Familia ya msichana mweusi wa Ireland aliyebaguliwa yasema msamaha 'hauna maana'

Maelezo ya video, Familia ya msichana mweusi wa Ireland aliyebaguliwa yasema msamaha 'hauna maana'
Familia ya msichana mweusi wa Ireland aliyebaguliwa yasema msamaha 'hauna maana'
g

Mama wa msichana mweusi ambaye hakupewa medali katika sherehe ya michezo ya sarakasi nchini Ireland anasema msamaha aliopokea "hauna maana".

Video iliibuka hivi karibuni ikionyesha madai ya ubaguzi wa rangi ya kijana mweusi akipuuzwa na afisa ambaye alikuwa akigawa medali katika hafla iliyofanyika mjini Dublin mwaka jana.

Mama huyo alisema kuwa kutazama tukio hilo wakati huo ilikuwa "tisho".

Taasisi ya michezo ya viungo -Gymnastics Ireland iliomba msamaha "kwa hasira ambayo iliyosababishwa" na tukio hilo.