Watu wa Kale:Ngono ilikuwakeje kwa watu wa kale wa Neanderthals?

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanasayansi wabaini kuwa mababu na mababu zetu huenda walifanya mapenzi na spishi ya Neanderthal.
Macho yao yalikutana katika eneo la milimani la Romania ya zama za kale.
Alikuwa ameketi mkao mzuri na ngozi yake ya kupauka, pengine hilo limetokana na kuchomwa na jua sana.
Katika moja ya misuli yake amevaa mkufu uliotengenezwa kwa tai. Alikuwa binadamu wa zamani za kale aliyevaa ngozi ya mnyama yenye manyoya. Ngozi yake ilikuwa nyeusi, miguu mirefu na nywele zake zilikuwa zimesokotwa.
Alisafisha koo lake akamwangalia juu na chini na kwa sauti yake nzito akaanza kumtongoza.
Naye akaanza kumtazama kwa haya. Bahati nzuri, hawakuwa wanaelewana lugha. Wote wakacheka kwa namna ya ajabu na sote tunaweza kubahatisha kilichotokea.
Bila shaka, ingekuwa ni kama matukio ya kwenye riwaya za mapenzi.
Pengine mwanamke alikuwa binadamu wa zamani na mwanamume alikuwa wa spishi nyengine. Pengine uhusiano wao ulikuwa wa kawaida, wa kiutendaji zaidi kwasababu wakati huo hakukuwa na watu wengi. Inasemekana kuwa mahusiano ya aina hiyo hayakuwa ya makubalino.
Wakati hatutawahi kujua kilichotokea katika tukio hili - au kwa mengine kama hili - kile tulicho na uhakika nacho ni kwamba wanandoa kama hao walikuwepo.

Chanzo cha picha, Alamy
Karibu, miaka 37,000- 42,000 baadaye. Februari 2002, wavumbuzi wawili walivumbua kitu kipya katika pango moja kusini mashariki mwa milima ya Carpathia, karibu na mji wa Romania wa Anina.
Ndani ya pengo hilo, walibaini maelfu ya mifupa ya mamalia. Kutokana na historia yake ndefu, ilidhaniwa kuwa ni ya dubu wa kiume wa rangi ya kahawia. Mbali na mifupa hiyo ilikuwa ni taya za binadamu na uchunguzi ulibaini ilikuwa ni ya mwanadamu wa sasa wa Ulaya.
Inasemekana kuwa mifupa hiyo ilijiosha yenyewe ndani ya pango bila kuguswa na yeyote tangu wakati huo.
Wanasayansi walibaini kuwa taya hizo pia zilikuwa na muonekano usio wa kawaida, kama vile za watu wa kale wanaojulikana kama Neanderthal.
Miaka mingi baadaye bado hili lilithibitishwa.
Wanasayansi walipofanya uchunguzi wa DNA mwaka 2015, walibaini kwamba alikuwa mwanamume na kuna uwezekano mkubwa asilimia 6 hadi 9 alikuwa wa mtu wa zamani sana wa Neanderthal.
Pia ilibainika kwamba alikuwa na chembe za urithi za kizazi cha nne hadi cha sita kilichopita.
Mbali na taya, timu hiyo pia ilibaini vipande vya fuvu kutoka kwa mtu mwingine ambaye alikuwa na muonekano kama wa kwanza. Hata hivyo, wanasayansi bado hawajafanikiwa kuchunguza mabaki ya mtu huyo lakini pia naye taya zake, zinasemekana kuwa zenye kuhusishwa na watu wa kale (Neanderthal).
Na tangu wakati huo, ushahidi wa kwamba kulikuwa na mapenzi kati ya wanadamu wa kisasa wa mapema na Neanderthal ni kitu ambacho kilikuwepo.
Ikiwa vimejificha katika vinasaba vya kizazi cha sasa, kuna ishara kwamba katika maeneo mbalimbali duniani. Hadi hii leo, kuna binadamu wenye DNA za angalau vizazi tofauti vya Neanderthal.
