Tetesi za soka Ulaya Jumanne: Grealish kuondoka Man city

Grealish

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Grealish
Muda wa kusoma: Dakika 2

Winga wa Uingereza wa Manchester City, Jack Grealish, 29, huenda akawa mbadala wa kiungo wa Ujerumani Florian Wirtz, 22, endapo ataondoka Bayer Leverkusen. (Sun)

Mshambuliaji wa Sweden Viktor Gyokeres anahasira na klabu yake Sporting ambayo imemgeuka kwenye makubaliano ya heshima kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 angeweza kuondoka msimu huu wa joto kwa pauni milioni 67. (Record)

Manchester City wamekubaliana mpango wa pauni milioni 34 na Lyon kwa ajili ya kiungo wa Ufaransa Rayan Cherki, 21. (Times)

Arsenal kumsajili kipa wa Chelsea wa Hispania, Kepa Arrizabalaga, 30, kwa pauni milioni 5 tu. (Sky Sports)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Antoine Semenyo

Tottenham wameongeza nia yao kwa Antoine Semenyo wa Bournemouth, huku Manchester United pia wakiendelea kumshawishi mshambuliaji huyo wa Ghana, 25. (Sky Sports)

Burnley wanataka pauni milioni 50 kwa ajili ya beki wao wa kati kutoka Ufaransa, Maxime Esteve, 23, kwa huku kukiwa na nia kutoka Bayern Munich, ambao wako chini ya kocha wa zamani wa Clarets, Vincent Kompany. (Football Insider)

Winga wa Ufaransa wa Paris St-Germain, Bradley Barcola, 22, ndiye chaguo la kwanza la Bayern kwa usajili mpya wa winga msimu huu wa joto, huku winga wa Hispania wa Atletico Madrid, Nico Williams, 22, akiwa mbadala ikiwa watamkosa Barcola. (Sky Sport Germany)

PSG wanamtaka Ilya Zabarni wa Bournemouth lakini Cherries wanadai pauni milioni 59 kwa beki huyo wa kati kutoka Ukraine mwenye umri wa miaka 22. (L'Equipe)

Mohammed Kudus

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mohammed Kudus

Newcastle United wanataka kumsajili winga wa Ghana, Mohammed Kudus, 24, kutoka West Ham baada ya kumkosa Bryan Mbeumo wa Brentford. (Football Insider)

West Ham wanazingatia mpango wa kubadilishana wachezaji na Chelsea unaomhusisha Kudus, huku Hammers wakiwa tayari kumruhusu beki wa kati wa Morocco, Nayef Aguerd, aondoke msimu huu wa joto kwa pauni milioni 25. (Teamtalk)

Manchester City wako tayari kumsajili kipa wa England wa Chelsea, Marcus Bettinelli, 33, kufuatia kuondoka kwa Scott Carson. (Telegraph)

Tottenham ni moja ya vilabu vya hivi karibuni kuonyesha nia kwa winga wa Mali wa Red Bull Salzburg, Dorgeles Nene, 22. (Teamtalk)