Jinsi janga la ugonjwa wa majipu kutoka miaka 700 iliyopita linavyoathiri afya yako sasa hivi

.

Chanzo cha picha, MUSEUM OF LONDON

Maelezo ya picha, Mabaki ya binadamu kutoka kwa makaburi ya wagonjwa wa janga la majipu huko London yalitumiwa katika uchanganuzi wa vinasaba

Mabaki ya binadamu kutokana na janga la ugongwa wa majipu kwenye makaburi ya kitambo yalitumika katika utafiti wa vinasaba yaani DNA.

Uharibifu wa janga hilo uliacha alama nyuma mwendelezo wa kijenetiki kwa binadamu kiasi kwamba bado linaathiri afya zetu karibu miaka 700 baadaye.

Karibu nusu ya idadi ya watu walifariki dunia wakati janga hilo la tauni ya majipu lilipotokea Ulaya katikati ya karne ya 13.

Utafiti wa hali ya juu uliochambua vinasaba yaani DNA ya mifupa ya karne nyingi tu uligundua mabadiliko ambayo yalisaidia watu kustahimili janga hilo.

Lakini mabadiliko hayo hayo yanahusishwa na magonjwa yanayotokea kwa sababu ya mfumo wake wa kinga kushambulia chembe yanayowaathiri watu leo.

Janga hilo ni moja ya nyakati muhimu sana, zilizosababisha vifo na giza katika historia ya binadamu.

Inakadiriwa kuwa hadi watu milioni 200 walipoteza maisha.

Urithi wa DNA kwa binadamu

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Chicago walishuku kwamba tukio la kutisha kama hilo lazima lilichangia katika mabadiliko ya vinasaba ya binadamu.

Walichambua DNA iliyotolewa kutoka kwenye meno ya mifupa 206 ya kale na waliweza kwa usahihi kabisa kupata mabaki ya binadamu ya kabla, wakati, au baada ya janga hilo la ugonjwa wa majibu.

Uchambuzi huo ulihusisha mifupa kutoka kwenye makaburi yaliyokuwa na mabaki ya binadamu ya janga hilo huko Smithfield ya Mashariki ya London, ambayo yalitumika kwa ajili maziko ya halaiki jijini humo, huku sampuli zaidi zikitokea Denmark.

.

Chanzo cha picha, MCMASTER UNIVERSITY

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Matokeo ya utafiti huo yalichapishwa katika jarida la Nature, na yalihusisha mabadiliko katika vinasaba iitwayo ERAP2. Kama mtu alikuwa na mabadiliko sahihi, alikuwa na 40% ambayo ilikuwa asilimia ya juu zaidi kunusurika kutokana na janga hilo.

"Hiyo ni athari kubwa, inashangaza kupata kitu kama hicho katika jeni ya binadamu", mwandishi kiongozi wa utafiti huo, Profesa Luis Barreiro wa Chuo Kikuu cha Chicago, alisema.

Kazi ya jeni ni kutengeneza kinga ambazo hukabiliana na vidudu wavamizi mwilini na kujulisha mfumo wa kinga ya mwili, kuuandaa kupigana vita kwa ufanisi zaidi ili kutambua na kumkabili adui.

Vinasaba zinakuja katika matoleo mbalimbali, ambayo hufanya kazi vizuri na kuna zile ambazo haziwezi, na kupata nakala moja kutoka kwa kila mzazi.

Hivyo, wale waliobahatika, wale ambao walikuwa zaidi na uwezekano wa kuishi, walirithi mfumo wa kinga wenye nguvu ya juu kutoka kwa mama na baba.

Walionusurika walikuwa na watoto na kupitia mabadiliko hayo yenye manufaa makubwa , hivyo ghafla hii ikawa kawaida.

"Ni jambo zuri sana, tunaona mabadiliko ya 10% katika vizazi viwili au vitatu, ni tukio zuri zaidi katika binadamu hadi leo", Profesa Hendrik Poinar, mtaalamu wa mazingira wa Chuo Kikuu cha Mcuzamili, alisema.

Matokeo yalithibitishwa katika majaribio ya kisasa na bakteria ya janga la, Yersinia pestis.

.

Chanzo cha picha, UNIVERSITY OF CHICAGO

Sampuli za damu kutoka kwa watu wenye mabadiliko hayo walikuwa na uwezo mzuri wa kukabiliana na maambukizi kuliko wale ambao hawakupata mabadiliko hayo.

Hata hii leo, mabadiliko hayo ya haraka ni ya kawaida zaidi kuliko kabla ya janga hilo la ugonjwa wa majipu.

Tatizo ni kwamba yamekuwa yakihusishwa na magonjwa yanayotokea kwa sababu ya mfumo wake wa kinga kushambulia chembe fulani za mwili. Kwa hiyo kilichosaidia kuwaweka hai mababu zako miaka 700 iliyopita kinaweza kuathiri afya yako leo.

Makovu ya zamani

Kuna kihistoria zingine katika DNA yetu na urithi ambao unatuathiri. Karibu 1-4% ya DNA ya kisasa ya binadamu inatoka kwa mababu zetu ambao walizaliana na watu wa kale (Neanderthals) na urithi huu unaathiri uwezo wetu wa kukabiliana na magonjwa, ikiwa ni pamoja na covid.

"Kwa hiyo makovu yale ya zamani bado yanaathiri usugu wetu wa magonjwa leo kwa namna ya ajabu kabisa", anasema Profesa Barreiro. Na hilo linaelezea kwamba 40% ya uwezo wa kuishi kuwa "uwezo wa juu zaidi wa ufanisi kuwahi kubainiwa katika binadamu".

Inaonekana kuzidi faida ya mabadiliko ya VVU-resistance au wale ambao kusaidia meng’enya maziwa, ingawa mtafiti anaonya kwamba kulinganisha moja kwa moja ni kupotosha. Hata hivyo, janga la corona, halitaacha urithi kama huo.

Mabadiliko yanafanya kazi kupitia uwezo wako wa kuzaa na kurithisha wengine jeni yako. Covid kikubwa inachofanya ni huua zaidi wazee ambao wamepitisha muda wa kupata watoto.

Kwa janga hili, ilikuwa ni uwezo wa ugonjwa kuua watu wenye umri tofauti tofauti na kwa idadi kubwa ambako kulisababisha urithi wake kuwa na athari za kudumu.