasnia ya mali ya Uingereza imetambua kuwa ina suala la utofauti na kukuza talanta.
Ripoti ya mwaka jana ya shirika la ushauri la Action Sustainability ilibaini kuwa watu kutoka makabila madogomadogo waliunda 13.6% ya wafanyakazi wa kampuni zilizounganishwa na mazingira ya ujenzi. Hii ilikuwa bora zaidi kuliko takwimu ya 1.2% ya uchunguzi mwingine mkuu wa Taasisi ya Kifalme ya Wakaguzi walioidhinishwa iliyopatikana mwaka wa 2016, l ambayo bado iko chini ya kielelezo cha ONS cha 18.5%.
End of Unaweza pia kusoma:

Chanzo cha picha, Rehoboth
Gazeti la masuala ya makazi ( Estates Gazette,) ambalo hutoa data na uchanganuzi kwa soko la nyumba za biashara, liligundua katika uchunguzi wake wa 2021 kuwa 84% ya washiriki kutoka watu wa jamii za walio wachache waliona kuwa ubaguzi wa rangi ni tatizo kazini, huku 75% wakisema wameupitia.
"Tuna hamu hii ya kumiliki nyumba katika nchi hii na hii inaashiria tasnia, kwa sababu mali inahusu uhusiano," anasema Bi Aggarwal-Shah. "Unawaamini watu wenye kiasi kikubwa cha pesa, kwa hivyo upendeleo wetu wa asili wa mshikamano unaingia - tunataka kufanya kazi na watu sawa na sisi."
Anadai hii ndiyo sababu watu wengi kutoka jamii za walio wachache wanaofanya kazi katika sekta hiyo, kama Bw Adegoke, huishia kuanzisha kampuni zao za kumiliki nyumba.
“Ndoto yangu ya kibiashara iliwezekana kwa sababu nilianza na kile nilichokifahamu,” anaeleza Bw Adegoke.
"Mchakato wa mabadiliko unajengwa hatua kwa hatua," anaongeza. Anaamini watoto wake hawatalazimika kukumbana na aina kama hiyo ya ubaguzi wa rangi aliofanya katika kipindi cha miaka 20.
"Kwa kweli, hadithi yangu itawaambia - unaona mtu huyo ambaye alikuwa akifanya kazi McDonald's? Angalia kile alichokifanya."
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












