Ndani ya ulimwengu wa "mungu wa kike" mwenye utata

h
Maelezo ya picha, Radhe Ma ni mmoja wa wanawake wachache katika jambo lenye utata la " mungu binadamu" nchini India.
Muda wa kusoma: Dakika 8

Anadai kufanya miujiza, na wafuasi wake wanaamini kuwa yeye ni "mungu mwanamke."

Lakini je Radhe Ma ni nani?

Radhe Ma ni mmoja wa wanawake wachache ambao wameingia katika ulimwengu wa "miungu ya kibinadamu" nchini India, jambo lenye utata na linalokua ambalo huvutia idadi kubwa ya watu. BBC ilipata fursa adimu ya kuingia katika ulimwengu wa mwanamke huyu wanayemwona kama "mungu mwanamke", ikitafuta kufichua siri za mchanganyiko huu wa ajabu wa imani na hofu.

Wanawake waliobeba mikoba ya Louis Vuitton na Gucci, waliovaa nguo za kitamaduni za kifahari na kupambwa kwa vito vya dhahabu na almasi, hukusanyika kwa kusanyiko la jioni la Radhe Ma.

Tofauti na watu wengi watakatifu, hapendi kuamka mapema, havai nguo rahisi, hafurahii mazungumzo marefu, na anajiita "Mama wa Miujiza."

Radhe Ma aliniambia, "Miujiza hutokea kwa wafuasi wake, mahitaji yao yanatimizwa, kwa hivyo wanatoa michango."

Watu hapa wanasimulia hadithi nyingi za jinsi Radhe Ma alivyowabariki wanandoa wasio na watoto, kuwasaidia wanawake ambao walikuwa wamejifungua watoto wa kike pekee hatimaye kuzaa watoto wa kiume, kuwaponya wagonjwa, na kusaidia kuokoa biashara ambazo zilikuwa karibu kuanguka.

Madai ya nguvu za kimungu sio ya kipekee kwa Radhe Ma. India imejaa wale wanaoitwa "miungu ya kibinadamu," na ingawa hakuna takwimu sahihi rasmi, idadi yao inaonekana kuongezeka mwaka baada ya mwaka.

g
Maelezo ya picha, Pushpinder Bhatia aliiambia BBC "alivutiwa na aura ya Radhe Ma."
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Baadhi yao huwakuepusha na mashtaka ya ufisadi, ukiukaji wa maadili, na hata unyanyasaji wa kijinsia. Radhe Ma alizungukwa na madai ya ushirikina (chawi) na kuwezesha malipo ya mahari, licha ya sheria ya India kukataza mazoea kama hayo. Lakini , uchunguzi wa polisi ulimalizika na mashtaka yote dhidi yake kufutwa.

Licha ya hayo, maelfu ya waja bado wanamiminika kuwaona wanaume na wanawake hawa, ambao wanachukuliwa kuwa vyombo vitakatifu, na mwaka jana, mkanyagano katika moja ya mikusanyiko hii ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 120.

"Wahindi wengi hukulia katika familia zinazoamini kwamba nguvu za kimungu zinaweza kupatikana kupitia ibada, kutafakari, au maombi, na kwamba wale wanaozipata wana uwezo wa kufanya miujiza," anasema Shyam Manav, rais wa Shirika la India la Kupambana na Ushirikina.

Anaongeza: "Mtu kama huyo anachukuliwa kuwa kiumbe wa kimungu, au anaitwa mtakatifu

Nilikutana na Pushpinder Bhatia, mhitimu wa Shule ya Biashara ya Saïd ya Chuo Kikuu cha Oxford na mkurugenzi wa ushauri wa elimu, alipokuwa amesimama kwenye foleni ya wanawake wakisubiri kukutana na Radhe Ma. Aliniambia hakuwahi kufikiria angejikuta mwanafunzi wa "kiumbe mkuu aliyepata mwili katika umbo la mwanadamu."

Aliniambia, "Mwanzoni, nilikuwa na maswali mengi: Je, mungu anaweza kweli kupata mwili katika umbo la mwanadamu? Je, hii ni kweli? Je, kweli anaweza kutoa baraka zinazobadilisha maisha ya mtu? Na ni nini siri ya miujiza hii wanayodai kutokea?"

Lakini , Bhatia alikutana na Radhe Ma baada ya msiba kuikumba familia yake.

