China inarekebisha jeni : Ni kwanini dunia ina wasi wasi?

Chanzo cha picha, TEK IMAGE/SCIENCE PHOTO LIBRARY
Wanasayansi wanaamini kwamba magonjwa ya urithi yanaweza kutokomezwa kwa usaidizi wa urekebishaji wa vinasaba (DNA) au kwa mbinu za kuhariri jeni za urithi.
Mtaalamu wa ngazi ya juu anaonya kuwa sheria mpya za China za kuthibiti jeni za binadamu sio kali vya kutosha.
Joy Zhang kutoka Chuo kikuu cha Kent, nchini Uingereza, mtaalamu wa udhibiti wa uhariri wa jeni nchini China, amesema kuwa maafisa wanatakiwa "kupunguza udhibiti " wa sekta ya uhariri wa jeni.
Miaka mitano iliyopita, baada ya mwanasayansi wa Uchina kuzalisha kwa mara ya kwanza watoto wenye jeni zilizorekebishwa, sheria zinazoongoza sekta ya uhari wa jeni zilirekebishwa.
China inasema kwamba sheria mpya zinaendana na matakwa ya kimataifa.
Sheria hizi zinahitaji mabadiliko ya maumbile ya jeni kuidhinishwa kimaadili, kudhibitiwa na kuhakikiwa, lakini wataalamu wana wasi wasi kwamba huenda sheria hizi zisiifae sekta binafsi.
Dkt. Zhang, mmoja wa wazungumzaji wakuu katika kikao cha kimataifa kuhusu marekebisho ya maumbile ya jeni za binadamu mjini London, aliiambia BBC News: Hofu yangu kuu ni kwamba sheria mpya hazitayahusisha mashirika binafsi ya kimataifa " , ambayo yanatafuta suluhu za magonjwa ya kudumu kando na taasisi za kawaida za kisayansi zinazofahamika."
"Sheria mpya huenda zisiendane na kasi ya uvumbuzi nchini China ."
Marekebisho ya jeni yanayofahamika kama (Genetic modification) ni mbinu mpya inayowaruhusu wanasayansi kufanya mabadiliko fulani ya kipekee katika vinasaba (DNA).
Wanasayansi wanaamini kwamba magonjwa mengi ya urithi yanaweza kutokomezwa kwa usaidizi wa mbinu hii.
Hatahivyo, licha ya hili, limesalia kuwa suala tata kwasababu ya uwezekano wa kufanya mabadiliko ya kudumu ya muundo wa mtu kutoka kizazi hadi kizazi.
Suala la uzoefu
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Miaka mitano iliyopita, wakati Dkt. He Jiankui kutoka Shenzhen, katika jimbo la Guangdong ,alitangaza kuwa amejifungua mapacha wa kwanza wa dunia ambao jeni zao zimerekebishwa, Lulu na Nana, wanasayansi wa ngazi ya juu katika sekta hii walishituka.
Vinasaba (DNA) vya watoto hawa wa kike vilibadilishwa mapema wakiwa bado vijusi. Kulingana na Dkt. Han, hii inapaswa kuwafanya wasipate maambukizi ya virusi vya HIV.
Mnamo mwa 2019, alipigwa faini na kufungwa kwa miaka mitatu.
Hakuna yeyote aliyewahi kuwaona mapacha hao isipokuwa daktari. Lakini katika mkutano wa sayansi uliopita, alisema afya yao ni nzuri.
Baada ya kuachiliwa kwake mwezi uliopita, ilifichuliwa kwamba anataka kufungua kliniki mjini Hong Kong kwa ajii ya kufanya utafiti kwa ktumia uhariri wa jeni kuwatibu watoto wenye ugonjwa wa urithi wa misuli unaoitwa Duchenne muscular dystrophy.
Maafisa wa uhamiaji walitangaza kuwa kibali chake cha kusafiria - Viza imefutwa baada ya kugundulika kuwa alikuwa na rekodi ya uhalifu.

Chanzo cha picha, HE JIANKUILAB
Sheria mpya zinafunga mianya ambayo awali Dkt. Hega aliitumia kufanya majaribio kwa ajili ya binadamu ambayo hufanyika kwenye hospita, kama vile majaribio ya dawa.
Sheria mpya zitatumiwa katika taasisi zote za utafiti wa kisayansi na kila kitu kinachohusiana na binadamu – tishu, viungo vya ndani ya mwili, na seli za viini tete.
Mwandalizi wa mkutano wa Kent, Profesa Robin Lovell-Badge wa taasisi ya Crick, ambako mkutano unafanyika, alisema kuwa ana hofu kuwa kuna usiri mkubwa katika utafiti nchini China.
"Ninaelewa ni kwanini China inataka kuongoza katika sekta hii ya teknolojia, lakini kuna maeneo ambayo yanahitaji umakini wa kipakee, na uhariri wa jeni ni mojawapo," alisema
Akizungumza katika mkutano , Dkt. Yangying Peng kutoka taasisi ya Academy of Sciences alisema kuwa serikali ina sheria na kanuni kuhusu uhariri wa jeni za urithi.
"China imeimarisha pakubwa sheria na kanuni zake," alisema. "Mabadiliko ya kudumu ya jeni yamezuiwa, uongozi unalishugulikia suala hili kwa tahadhari, na sheria zinaendana na kanuni za kimataifa ."

Chanzo cha picha, SPL
Dkt. Françoise Bayliss, mtaalamu wa maadili ya athari za utafiti wa sayansi ya tiba katika Chuo kikuu cha Dalhousie, anasema angependa kujua zaidi kuhusu kanuni mpya nchini uchina kuhusiana na urekebishaji wa jeni.
"Niliona [katika sheria zilizorekebishwa] kwamba watafiti wanatakiwa kutekeleza kanuni za kimaadili. Lakini ningependa kujua ina maanisha nini kwa misingi ya maadili," alisema.
Aliongeza kuwa China sio nchi pekee inayohangaika kudhibiti sekta binafsi.
"Amerika Kaskazini, pia tuna matatizo sawa na hayo, kwahivyo, ninafikiri sio sahihi kuiangazia china pekee," alisema.
Dkt. Pierce Millett, ambaye ni mwakili wa taasisi ya kimataifa ya masuala ya usalama wa kibaiolojia (Biosafety and Biosecurity Initiative) yenye makao yake mjini Washington alisema: "China inaweza kuongoza katika kurekebisha upya kanuni katika sekta hii."

Chanzo cha picha, SEBASTIAN KAULITZKI/SCIENCE PHOTO LIBRAR
Wanasayansi wengi walishangaa ni vipi Dkt. He aliruhusiwa kurejea katika utafiti wa kimatibabu baada ya kufungwa.
"Mimi, sawa na wengine tunashangaa, iwapo kulikuwa na mtu au shirika lolote nchini China ambalo lilimuunga mkono au kumtetea He Jiankui," alisema Dkt. Zhang.
Lakini kulingana naye, anadhani kwamba tunaona "mfano rahisi wa uzembe katika utaratibu wa udhibiti".
"Wakati ambapo kisa cha Dkt. He hakiko wazi, mazungumzo ya hivi karibuni kuhusu utawala bora ni unafiki ," alisema.
"Nina wasi wasi zaidi kuhusu kile ambacho maafisa wa China wanakifanya kuliko He Jiankui anakifanya," alisema.















