Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 22.10.2024

Rushford

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Bayern Munich na Marseille wanavutiwa na Marcus Rashford, Manchester United wako tayari kumtoa Antony kwa mkopo, Francesco Totti huenda asistaafu.

Bayern Munich na Marseille wameungana na Paris St-Germain katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 26, kutoka Manchester United. (Tea Talk)

Manchester United wako tayari kupokea ofa za mkopo kwa ajili ya winga wa Brazil Antony, 24 wakati wa usajili wa Januari. (Football Insider)

Gwiji mstaafu wa Italia na Roma Francesco Totti, 48, anasema huenda akarejea uwanjani baada ya kuwasiliana na klabu kadhaa za Serie A. (Gazzetta Dello Sport - kwa Kiitaliano)

Xabi Alonso

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Bayer Leverkusen wanajiandaa kwa ajili ya kuondoka kwa kocha Xabi Alonso msimu ujao

Arsenal, Aston Villa na Newcastle wanavutiwa na kiungo mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Oscar Gloukh, 20. (Caught Offside)

Bayer Leverkusen wanajiandaa kwa ajili ya kuondoka kwa kocha Xabi Alonso msimu ujao, huku Mhispania huyo akinyatiwa na Real Madrid na Manchester City, iwapo Pep Guardiola ataamua ataondoka. (Sky Germany)

Everton wanaandaa dau la pauni milioni 17 kumnunua mshambuliaji wa Besiktas wa miaka 19 wa Uturuki Semih Kilicsoy. (Kontraspor - kwa Kituruki)

La Liga inaomba Shirikisho la Soka la Uhispania, Uefa na Fifa kuruhusu mchezo wa Barcelona dhidi ya Atletico Madrid wa mwezi Desemba kufanyika Miami. (Mail)

Arsenal wanatafuta mbinu za kupanua Uwanja wa Emirates. (Times - usajili unahitajika)

Rapa wa Marekani A$AP Rocky ni sehemu ya kundi la uwekezaji linalotaka kununua hisa za Ligi ya Pili ya klabu ya Tranmere Rovers kwa £15m. (Sun)

Bryan Mbeumo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arsenal wanapania kumsajili mshambuliaji wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo

Arsenal wanapania kumsajili mshambuliaji wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo, 25, baada ya kuanza vyema msimu huu. (Football Insider)

Julen Lopetegui hayuko katika hatari ya kufutwa kazi kama meneja wa West Ham licha ya msimu huu mbaya wa klabu hiyo. (Mlezi), nje

Arsenal na Chelsea wanamfuatilia mshambuliaji wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 24. (TBR Football)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi