Argentina yashinda fainali ya Kombe la Dunia 2022 - katika picha

Argentina wameibuka kuwa mabingwa wa Kombe la Dunia 2022 kwa mara ya tatu baada ya kuishinda Ufaransa kwa mikwaju ya penalti katika fainali iliyofanyika Qatar.

Gonzalo Montiel alifunga goli la penalti na kulipa taifa la Amerika ya kusini ushindi wa 4-2 kwenye magoli ya penalti, baada ya mchezo mkali kumalizika kwa 3-3 baada ya muda wa ziada.

Lionel Messi alifunga mabao mawili na Angel di Maria akaifungia Argentina, huku Mfaransa Kylian Mbappe akiwa mchezaji wa kwanza tangu Geoff Hurst mwaka 1966 kufunga magoli matatu katika fainali ya Kombe la Dunia.

Hatimaye Argentina waliibuka kidedea na kunyakua taji lao la tatu la dunia, huku Messi akitwaa taji la kipekee kwa kunyanyua taji la dhahabu kwenye Uwanja wa Lusail.

Hizi hapa ni simulizi za mechi ya kandanda ya ajabu, iliyosimuliwa kupitia picha bora zaidi za fainali...

france

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baada ya mechi 63 ndani ya mwezi mmoja, fainali ya Kombe la Dunia 2022 , Argentina iliibuka na ushindi dhidi ya Ufaransa kwenye Uwanja wa Lusail. Baada ya kumalizika kwa mchuano huo hiyo, hafla kuu ilianza ...
m

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Argentina walianza kwa nguvu zaidi na wakapewa penalti dakika ya 23 wakati Ousmane Dembele alipomuangusha Angel di Maria. Na Messi aliingilia kati na kuipa nchi yake ushindi.
m

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Argentina waliongoza katika kipindi cha kwanza, Di Maria alikamilisha shambulizi la haraka la kukabiliana na Hugo Lloris.
m

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baada ya kushindwa kupiga shuti hata moja hadi dakika ya 67, Kylian Mbappe aliipa Ufaransa matumaini kwa mkwaju wa penalti baada ya Nicolas Otamendi kumchezea vibaya Randal Kolo Muani.
m

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Matumaini yalibadilika na kuwa shangwe wakati Mbappe alipomshinda Emi Martinez na kufanya matokeo kuwa 2-2. Mabao mawili ya kwanza ya mshambuliaji huyo yalitenganishwa kwa sekunde 97 pekee
m

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mchezo ulikwenda mpaka muda wa ziada, na Messi alikuwa ameipa ushindi Argentina ,Jitihada za Jules Kounde kutaka kuokoa ziliambulia patupu
mbape

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lakini Mbappe, nyota wa PSG alifanya matokeo kuwa 3-3...
m

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, ...na kuwa mchezaji wa kwanza kwa miaka 56 kufunga matatu ya fainali ya Kombe la Dunia. Baada ya penati tatu ndani ya dakika 120, mchezo ulipaswa kuamuliwa kwa mikwaju.
n

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbappe na Messi walipiga penalti za kwanza na wote wakafunga. Kisha akapanda Mfaransa Kingsley Coman - ambaye alikosa kwa kipa wa Aston Villa Emiliano Martinez.
m

Chanzo cha picha, Getty Images

m

Chanzo cha picha, Getty Images

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Montiel alifunika uso wake kwa tshirt lake kwa hisia ya furaha, kabla ya kuandamwa na wachezaji wenzake wenye furaha.
m

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Huu ulikuwa ushindi wa tatu wa Kombe la Dunia kwa Argentina, baada ya 1978 na 1986. Ushindi huu unakuja baada ya miaka miwili ya kifo cha Diego Maradona, ambaye aliipatia nchi yake ushindi katika fainali hizo mbili.
m

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Usiku wa Jumapili, Messi aling'ara duniani kote