Argentina yashinda fainali ya Kombe la Dunia 2022 - katika picha

Argentina wameibuka kuwa mabingwa wa Kombe la Dunia 2022 kwa mara ya tatu baada ya kuishinda Ufaransa kwa mikwaju ya penalti katika fainali iliyofanyika Qatar.

Gonzalo Montiel alifunga goli la penalti na kulipa taifa la Amerika ya kusini ushindi wa 4-2 kwenye magoli ya penalti, baada ya mchezo mkali kumalizika kwa 3-3 baada ya muda wa ziada.

Lionel Messi alifunga mabao mawili na Angel di Maria akaifungia Argentina, huku Mfaransa Kylian Mbappe akiwa mchezaji wa kwanza tangu Geoff Hurst mwaka 1966 kufunga magoli matatu katika fainali ya Kombe la Dunia.

Hatimaye Argentina waliibuka kidedea na kunyakua taji lao la tatu la dunia, huku Messi akitwaa taji la kipekee kwa kunyanyua taji la dhahabu kwenye Uwanja wa Lusail.

Hizi hapa ni simulizi za mechi ya kandanda ya ajabu, iliyosimuliwa kupitia picha bora zaidi za fainali...