Tunachokifahamu kuhusu shambulizi la Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia nchini Iran

Muda wa kusoma: Dakika 7

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba ndege za kijeshi za Marekani zimerusha mabomu katika maeneo matatu yaliyo na vituo vya nyuklia nchini Iran, hali ambayo inaweka shinikizo kubwa katika mzozo kati ya Iran na Israel ambao unaendelea kwa sasa.

'Kumbuka, kuna maeneo mengi yaliyosalia ambayo bado tunaazimia kuyalenga. Usiku huu, umekuwa mgumu sana katika muda huu wote, na huenda umeshuhudia shambulizi kali na hatari zaidi,' alisema Rais Trump alisema katika hotuba kwa taifa la Marekani kwenye televisheni.

'Lakini ikiwa amani haitokuja kwa haraka basi tutalenga vituo vingine kwa ujuzi mkubwa, haraka na umakini.'

Mojawapo ya vituo vilivyolengwa ni kile cha Fordo - ambapo madini ya Urania yanaratibishwa – ambacho kiko kwenye eneo la milimani nchini Iran na ambacho kinatajwa kama eneo muhimu zaidi katika azimio la mpango wa kinyuklia wa Iran. Hatuna taarifa kamili kuhusu hasara iliyopatikana katika kituo hicho.

Mamlaka nchini Israel zimesema kwamba serikali ya taifa hilo inashirikiana kabisa na Marekani katika mipango yake ya kutekeleza mashambulizi hayo.

Kwa mujibu wa shirika la Habari la Marekani la CBS ambalo ni mshirika wa BBC , Marekani iliwasiliana na Iran kupitia njia za Kidiplomasia Jumamosi kuwaarifu kwamba mashambulizi ya angani yalikuwa yanalenga kuharibu vituo vya Kinyuklia na kwamba hawana mpango wa kuondoa uongozi wan chi hiyo.

Iran huenda ikajibu shambulizi la Marekani kwa kulenga kambi za kijeshi za Marekani zilizopo katika ukanda wa mashariki ya kati. Maafisa wa serikali hiyo wameonya kwamba shambulizi lolote kutoka Marekani linaweza kuchangia vita vikubwa katika ukanda huo na kwamba wanaweza kulipiza kisasi.

Huu hapa utaratibu wa kila tunachokifahamu kwa sasa:

Operesheni hii ilianza vipi?

Israel ilitekeleza shambulizi dhidi ya vituo kadhaa vya kinyuklia na kambi za kijeshi nchini Iran Juni 13. Ilisema kwamba azimio lake lilikuwa kuharibu mpango wa kinyuklia nchini humo, ambao Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema katika siku za usoni ungeweza kutengeneza mabonu ya kinyuklia.

Iran imesisitiza kwamba mpango wake wa Kinyuklia ulitarajiwa kuwa wa amani tu. Na muda mfupi baadaye, Tehran ilijibu mashambulizi hayo kwa kurusha makumi ya makombora kulenga Israel. Mataifa hayo mawili yameendelea kushambuliana kwa kurusha makombora angani tangu hapo, katiika vita ambavyo vimeendelea kwa zaidi ya wiki moja sasa.

Trump amekuwa akisema kwa muda mrefu sasa kwamba hakubaliani na mpango wa Iran kumiliki silaha ya kinyuklia. Israel imesemwa kwamba ina aminiwa kumiliki silaha hizo, japo haijathibitisha wala kukanusha.

Mwezi Machi, Mkurugenzi wa idara ya ujasusi nchini Marekani Tulsi Gabard, alisema kwamba japo Iran ilikuwa imeongeza madini ya Urania inayomiliki, haikuwa inatengeneza mabomu ya kinyuklia – tathmini ambayo Rais Trump alisema haikuwa ya kweli.

Katika kampeni yake, Rais Trump aliwakosoa baadhi ya maafisa wa serikalini nchini Marekani kwa kujihusisha na 'vita visiyokuw ana msingi kwa muda usiojulikana' katika eneo la Mashariki ya kati na kuahidi kutoihusisha Marekani katika mizozo ya mataifa ya kigeni.

