Maeneo hatari yanayozuia mashambulizi ya Ukraine dhidi ya Urusi

Chanzo cha picha, JOE PHUA
Mwanajeshi wa Ukraine anajikokota kwenye nyasi ndefu, mguu mmoja unaochechemea ukifuata nyuma.
Sekunde chache baadaye, mwako wa rangi ya chungwa angavu na wingu la moshi mweupe unaonekana umbali wa mita chache tu, ambapo bomu jingine la ardhini limelipuka.
Mwanajeshi wa pili aliyejeruhiwa vibaya anajisogeza hadi kwenye eneo salama katika shehena yenye silaha iliyo karibu - silaha zikiruka kama mwogeleaji anayejaribu kung'ang'ania kupanda boti ya kuokoa maisha - damu nyekundu nzito inaashiria maumivu makali anayopitia.
Haya yote yalinaswa moja kwa moja, wiki iliyopita, na ndege isiyo na rubani ya jeshi la Ukraine iliyokuwa ikipaa juu kwenye eneo la vita kusini mwa mji wa Donbas wa Bakhmut.
Kutoka juu, uwanja wenye mabomu ulionekana usio na mpangilio wenye mazao ya hudhurungi iliyokolea.
"Mabomu yanatisha. Yananitisha kuliko kitu kingine chochote," alisema Artyom, mwanajeshi mwenye umri wa miaka 36 kutoka Kikosi cha 108 cha Ulinzi wa Eneo la Ukraine.
Siku mbili kabla, wenzake wawili walikuwa wamesimama kwenye "petali" - ndogo, za kijani kwenye mabomu ya ardhini - ambayo yalikuwa ndiyo tu yametawanywa hivi karibuni kwenye uwanja na roketi za Urusi.
"Watu wetu walikuwa na uzoefu. Lakini ni vigumu macho yako kuangalia kila mahali. Wote wawili wamekatwa mguu. Mguu mmoja kila mmoja. Tuna majeraha kutokana na mabomu baada ya kila mapigano," alisema Artyom, mwanajeshi wa kikosi cha sapper mwenye uzoefu akieleza kuwa roketi hizo huwezesha wanajeshi wa Urusi kuweka mabomu mpya katika maeneo ambayo tayari yamekombolewa na vikosi vya Ukraine.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwa vile mashambulizi ya muda mrefu ya Ukraine bado hayajafikia aina ya mafanikio ambayo wengine walitarajia - ikiwa ni pamoja na Rais Volodymyr Zelensky ambaye alikiri yalitekelezwa "polepole kuliko ilivyotarajiwa".
Wanajeshi kadhaa ambao tumezungumza nao kwenye sehemu tofauti vitani wamelaumu maeneo yenye mabomu ya Urusi kuwa sehemu ya ucheleweshaji huo.
"Bila shaka, inapunguza kasi ya harakati za wanajeshi," alisema Dill, kamanda wa kikosi cha watu tisa cha kijeshi cha sapper. Alikuwa amemaliza tu kazi ya uondoaji mabomu ya ardhini vitani karibu na mashariki ya kijiji kidogo, kilichoharibiwa cha Predtechyne, nje ya Bakhmut. Aliweka safu ya mabomu yaliyoharibiwa ya Urusi yaliyokuwa chini ya mti, akiwa makini kuhakikisha kuwa hangeweza kuonekana na ndege zisizo na rubani za Urusi.
"Adui hawana huruma kwa wanajeshi wao wenyewe. Wanatumika kama wanajeshi ambao sio muhimu sana vitani. Lakini tunajaribu kusonga mbele na idadi ndogo ya majeruhi," alisema Luteni Serhii Tyshenko kutoka Kikosi cha 3 cha Mashambulizi, akizungumza kutoka eneo alilopojihifadhi lililo karibu.
Kwa mwendo wa saa tatu kwa gari kuelekea kusini, kuvuka majukwa ya madaraja yenye ncha-upande, kikosi cha sapper cha Ukraine wakiwa wamejikunyata kando ya barabara iliyoporomoka, wakiyamaliza nguvu kwa uangalifu mabomu ya ardhini yaliyofichwa karibu na nguzo ya umeme, wakiwa tayari kutuma makombora kwa wanajeshi wanaotembea kwa miguu au magari.

