Wanasayansi waunda familia kongwe zaidi duniani kwa kutumia DNA

Mchoro wa msanii unaonesha ujenzi wa mpya wa makaburi ya Hazleton North

Chanzo cha picha, Corinium Museum © Cotswold District Council

Maelezo ya picha, Mchoro wa msanii unaonesha ujenzi wa mpya wa makaburi ya Hazleton North

Wanasayansi wamekusanya familia kongwe zaidi duniani kutoka kwa mifupa ya binadamu iliyozikwa kwenye kaburi la miaka 5,700 huko Cotswolds, Uingereza.

Uchambuzi wa chembe chembe za vinasaba (DNA) kutoka kwa mabaki kwenye kaburi hilo ulibaini kuwa watu waliozikwa hapo walikuwa kutoka kwa vizazi vitano vya familia moja kubwa.

Wengi wa waliopatikana kaburini walitokana na wanawake wanne ambao wote walizaa watoto na mwanamume mmoja.

Uamuzi wa kutumia eneo hilo ulitokana na ukoo wa mtu mmoja.

Lakini watu walizikwa katika sehemu tofauti za kaburi kulingana na walikotoka wanawake wa kizazi cha kwanza

Hii inaonyesha kuwa wanawake wa kizazi cha kwanza walishikilia nafasi muhimu katika kumbukumbu za jamii hii

Kaburi la Neolithic, au "cairn", Hazleton Kaskazini huko Gloucestershire lina vyumba viwili vya umbo la L, moja ikielekea kaskazini na nyingine kusini.

Mtafiti mwenza kutoka Prof David Reich, kutoka chuo cha matibabu cha Harvard Medical mjiniBoston, US, ambaye aliongoza uchunguzi wa DNA ya kale kutoka kwa mabaki hayo ya watu, alieleza: "Wawili kati ya wanawake, watoto wao wote wako katika chumba cha kusini - na watoto wao hadi kizazi cha tano.

"Halafu wanawake wengine wawili, watoto wao kimsingi wako katika chumba cha kaskazini - ingawa baadhi yao wanahamia chumba cha kusini baadaye katika maisha ya matumizi ya kaburi - pengine kwa kukisia kuporomoka kwa njia ya kaskazini ambayo ilimaanisha kuwa haikuwezekana kuzika hapo tena."

Dk Chris Fowler wa Chuo Kikuu cha Newcastle, Uingereza, mwandishi wa kwanza na mwanaakiolojia mkuu katika utafiti huo, alisema: "Hii ni ya umuhimu mkubwa zaidi kwa sababu inaonyesha kwamba mpangilio wa usanifu wa makaburi mengine ya Neolithic unaweza kutuambia kuhusu jinsi undugu ulifanyika kwenye makaburi hayo."

Family tree
Maelezo ya picha, Familia zilivyozika jamaa zao katika eneo la Hazleton North cairn

Kaburi hilo lilianzia kipindi muhimu baada kilimo kuletwa Uingereza na watu ambao mababu zao walikuwepo - miaka elfu kadhaa awali - walithama na Ulaya kutoka Anatolia (Uturuki ya sasa) na Aegean. Kazi hii itawasaidia watafiti kuelewa mienendo ya familia za kale na kujifunza zaidi kuhusu utamaduni wao.

"Tunatumai hii itakuwa moja kati ya tafiti nyingi kama hizi," Prof Reich alisema. "Inaweka wazi maisha ya watu hawa ... ambao waliishi mahali hapa muda mrefu sana uliopita."

Pia kuna dalili kwamba "watoto wa kambo" waliasiliwa katika familia hizo, watafiti wanasema - wanaume ambao mama yao alizikwa kaburini ijapokuwa baba mazazi hakuzikwa hapo. Mama yao pia alizaa watoto na mwanamume aliyekuwa na uhusiano wa damu na mwanzilishi wa awali wa familia.

Wanawake waliyotoweka

Wakati wanafamilia wawili wa kike waliokufa utotoni wakizikwa kaburini, kutokuwepo kabisa kwa mabinti watu wazima kunaonyesha kwamba mabaki yao yaliwekwa kwenye makaburi ya wenzi wa kiume ambao walipata nao watoto, au mahali pengine

"Kuna wanawake waliotoweka. Swali ni je wako wapo -Kwasababu wanaume na wanawake wanazaliwa kwa kiwango sawa. Ni fumbo - na sio kwamba wako kwenye kaburi linalofuata kwa sababu kwa ujumla jamii nzima inawakosa," Prof Reich alisema.

"Je watu wanachomwa? Kuna baadhi ya tamaduni za kuchoma wafu. Je watu Je, watu wanazikwa kwa njia tofauti katika mazingira au tunaona tu watu wanaofikia hadhi fulani ya kijamii?"

Ijapokuwa kaburi hilo lilifichua ushahidi wauzazi uliyotokana na -wanaume wanaozaa na wanawake wengi - pia inaonesha kuwa wanawake wazilizaa watoto na wanaume zaidi ya mmoja.

Wanawake tofauti waliyozaa na watoto na mwanamume mmoja hawakuwa na uhusiano wa damu.Lakini katika visa ambapo wanawake walizaa watoto na zaidi ya mwanamume mmoja, wanaume hao walikuwa jamaa wa karibu.

Iñigo Olalde, kutoka Chuo Kikuu cha Basque Country, Uhispania, ambaye ambaye ni mtaalamu mkuu wa sayansi ya vinasaba katika utafiti huo, alisema: "Uhifadhi bora wa DNA kwenye kaburi na utumiaji wa teknolojia za hivi karibuni katika urejeshaji na uchanganuzi wa DNA ya zamani ulituruhusu kufichua familia kongwe zaidi kuwahi kuundwa upya na kuuchambua ili kuelewa jambo la kina kuhusu muundo wa kijamii wa vikundi hivi vya zamani."

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la Nature.