Marekani na Iran walikuwa wanafanya mazungumzo ya kudhibiyi mfumo wa kinyuklia wakati ambapo shambulizi hili la ghafla lilipotekelezwa. Ni siku mbili tu zilizopita ambapo Trump alisema kwamba angefanya uamuzi wake na kuipa Iran siki mbili kabla dunia kujuwa ikiwa jeshi la Marekani lingeingilia vita hivi – lakini muda huo umefupishwa mno.

Jeshi la Marekani limerusha mabomu wapi na limetumia silaha gani?

Fordo imefichiki kwenye milima iliyopo kusini mwa Tehran na inaaminiwa kuwa umbali mkubwa chini ya ardhi kuliko kivukio kinachounganisha Uingereza na Ufaransa chini ya ardhi.

Umbali wa kituo cha Fordho chini ya ardhi umekuwa changamoto kubwa na kuitatiza Israel kuifikia kwa kutumia silaha zake. Ni Marekani pekee ambayo imesemekana kuwa na mabomu maalum yenye uwezo wa kufikia na kuharibi mahandani yanayozuia uharibifu mkubw awa mabomu na yenye uwezo mkubwa wa kufikia meeneo yaliyo mbali kama Fordo.

Bomu hilo la Kimarekani linafahamika kama GBU-57 Massive Ordnance Penetrator (MOP). Lina uzani wa kilo 13,000 na lina uwezo wa kupenyeza na kuharibu mita 18 za saruji au mita 61 za udongo wa ardhi kabla ya kulipuka kw amujibu wa wataalamu.

Mashimo ya handaki la Fordo, yanaaminiwa kuwa takriban mila 80 hadi 90 kwa umbali chini ya ardhi, kwa hivyo bomu la aina ya MOP halidhaniniwa kuwa na uwezo wa kufanikiwa kufikia eneo hilo, ila ndilo bomu la pekee lenye uwezo wa kujaribu kutekeleza jukumu hilo.

Maafisa wa Marekani wametjibitisha kwa kituo cha Habari cha CBS kwamba mabomu ya aina ya MOP ndiyo yaliyotumika kwenye shambulizi la Marekani mapema leo, ambapo mbili zilirushwa kwa kila kituo kilicholengwa.

Jinsi ambavyo Mabomu ya kuharibu mahandaki ya Marekani yanayvyofanya kazi

Mobu la aina ya GBU-57 Massive Ordnance Penetrator

  • Bomu linarushwa kutoka kwa ndege ya kivita ya aina ya B-2 Stealth kutoka umbali wa kilomita 12 juu ya eneo linalolengwa.
  • Bila ya kuwa na injini, ni umbali wa juu ya anga ambao unawezesha bomu hilo kupata kasi inayohitaji kushuka ardhini.
  • Bomu hilo linaongozwa na satelaiti inayodhibiti mkia wake.
  • Uzito mkubwa wa bomu hilo husababisha kiwango kikubwa cha nishati inayoleta hasara kubwa kivita.
  • Nguvu hii ya nishati inaisukuma chum hiyo nzito kwa umbali wa mita 60 chini ya ardhi.
  • Mwisho, fyuzi iliyomo ndani inalipuwa vilipuzi vyenye uzito wa kilo 2,400.

Athari ya shambulizi hili nig ani kwa Iran?

Haijabainika wazi kwa sasa thari ya shambulizi la Marekani katika vituo vya kinyuklia nchini Iran, au ikiwa kuna majeraha yeyote au maafa.

Naibu mkurugenzi wa masuala ya kisiasa nchini Iran Hassan Abedini amaiambia kituo cha Habari cha kitaifa nchini humo kwamba Iran ilikuwa imewaondoa watu kwenye vituo hivyo vitatu muda mrefu uliopita.

Akizungungmza kwenye kituo hicho kinachomilikiwa na serikali, Abedini amesema kwamba , Iran haikupata hasara kubwa kwa sababu bihdaa zilizokuwa katika maeneo hayo tayari zilikuwa zimeondolewa.

Katika hotuba yake ya televisheni kwa taifa, Trump amesema kwamba vituo vya kurutibisha madini ya Urania yameharibiwa kabisa.