Mwaka 2016, wanasayansi walibaini Neanderthal kutoka milima ya Altai huko Siberia na inasemekana walishirikishana chembe zao za urithi na asilimia 1-7 na binadamu wa sasa walioishi takriban miaka 100,000 iliyopita.
Kupigana busu
Mwaka 2017, Laura Weyrich - anthropolojia wa chuo kikuu cha Pennsylvania - aligundua viini vilivyoishi miaka 48,000 katika jino la siku za kale.
"Naangalia bakteria za kale kama namna ya kujifunza zaidi juu ya siku za nyuma, na hesabu ya meno ndio njia pekee ya kujenga viini ambavyo viliishi kwa mwanadamu wa kale," amesema Weyrich. Pia alikuwa na shauku ya kujua kile ambacho Neanderthal walikuwa wa kila na namna walivyoishi. Na ili kupata jibu alichunguza meno yaliyopatikana katika mapango matatu tofauti.
Aina mbili zilichukuliwa miongoni mwa Neanderthal 1 waliopatikana El Sidrón kaskazini magharibi mwa Uhispania. Na kuonekana kuwa wengi wao walikuwa na kasoro za kuzaliwa.
Moja ya kilichomshangaza Weyrich ni kwamba, moja ya jino kutoka El Sidrón lilikuwa na bacteria ambao hadi hii leo bado wako kwenye mdomo wetu.
Ukilinganisha bakteria wa Neanderthal na wanadamu wa kisasa wa mapema alifanikiwa kukadiria kuwa wawili hao waliachana kwa miaka 120,000 iliyopita.
"Kwangu mimi ina furahisha kwasababu ni mara ya kwanza tunazungumzia kukutana kiapenzi kati ya binadamu na Neanderthal," Weyrich amesema.
Weyrich anaeleza kuwa huenda hiyo ndio sababu moja wapo ya kuwepo kwa busu lile lile hadi leo na kusambaziana viini. "Unapombusu mtu, bakteria wa kwenye mdomo watakuwa wana zunguka zunguka mdomoni," anasema. "Huenda ni kitendo ambacho kilitokea zaidi ya mara moja."
Namna nyengine ya kuhamishiana bakteria ni kwa njia ya kula pamoja. Na ingawa hakuna ushahidi unaoonesha Neanderthal akitayarisha chakula kwa ajili ya binadamu wa kisasa wa mapema zaidi huenda kula chakula pamoja ni moja ya chanzo cha kusambaziana viini hadi kwa mwanadamu wa sasa.
Kwa Weyrich, ugunduzi huo unafurahisha kwasababu unaonesha vile mahusiano yetu na aina ya binadamu wengine yalivyokuwa zamani za kale na jinsi yalivyoendeleza jamii ya bakteria waliopo sasa hivi.
Wanaume na wanawake wa Neanderthal
Ni vigumu kusema kwa uhakika ikiwa ni wanawake wa Neanderthal ndio waliokuwa na uhusiano na wanaume wa kisasa wa mapema au vyenginevyo lakini kuna vidokezo.
Mwaka 2008, wanasayansi walibaini kidole kilicho katika na jino moja aina ya gego katika mapango ya Denisova, nchini Urusi milima ya Altai kulikopelekea kubainiwa kwa vispishi vipya vya binadamu.
Mapango ya Denisovan yalihusishwa kwa karibu na Neanderthal kuliko binadamu wa sasa; Hili lilijitokeza zaidi mwaka 2018 baada ya ugunduzi wa mifupa ya msichana mdogo aliyepewa jina la Denny ambaye mama yake alikuwa ni wa mtu wa kale aina ya Neanderthal na baba yake alikuwa wa mtu wa kale aina ya Denisovan.
Pia, alisema itaeleweka zaidi ikiwa kromosomu ya jinsia ya kiume ya watu wa kale aina ya Neanderthal zilifanana na zile za Denisovan. Lakini wanasayansi walipofanya uchunguzi wa DNA kwa Neanderthal watatu walioishi miaka 38,000-53,000 iliyopita, walistaajabu kupata kromosomu za Y zilizofanana zaidi na zile za binadamu wa sasa.