Ingawa wengine wanaweza kufikiria alikuwa katika hali yake dhaifu ya kisaikolojia wakati huo.

Anasema, "Nadhani katika mkutano wangu wa kwanza wa kiroho naye, nilihisi mvuto mkubwa kwa mazingira yaliyomzunguka. Ninaamini kwamba unapovuka sura yake kibinadamu, unahisi uhusiano wako na yeye kwa haraka."

"Wafuasi katika chumba cha dhahabu"

g
Maelezo ya picha, Mikutano ya Radhe Maa na waumini wake hufanyika katika chumba kilichopambwa kwa rangi nyekundu na dhahabu, rangi anazozipenda.

'darshan' (kukutana kiroho) na Radhe Ma ni wakati unaotafutwa na wengi, na nilishuhudia mkutano mmoja kama huo, ambao ulifanyika usiku wa manane katika nyumba ya kibinafsi huko Delhi.

Miongoni mwa mamia ya waja walikuwa wafanyabiashara mashuhuri na familia ya afisa mashuhuri wa polisi, ambao wote walikuwa wamekuja kutoka mbali kabisa kumuona.

Nilikuwa pale kama mwandishi wa habari, nikitazama na kurekodi kile kilichokuwa kikitokea, lakini niliambiwa kwamba kwanza kabisa lazima nipokee baraka zake, na haraka nilijikuta nikisukumwa mbele ya foleni ndefu. Si hivyo tu, lakini nilipewa maagizo sahihi juu ya jinsi ya kufanya sala, na maonyo kwamba kosa lolote ndani yake linaweza kuleta madhara kwa familia yangu.

Katika chumba hicho kilichopambwa kwa rangi nyekundu na dhahabu, rangi zinazopendwa na Radhe Ma, macho yake yalitawala kila kitu.

Wakati mmoja nilimwona akiwa amejawa na furaha, iliyofuatwa na hasira, hasira ambayo ilionekana kuenea kwa kushangaza wafuasi wakewake, ambaye mara moja alionekana kupoteza fahamu, na kisha chumba kikanyamaza wakati mwanafunzi huyo alipoanza kuzunguka sakafuni.

Dakika chache baadaye, baada ya wafuasi wake kumuomba msamaha, wimbo maarufu wa Kihindi ulicheza na akaanza kucheza, akiashiria kurudi katika hali ya utulivu. Kisha foleni ya wafuasi ilianza kusonga tena.

Kufikia hadhi ya "wanaoabudiwa"

gh
Maelezo ya picha, Hekalu linaloitwa Radhe Ma lililojengwa na mumewe Mohan Singh

Radhe Maa asili yake ni jimbo la kaskazini mwa India la Punjab.

Mzaliwa huyo wa Sukhwinder Kaur katika familia ya tabaka la kati katika kijiji chenye maisha ya chini, anadai kuwa alipata nguvu za kimungu baada ya kupokea uchawi kutoka kwa gwiji wa kiroho.

"Wakati ambapo watoto wenzake walikuwa na ndoto ya kuwa marubani au madaktari, Radhe Ma kila wakati aliuliza swali, 'Mimi ni nani?' Kwa hivyo, baba yetu alimpeleka kwa gwiji mashuhuri wa kiroho, ambaye alimtangaza kuwa mungu mwenye mwili katika umbo la mwanadamu," anasema dada yake Rajinder Kaur.

Dada yake anasimamia hekalu dogo, la chumba kimoja liitwalo Radhe Ma, lililojengwa na mumewe, Mohan Singh.

"Tunamwita 'Papa,' kwasababu kwa kuwa yeye ni mama yetu, yeye ni baba yetu," Kor anaongeza.

Radhe Ma alipofikia umri wa miaka ishirini, wakati mumewe alikuwa nje ya nchi, alikabidhi utunzaji wa wanawe wawili kwa dada yake na kuanza kutumia maisha yake katika nyumba za waja wake, ambao wengi wao walikuwa wafanyabiashara.

Alisafiri kutoka jiji hadi jiji hadi mwishowe akaishia Mumbai, moyo kitovu cha uchumi wa India, ambapo alikaa zaidi ya miaka kumi chini ya uangalizi wa mfanyabiashara kabla ya kurudi kwa familia yake.

Watetezi waaminifu na wenye bidii zaidi wa hekalu hilo ni wafuasi ambao wameishi katika nyumba zake kwa miaka, na ambao wanadai kuwa hii imechangia ustawi wao.

Radhe Ma anaishi katika ulimwengu wa ajabu, ambapo "uungu" unaodhaniwa umeunganishwa na mtandao wa mali na mahusiano ya kidunia.

Radhe Ma kwa sasa anaishi katika jumba la kifahari lililojengwa kwa ajili yake na wanawe wawili, wote wafanyabiashara waliofanikiwa kibiashara.

Lakini, anaishi kwenye gorofa lake mwenyewe, tofauti na jumba lingine, hajawahi kuiacha isipokuwa kupokea wageni au kusafiri kwenda jiji lingine kwa hafla ya umma.

h
Maelezo ya picha, Baadhi ya waumini huweka picha za Radhe Ma majumbani mwao.

"Kwanza, haishi nasi. Sisi ndio waliobahatika kuishi chini ya ulinzi na baraka zake. Pili, hatuoni sisi kama familia yake. Anatuona kama waja tu," anasema mkwe wake wa kike, Megha Singh, ambaye ana jukumu la kuandaa shughuli zake zote za umma.

Familia ya Radhe Ma na washirika wake wachache waumini wa karibu wanasimamia michango anayopokea.

"Michango anayopokea huwekwa katika shirika la misaada linaloendeshwa na waja wake, ambao hukagua maombi ya wale wanaohitaji na kisha kusambaza pesa au zawadi.

Hata hivyo, mwanamke huyu, ambaye anaonekana kama sanamu, anafurahia kuvaa nguo za kifahari na kujipamba kwa vito vya mapambo.

"Ninapenda kuvaa nguo za kifahari na lipstiki nyekundu, ndivyo kila mwanamke aliyeolewa anapaswa kufanya," anasema Radhe Ma. "Lakini mimi si shabiki wa vipodozi," anasema, ingawa anavaa sana.

"Ukiwa na sanamu takatifu ya binadamu, unachagua mavazi ambayo yanafaa zaidi. Kwa nini usifanye vivyo hivyo na mungu aliye hai? Tumebarikiwa na uwepo wake, na tumebarikiwa kwa heshima ya kuitumikia," Megha Singh anaongeza.

Ikumbukwe kwamba mnamo 2020, Radhe Ma alionekana kwenye toleo la Kihindi la Big Brother kutoa baraka zake kwa nyumba ya washiriki, aking'aa katika mavazi yake mekundu na kubeba mkuki wa dhahabu.

Picha yake ya sasa ni tofauti kabisa na picha zake kama msichana wa kawaida ambazo wafuasi wake walinionyesha wakati wa ziara yangu huko Punjab.

Mja mmoja, Santosh Kumari, anaweka picha za Radhe Ma kwenye chumba maalum nyumbani kwake. Alinieleza kuwa imani yake kwake ilitokana na baraka aliyopokea wakati mumewe alikuwa hospitalini baada ya mshtuko wa moyo, ambao baadaye alipona.

Aliniambia, "Alitokwa na damu kutoka kinywani mwake, na akaipaka kwenye paji la uso wangu, kisha akasema, 'Hutaumia, mume wako atapona.'"

Nilishangaa pia wakati waumini kadhaa walipozungumza juu ya ulimi wa Radhi Ma kugeuka mwekundu na wenye damu, wakiamini kwamba haya yalikuwa ni matokeo ya udhihirisho wa nguvu za kimungu alizonazo.

Kumari ni mmoja wa wanawake wapatao 500, wengi wao wakiwa wajane, ambao hupokea pensheni ya kila mwezi ya kati ya rupia 1,000 na 2,000 (takriban $11 hadi $22) kutoka kwa Shri Radhe Maa Charitable Trust.

Walengwa wengine wa pensheni pia walisimulia hadithi za miujiza, lakini wakati mwingine waliongeza maelezo ya tahadhari.

Hofu

g
Maelezo ya picha, Radhe Ma anaishi katika kasri na wanaye wawili

"Hatuwezi kusema chochote juu yake," alisema Sarjit Kaur kwa tahadhari. "Inaweza kutuletea madhara. Ikiwa sitawasha taa kwa ajili yake, kitu kibaya kitanitokea na nitajikuta nimelazwa kitandani."

Kaur hakosi siku bila kuwasha taa kwa Radhe Ma, kwani moyo wake umejaa imani thabiti katika nguvu zake za kimungu.

Profesa Manav anahusisha hii na hofu ya mfuasi wake kupoteza baraka ya "sanamu" hii.

Anasema, "Kulingana na sheria ya uwezekano, utabiri fulani hutimia, na mtu mtakatifu anapewa sifa kwa hilo. Lakini wakati utabiri ni mbaya, hawajibishwi. Badala yake, kosa hilo linahusishwa na mapungufu ya mtu binafsi, iwe katika maombi yake, imani yake dhaifu, au hata bahati mbaya yake."

Wachache wa wale niliokutana nao kwenye mikusanyiko ya hadhara ya Radhe Ma walionyesha waziwazi kutoamini uwezo wake wa kufanya miujiza.

Mtu mmoja alielezea madai hayo kama "hadithi tu," wakati mwingine alionyesha vipodozi na nguo za bei ghali, akidai kuwa mambo haya hayafanyi mtu kuwa "kama mungu," akiongeza kuwa hajaona ushahidi wowote wa yeye kufanya miujiza mwenyewe.

Lakini, hawakusita kuhudhuria mikusanyiko ya umma ya Radhe Ma, wakiiona "ya kufurahisha na ya kuburudisha" na walikuwa na hamu ya kumuona mwenyewe baada ya kumtazama kwenye onyesho halisi.

Wakati wa safari yangu, nilikutana na baadhi ya waja wa zamani wa Radhe Ma, ambao walithibitisha kwamba unabii wake haukutimia na hata kuwadhuru, lakini walipendelea kutotajwa jina.

Hii iliongeza udadisi wangu juu ya wafuasi wake, na kiwango cha imani yao katika uungu wake na utii wao kwake.

''Hadithi au imani''

h
Maelezo ya picha, Waumini wengi wa Radhe wanatoka katika familia tajiri.

Jioni moja, alishtuka kuona Radhe Ma akiuliza wandani wake, ambao walikuwa wamekaa sakafuni, kuigiza sauti za wanyama, na mara moja walitii amri zake.

Niliwaambia wafanye kama mbwa na nyani, na wakaanza kubweka, kulia, na kufanya ishara za kukwaruza.

Sijawahi kuona kitu kama hiki hapo awali, na kwa kuwa binti-mkwe wa Radhe Ma, Megha Singh, alikuwa chumbani, nilimuomba aelezee maana ya tabia hii.

Hakukuwa na ishara ya mshangao usoni mwake.

Alianza hotuba yake kwa kusema kwamba mwanamke huyu mtakatifu hakuwa ameondoka kwenye mipaka ya chumba chake kwa zaidi ya miaka thelathini.

"Kwa hivyo, tabia hii ndio chanzo pekee cha burudani inayopatikana kwake, na tunatafuta kusema utani au kuleta furaha moyoni mwake kupitia vitendo hivi," aliongeza.

Hii ilinikumbusha onyo ambalo nilikuwa nimesikia mara nyingi, kwamba wafuasi wake wanapaswa kuwa na imani thabiti bila kutoridhishwa.

Nilimuuliza mja anayeitwa Pushpinder Singh ni nini Radhe Ma nawataka wafuasi wake wafanye?. Alijibu, "Yeye hajawaomba lolote, isipokuwa kusema, 'Unapokuja kwangu, na iwe kwa moyo wazi na imani thabiti. Nimeiona mwenyewe. Watu wanapokuja na imani hii, miujiza hutokea kwao. Lakini ikiwa watakuja kumuona, ninaamini kwamba kwa heshima na adabu zote, hawatakuwa tena na nafasi katika kikundi hicho.'"

Profesa Manav anaamini kwamaba maelezo haya bila shaka ndio kiini cha "hadithi."

Tunaambiwa kwamba hekima inaweza kupatikana tu kupitia imani isiyotikisika kwa mwalimu, na yeyote anayemtilia shaka au anayetaka kumjaribu anapoteza imani yake na baraka zake.

Je, ni hadithi au imani? Radhi Ma ana hakika kwamba waja huendelea kuwa waaminifu.

Anasema hajali wale wanaomwita mlaghai.

"Sijali," anatabasamu.

Anaongeza, "Mungu ananiona kutoka juu na ananitunza."