Lakini akizungumza na BBC, aliyekuwa Naibu Waziri wa mambo ya kgeni wa Marekani Mark Kimmitt, alikuwa mwenye kutotaka kuchukuliwa kwa hatua hiyo.

'Hakuna njia ya kusema kwamba vituo hivyo vimeharibiwa kabisa,' alisema.

Iran imesema kwamba zaidi ya watu 200 wameuawa tangu makabiliano ya hivi maajuzi kuanza kati ya Israel na Iran huku wengine 1200 wakijeruhiwa.

Wakati huo huo, Israel inadhibiti usalama wake wakati baada ya shambulizi la Marekani dhidi ya vituo muhimu vya Kinyuklia nchini Iran.

Israel imekaza usalama wake na kuweka vikwazo zaidi vya kiusalama kote nchini, kw amujibu wa jeshi la Israel (IDF).

Hatua hiyo – inayojumuisha kufunga shule na kukataza mikusnyiko ya watu na ha hata kuwazuia watu kutoka nje kwa ajili ya kuenlekea kazini – imetolewa muda mfupi tu baada ya shambulizi hilo la Marekani.

Iran inaweza kujibu vipi shambulizi hilo?

Iran imelemezwa pakubwa na mashambulizi ya Iran yaliyolenga kambi zake za kijeshi kwa mujibu wa wataalamu, na vile vile Israel imefanikiwa kulemaza shughuli za makundi ya wapiganaji ambayo yaliungw amkono na Iran kama vile Hezbollah nchini Lebanon, na Hamas nchini Syria na Gaza. Lakini Iran bado ina uwezo wa kutekeleza uharibifu mkubwa.

Maafisa wa serikali ya Iran wameonya Marekani dhidi ya kuingilia kati, wakisema kwamba taifa hilo lingekabiliwa na uharibifu ambao hauwezi kurekebishwa na kwamba inakumbw ana tishio la kuzuka kwa vita vikuu katika ukanda wa mashariki ya kati.

Iran aidha imetishia kulenga kambi za jeshi la Marekani katika ukanda huo. Marekani ikon a kambi kadhaa za kijeshi katika maeneo 19 ya Mashariki ya kati, ikiwemo Bahrain,Misri, Iraq, Jordan,Kuwait, Qatar,Saudi arabia na katika Falme za Milki za Kiarabu.

Mojawapo ya maeneo ambayo huenda yakalengwa na Iran ni Makao makuu ya kivita ya jeshi la majini la Marekani la 5th Fleet iliyopo Mina Salman huko Bahrain.

Inaweza pia kulenga njia muhimu ya usafiri wa majini inayofahamika kama Strait of Hormuz ambayo inaunganisha ghuba ya Persia na Bahari Hindi ambapo asilimia 30 ya mafuta inayotumika duniani hupitia.Aidha hali hii pia inaweza kuathiri njia nyinginezo za uchukuzi wa majini ambazo Iran ina uwezo wa kulenga na kutatiza soko la kitaifa.

Iran huanda pia kulenga maeneo au vituo vinavyomilikiwa na Marekani au mataifa Jirani ambayo inahisi yanaisaidia Marekani , hali ambayo inatishia kuvuja kwa vita katika ukanda mzima.

Je, Trump anahitaji idhini ya bunge la Makrekani kuvituma vikosi vya Marekani vitani?

Sheria za Marekani zina ipa Bunge la kitaifa na seneti nchini humo uwezo wa kumpa Rais idhini ya kuchukuwa hatua ya kuishambulia taifa lingine.

Lakini pia, sheria inasema kwamba Rais ambaye ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Marekani ana uwezo wa kuvituma vikosi vyake katika majukumu ya kijeshi bila ya kutangaza vita vya moja kwa moja.

Baadhi ya wabunge wa vyama viwili vikuu bungeni wamejaribu kudhibiti uwezo wa Trump kutoa amri ya jeshi la Marekani kuingia vitani kwa kupendekeza masuala kadhaa katika bunge la kitaifa kuifanya hatua hiyo kuchukuwa wiki kadhaa kabla ya kutekelezwa kwa kuw aitahitaji kura kupigwa bungeni.

Imetafsiriwa na Laila Mohammed