Watafiti wanasema ushahidi huu wa vinasaba kati ya Neanderthal na binadamu wa kisasa wa mapema, inaonekana viumbe Neanderthal walipokuwa wanaeelekea kuisha, kromosomu zao za Y huenda pia zilipotea, na badala yake zikaja zetu. Hili linaonesha kuwa wanaume wa kale zaidi walikuwa wakifanya mapenzi na wanawake Neanderthal.
Magonjwa ya zinaa
Miaka michache tu iliyopita, Ville Pimenoff alikuwa akifanya utafiti wa magonjwa ya kuambukiza human papillomavirus (HPV) alipobaini kitu ambacho si cha kawaida.
Virusi vya Papilloma huwa sana miongoni mwa wanyama wakiwemo dubu, pomboo, kasa, nyoka na ndege - yaani vimepatikana katika kila spishi ambayo wamekuwa wakiifanyia utafiti hivi karibuni.
Kwa binadamu pekee, kuna zaidi ya virusi 100 vinavyosambaa ambavyo vinasemekaa kuchangia asilimia 99.7 ya saratani ya kizazi kote duniani. Hatari zaidi ikiwa ni HPV-16 ambayo inaweza kumgandama mwanadamu kwa miaka kwasababu inaathiri seli ilizovamia.
"Nilifanya majaribio mara elfu kadhaa na matokeo yakawa yale yale," Pimenoff anasema. Kulingana na vile virusi vya HPV vinavyosambaa leo hii, aliamini kwamba sio eti vilisambazwa hadi kwa mwanadamu mara moja tu, lakini mara kadhaa.
Yaani anachomaaisha ni kwamba, kufanya mapenzi ati ya mwanadamu wa sasa na Neanderthal huenda kulisabisha uhamishaji wa virusi vipya kwa mwanadamu wa sasa ikiwemo vile vya HIV.
Lakini hakuna haja ya kuhisi vibaya kwasababu ushahidi unaonesha pia kuwa pia nao, tuliwapa ugonjwa wa zinaa - ikiwemo ule wa malengelenge kwenye viungo vya uzazi.
Viungo vya ngono
Najua sasa hivi unajiuliza viungo vya uzazi kwa wanaume na wanawake wakati wa Neanderthal vilikuwa vipi. Inasemekana kwamba kuna uwezekano mkubwa vimebadilika.
Ilijitokeza kuwa viungo vya uzazi vya wanyama vinaweza kuonesha mtindo wao wa maisha, namna walivyojamiana na historia ya mabadiliko ya viungo hivyo.

Chanzo cha picha, STR/AFP/Getty Images
Njia moja ambayo uume wa binadamu ni tofauti ni kwamba ni laini . Jamaa zetu wa karibu kama vile sokwe wa Bonobo ambao uhusiano wetu wa DNA ni karibu asilimia 99 walikuwa na vitu kama 'vifupa vidogo' kati sehemu hizo
Vifupa hivyo ambavyo vimeundwa kwa protini inayofanana na ile katika ngozi au nywele (keratin) ilitumiwa kuondoa manii ya wanaume wengine kutoka kwa sehemu za uke za wanawake na kuwazuia kushiriki ngono kwa muda
Neanderthal wa mwisho: Kumalizika kwa kizazi hiki
Hata kama huna haja ya kujua binadamu wa kale walivyokuwa, inasemekana kwamba wamechangia jinsi binadamu alivyo leo hii, kuanzia ngozi yake nywele zake, usingizi wake, hadi mfumo wa kinga ya mwili.
Kujifunza kuwahusu tayari kunapelekea uwezekano wa kujua kwa undani magonjwa ya sasa hivi kama vile dawa zilizokuwa zinalenga vinasaba vya Neanderthal hadi magonjwa hatari zaidi kama virusi vya corona.