Chanzo cha picha, JOE PHUA
"Ninachukia kazi hii," Artyom, fundi wa zamani wa gereji mwenye ndevu nyekundu, muda mfupi baada ya kumaliza kazi ya kuondoa mabomu na kuhakikisha eneo ni salama. Kulisikika filimbi, kisha mshindo mkubwa kama kombora la Urusi liligonga uwanja wa karibu.
Juu ya kilima kilicho karibu, wanajeshi wanaotembea kwa miguu wa Ukraine walikuwa wakisonga mbele polepole upande wa kusini zaidi katika kijiji kipya cha Rivnopil kilichotekwa.
Hasira ya Artyom haikuwa tu walivyoshughulikia maeneo hatari yenye mabomu lakini jinsi alivyohisi kwa kitendo cha kuwekwa mabomu na mtego ambao hauna madhara wenye kilipuzi kilichofichwa kilichoundwa ili kulipuka mtu anapokigusa, badala ya kupigana na adui yako "moja kwa moja".
Baadaye, katika kambi yao ya muda katika jumba lililo umbali wa kilomita kadhaa, wanajeshi walionyesha kufadhaika kuhusu ukosefu wa vifaa vya kuondoa mabomu, na uhaba wa wanajeshi wa sapper - wanne kati yao walikuwa wamejeruhiwa katika wiki za hivi karibuni.
Lakini kisha Artyom alituonyesha antena kubwa na akatoa kompyuta ya mkononi ili kuanza kucheza rekodi za kile alichosema ni miito ya hivi majuzi ya redio ya wanajeshi wa Urusi.
Jumbe zilizojaa matusi zilionekana kuashiria kiwango cha machafuko na ari ya chini.
"Ndege yetu isiyo na rubani ya kamikaze iligonga gari [letu]. Tuna mmoja aliyekufa, mwingine amejeruhiwa."
"[Wanajeshi] wanakimbia. Baadhi yao wanaiba magari... watu 50 wamekimbia. [Wametoroka] ..."
Kituo cha redio kilipendekeza kwamba wanajeshi wa Urusi walikuwa wakiondoka kwenye nafasi zao baada ya shambulio la mizinga la Ukraine.
"Hii hutokea mara kwa mara. Katika makundi ya 10 au 20 - [Warusi] hutoweka na kuondoka bila ruhusa. Warusi wametambua kuwa tunaweza kusikiliza mawasiliano yao lakini wakati mwingine wanasahau," alisema Artyom.
Alijieleza kuwa "mkweli" kuhusiana na hatua ya Ukraine ya kukabiliana na mashambulizi, akiamini kuwa watu wengi sana "katika vyombo vya habari na katika jamii wana haraka", na wanatarajia maendeleo ya ghafla.
"Ninaamini chaguo baya zaidi daima linawezekana. Mbaya zaidi ni kupiga hatua polepole," alisema.

Chanzo cha picha, JOE PHUA
Ndege mbili za kivita za Ukraine zilipaa chini chini kwa sauti ya kishindo, na kufuatiwa na msururu wa sauti kubwa kutoka eneo la vita kusini zaidi.
Muda mfupi baadaye, tuliweza kusikia mizinga na kile kilichosikika kama mfumo wa makombora ya masafa marefu wa HIMARS ukitua kwenye maeneo yaliyokuwa na wanajeshi wa Kirusi.
Mashambulizi ya kukabili ya Ukraine yanaweza kuwa ya polepole, na yenye kutekelezwa kwa tahadhari kiasi katika hatua hii.
Lakini afisa mmoja alipendekeza kuwa mbinu hii ya polepole ingeonyesha matokeo hivi karibuni kwa njia ya kushangaza, kwani mashambulizi ya masafa marefu yaliharibu uwezo wa Urusi kuhami tena wanajeshi walio vitani, na ari ya chini ya Urusi ilitoa fursa za mafanikio ya kimkakati kwa vikosi vya Ukraine.
"Utaona hili hivi karibuni," alisema.
Kuhusu sehemu kubwa za maeneo yenye mabomu ya ardhini mbele ya wanajeshi wa Ukraine wanaotekeleza shambulio la kukabili - Dill, kamanda wa kikosi cha kijeshi cha sapper karibu na Bakhmut, alikuwa anajiamini.
"Tunajifunza kujiboresha na kubuni mbinu za kutengeneza njia kwa haraka na salama katika maeneo yenye mabomu. Lakini tunapambana na adui mbaya sana," alisema.












