'Hatima ya Yemen ni hatima ya Tehran,' Israel yawatishia Wahouthi

Muda wa kusoma: Dakika 3

Israel imetishia kulipiza kisasi dhidi ya kundi la Houthi Ansar Allah nchini Yemen baada ya jeshi la Israel kulinasa kombora lililorushwa kutoka Yemen kuelekea Israel.

Siku ya Jumamosi, Wahouthi walitangaza kuwa wamerusha "kombora la balistiki" kuelekea Israel "kujibu mazoea ya Israel dhidi ya Wapalestina katika vita katika Ukanda wa Gaza," kulingana na kundi la Yemen.

Kombora la Jumamosi lilikuwa la kwanza kurushwa na kundi hilo tangu kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Iran mnamo Juni 24, kufuatia makabiliano ya siku 12.

Pia unaweza kusoma

Mkono wake utakatwa"

"Hatima ya Yemen ni hatima ya Tehran," Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz alisema katika taarifa yake. "Baada ya kupiga kichwa cha nyoka huko Tehran, tutawalenga Wahouthi huko Yemen pia. Yeyote atakayeinua mkono dhidi ya Israel atakatwa mkono wake."

Israel imelitishia kundi la Ansar Allah kwamba italiwekea vikwazo vya majini na angani iwapo litaendelea na mashambulizi dhidi yake.

Ving'ora vilisikika katika maeneo kadhaa, haswa huko Yerusalemu.

"Baada ya ving'ora kulia muda katika maeneo kadhaa ya Israel," jeshi lilisema katika taarifa, "kombora lililorushwa kutoka Yemen lilinaswa." Jeshi lilibaini kuwa uvamizi huo ulifanywa na jeshi la anga.

Kinyume chake, msemaji wa jeshi la Houthi Yahya Saree alitangaza katika taarifa Jumanne kwamba "operesheni nne za kijeshi" zimefanywa dhidi ya Israeli.

Sari' alizungumza kuhusu kulenga Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion huko Tel Aviv kwa "kombora la Palestina 2 hypersonic ballistiki," wakati ndege zisizo na rubani tatu zililenga "maeneo matatu ya adui wa Kizayuni katika maeneo ya Jaffa, Ashkelon, na Umm al-Rashrash," akimaanisha mji wa pwani wa Eilat kwenye Ghuba ya Aqaba.

'Labda ndege za kivita za B-2 zinapaswa kutembelea Yemen'

Balozi wa Marekani nchini Israel Mike Huckabee alisema katika chapisho kwenye jukwaa la X, "Tulifikiri kwamba tumemaliza makombora kuja Israel, lakini Wahouthi walirusha kombora huko. Kwa bahati nzuri, mfumo wa ajabu wa anga wa Israel unatuwezesha kwenda kwenye makazi na kusubiri hatari. 'Labda ndege za kivita za B-2 zinapaswa kutembelea Yemen'

Marubani wa Marekani walifanya mashambulizi kwa kutumia ndege za kivita za B-2 kwenye maeneo ya nyuklia ya Iran wakati wa vita vya anga vya siku 12.

Waasi wa Houthi wanasema mashambulizi yao ni ya mshikamano na Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Tangu kuanza kwa Vita vya Gaza mnamo Oktoba 2023, Wahouthi wamelenga Israel pamoja na usafirishaji wa meli katika Bahari Nyekundu, na kutatiza shughuli za biashara za kimataifa.

Makombora mengi na ndege zisizo na rubani walizorusha zilinaswa.

Waasi wa Houthi walikuwa wamesitisha mashambulio yao wakati wa usitishaji vita wa miezi miwili kati ya Israel na Hamas, na walianza tena mashambulizi yao baada ya Israel kurejesha operesheni zake.

Israel imeanzisha mashambulizi kadhaa nchini Yemen, yakilenga bandari zinazodhibitiwa na Wahouthi na uwanja wa ndege wa Sanaa unaodhibitiwa na Wahouthi.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla