ChatGPT: Je, China inaweza kuipiku Marekani katika teknolojia ya akili bandia?

Watoto

Chanzo cha picha, Getty Images

Teknolojia ya Akili Bandia(Artificial Inteligence) imeibua wasiwasi kiasi kwamba imejumuishwa kwenye kile ajenda mkutano wa kilele wa G7 mwishoni mwa juma.

Wasiwasi kuhusu athari ya AI inaambatana na jaribio la Marekani kuzuia China kufikia teknolojia muhimu.

Kwa sasa, Marekani inaonekana kuwa mbele katika mbio za AI. Na tayari kuna uwezekano kwamba udhibiti wa sasa wa usafirishaji wa vifaa maalum kwenda China unaweza kuzuia Beijing kupiga hatua.

Lakini China inaweza kufikia lengo lake, kulingana na wachambuzi, kwani teknolojia ya akili bandia inachukuwa muda kukamilishwa.

Kampuni za kiteknlojia za Kichina "Bila shaka ni za hali ya juu zaidi kuliko za Marekani, kulingana na jinsi unavyotathmini ukuaji wa kiteknolojia," Kendra Schaefer, mkuu wa utafiti wa sera za teknolojia katika Trivium China aliambia BBC.

Hata hivyo, anasema "uwezo wa China wa kutengeneza vifaa vilivyo na ubora wa hali ya juu unakadiriwa kuwa miaka 10 hadi 15 nyuma ya Marekani."

Silicon Valley

Faida kubwa ya Marekani ni Silicon Valley, ambayo bila shaka ndiyo sehemu kuu ya ujasiriamali duniani. Ni nyumbani kwa makampuni makubwa ya teknolojia kama vile Google, Apple na Intel ambayo yamesaidia kuunda maisha ya kisasa.

Wavumbuzi nchini humo wamesaidiwa na utamaduni wake wa kipekee wa utafiti, anasema Pascale Fung, mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa teknolojia ya Akili Bandia katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Hong Kong.

Watafiti mara nyingi hutumia miaka kufanya kazi ili kuboresha teknolojia bila y akuwa bidhaa yoyote akilini, Bi Fung anasema.

OpenAI, kwa mfano, ilifanya kazi kama kampuni isiyo ya kiserikali kwa miaka kadhaa ilipotafiti mashine ya Transfomer kwa ajili ya elimu, ambayo hatimaye iliwezesha ChatGPT.

"Mazingira haya hayajawahi kuwepo katika makampuni mengi ya Kichina. Walitakiwa kuwekeza kwenye mifumo imara walipoona umaarufu wao," anaongeza. "Hii ni changamoto ya kimsingi kwa AI ya China."

Wawekezaji wa Marekani pia wamekuwa wakiunga mkono msukumo wa utafiti wa nchi hiyo. Mnamo 2019, Microsoft ilisema itawekeza dola bilioni moja kwenye teknolojia ya OpenAI.

"AI ni moja wapo ya teknolojia ya mabadiliko ya zama hizi na ina uwezo wa kusaidia kutatua changamoto nyingi duniani," mtendaji mkuu wa Microsoft Satya Nadella alisema.

Ushindani wa China

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

China, wakati huo huo, inafaidika na msingi mkubwa wa watumiaji. Ni nchi ya pili iliyo na watu wengi zaidi duniani, nyumbani kwa watu takriban bilioni 1.4.

Pia ina sekta ya mtandao inayostawi, anasema Edith Yeung, mshirika katika kampuni ya uwekezaji ya Race Capital.

Karibu kila mtu nchini anatumia programu bora zaidi ya WeChat, kwa mfano. Inatumika kwa karibu kila kitu kutoka kwa kutuma ujumbe wa maandishi, hadi kuweka miadi ya daktari na kutuma ushuru.

Kwa hivyo, kuna habari nyingi ambazo zinaweza kutumika kuboresha bidhaa. "Mtindo wa AI utakuwa mzuri tu kama data inayopatikana kwa kujifunza," Bi Yeung anasema.

"Kwa uzuri au ubaya, China ina sheria chache sana kuhusu faragha, na data nyingi zaidi [ikilinganishwa na Marekani]. Kuna utambuzi wa uso wa CCTV kila mahali, kwa mfano," anaongeza. "Fikiria jinsi hiyo hali hiyo ingekuwa muhimu kwa picha zinazozalishwa kwa mfumo wa AI."

Ingawa jumuiya ya teknolojia ya China inaweza kuonekana kuwa nyuma ya Marekani, watengenezaji wake wana uzoefu mkubwa, kulingana na Lee Kai-Fu, ambaye anajenga hoja katika kitabu chake AI Superpowers: China, Silicon Valley, na New World Order.

"Wanaishi katika ulimwengu ambao kasi ni muhimu, kunakili ni jambo linalokubalika, na washindani hawatafanya lolote ili kupata soko jipya," aliandika Bw Lee, mtu mashuhuri katika sekta ya teknolojia ya Beijing na mkuu wa zamani wa Google nchini China.

"Mazingira haya magumu na ya kusuasua yanatofautiana sana na Silicon Valley, ambapo kampuni huejiepusha na wazo sawa na la mwingine na badala yake kuzingatia wazo asilia."

Enzi ya China kuiba wazo la watu inakabiliwa na changamoto sihaba, ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusiana na hati miliki. Bw Lee anaandika kwamba imesababisha kizazi cha wafanyabiashara hodari na mahiri kutokuwa tayari kushindana.

Tangu miaka ya 1980, China imekuwa ikipanua uchumi wake, ambao ulikuwa ukiegemea zaidi kwenye viwanda, hadi ule unaotegemea teknolojia, Bi Fung anasema.

"Katika muongo uliopita, tumeshuhudia ubunifu zaidi kutoka kwa makampuni ya mtandao yanayoendeshwa na watumiaji wa China na miundo ya hali ya juu ya Kichina," anaongeza.

Je China inaweza kufikia Marekani?

Ingawa makampuni ya teknolojia ya China yanajivunia faida za kipekee, athari kamili ya sera ya udhibiti wa Beijing bado haijulikani.

Kuna maswali yanayoibuka kama vile, je, udhibiti unaweza kuathiri uundaji wa gumzo za AI za China. Je, wataweza kujibu maswali nyeti kuhusu Rais Xi Jinping?

"Sidhani kama kuna mtu yeyote nchini China atauliza maswali ya kutatanisha kuhusu Baidu au Ernie. Wanajua kuwa imedhibitiwa," Bi Yeung anasema. "Mada nyeti ni sehemu ndogo sana ya matumizi [ya chatbots]. Zinaangaziwa sana na vyombo vya habari," Bi Fung anaongeza.

Wasiwasi mkubwa zaidi ni kwamba juhudi za Marekani za kuzuia China kufikia teknolojia maalum zinaweza kuathiri sekta ya AI ya pili.

Chipu za kompyuta zinazofanya kazi vizuri, au halvledare, sasa ndizo chanzo cha mvutano mkubwa kati ya Washington na Beijing.

Zinatumika katika bidhaa za kila siku ikiwa ni pamoja na vipakatalishi au komyuta ya mkononi na simu za kisasa, na zinaweza kuwa na matumizi ya kijeshi. Pia ni muhimu kwa vifaa vinavyohitajika kujifunzia teknolojia ya akili bandia.

Kampuni za Marekani kama Nvidia kwa sasa zinaongoza katika kutengeneza chipu za AI na "kampuni chache [za Kichina] zinaweza kushindana dhidi ya ChatGPT" kutokana na vikwazo vya kuuza nje, Bi Fung anasema.

Ni wazi kwamba hii itaathiri sekta za teknolojia ya juu nchini China kama vile akili bandia ya kisasa, haitaathiri uzalishaji wa teknolojia ya watumiaji, kama vile simu za mkononi na kompyuta ndogo. Hii ni kwa sababu "udhibiti wa usafirishaji nje umewekwa ili kuzuia China kufikia teknolojia ya akili bandia ya hali ya juu kwa madhumuni ya kijeshi," Bi Schaefer anasema.

Ili kuondokana na hili, China inahitaji kuwa na Silicon Valley yake binafsi - utamaduni wa utafiti unaovutia vipaji kutoka asili mbalimbali, Bi Fung anasema.

"Hadi sasa imetegemea vipaji vya ndani na wale wa kutoka ng'ambo wenye asili ya Kichina. Kuna kikomo cha fikra za kitamaduni zinazofanana," anaongeza.

Beijing imekuwa ikijaribu kuziba pengo hilo kupitia "Big Fund", ambayo inatoa motisha kubwa kwa makampuni ya chip.

Lakini pia imeimarisha uweledi wake katika sekta hiyo. Mwezi Machi, Zhao Weiguo alikua tajiri wa teknolojia ya hivi punde kutuhumiwa na mamlaka kwa ufisadi.

Mtazamo wa Beijing kwenye tasnia fulani unaweza kuleta motisha za kifedha na kulegeza masharti, lakini pia unaweza kumaanisha uchunguzi zaidi, na hofu zaidi na kutokuwa na uhakika.

"Kukamatwa kwa Zhao ni ujumbe kwa makampuni mengine yanayomilikiwa na serikali: usichanganye na pesa za serikali, haswa katika nafasi ya chip," Bi Schaefer anasema. "Sasa ni wakati wa kuendelea na kazi."

Jinsi ujumbe huo utaathiri mustakabali wa tasnia ya AI ya Uchina bado ni suala linalosubiriwa kuonekana.