Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni kweli vita vya Iran na Israel vimesitishwa au danganya toto?
Rais wa Marekani, Donald Trump, alitangaza Jumapili jioni kuwa Israel na Iran zimekubaliana kusitisha mapigano, akisema kuwa makubaliano hayo yanaweza kuleta amani ya kudumu. Tangazo hili linakuja baada ya siku 12 za mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya Iran, mashambulizi ya kulipiza kisasi ya makombora na ndege zisizo na rubani kutoka Iran dhidi ya Israel, na mashambulizi ya Marekani kwenye maeneo ya nyuklia ya Iran.
Ingawa nchi zote mbili zimesema zitakubali usitishaji vita iwapo zitaacha kushambuliana, Rais Trump amezishutumu Israel na Iran kwa kukiuka makubaliano hayo.
Hata hivyo, inaonekana makubaliano hayo yamekuwa yakifanya kazi kwa muda sasa. Kuna matumaini makubwa kwamba usitishaji vita huu utasababisha amani ya kudumu. Lakini je, usitishaji vita ni sawa na amani ya kudumu?danganya toto? Uzoefu wa zamani unaonyesha nini? Na ni kiasi gani cha diplomasia kinahitajika kufikia hilo?
Usitishaji vita unamaanisha nini?
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN), hakuna ufafanuzi mmoja unaokubalika kimataifa wa neno "usitishaji vita," ingawa neno hilo linatokana na amri ya kijeshi "cease fire," ambayo inamaanisha kinyume cha ile ya amri "open fire." Maana yake inaweza kutofautiana kulingana na mazungumzo kati ya pande mbili zinazopigana.
Hata hivyo, UN mara nyingi inasema kuna tofauti kati ya maneno "usitishaji vita" na "kusitisha mapigano."
Usitishaji vita unahusisha kuundwa kwa makubaliano rasmi, ambayo yanajumuisha:
- Sababu ya usitishaji vita
- Hatua inayofuata ya kisiasa
- Lini utatekelezwa
- Wapi utafanya kazi
Inaweza pia kueleza ni shughuli gani za kijeshi zinaruhusiwa na zisizoruhusiwa, na jinsi usitishaji vita utakavyofuatiliwa.
Kwa mfano, vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia vilimalizika mwaka 1993 wakati pande mbili zilizokuwa zinasigana na kupigana nchini humo zilifikia makubaliano.
Je, usitishaji vita ni wa kudumu au wa muda?
Inaweza kuwa mojawapo ya aina hizo mbili, kulingana na UN.
Wakati mwingine pande zinazopingana zinaweza kukubaliana na usitishaji vita wa muda au usitishaji vita wa awali kabla ya kufanya operesheni yoyote. Hii inaweza kuwa kupunguza ghasia au kupunguza migogoro ya kibinadamu.
Makubaliano ya usitishaji vita yanaweza kujadiliwa ili kuunda mazingira yanayoruhusu mazungumzo kutafuta suluhisho la amani ya kudumu.
Israel na makundi ya wanamgambo yanayoongozwa na Hamas walikubaliana na usitishaji vita wa muda, ambao ulifanyika kati ya Septemba 24 na Septemba 30, 2023. Hamas waliwaachia mateka 105 badala ya wafungwa wapatao 240.
Usitishaji vita wa muda unaweza pia kukubaliwa ili kukuza mazingira ambayo yangeisaidia mazungumzo na kusaidia kuweka mkondo wa usitishaji vita wa kudumu, au wa mwisho.
Mnamo 2000, usitishaji vita wa muda kati ya jeshi la Ethiopia na Eritrea ulisababisha kusainiwa kwa makubaliano ya amani ya kudumu.
Je, kuna ukomo kwenye kusitisha vita?
Israel na Hamas walitangaza usitishaji vita wa muda mnamo Machi 2023 kama "kipindi cha kibinadamu." Wakati wa baadhi ya misaada ya kibinadamu, hutumika kupunguza ghasia au kupunguza migogoro ya kibinadamu.
Kwa mfano, serikali ya Sudan ilikubaliana na usitishaji vita na makundi mawili yenye silaha, harakati ya ukombozi wa Sudan na harakati ya haki na usawa, na hivyo kumaliza mapigano ya siku 45 huko Darfur na kuruhusu mashirika ya kibinadamu kuwaokoa wakazi.
Baada ya Indonesia kugongwa na tsunami mwaka 2004, serikali ya Indonesia na Harakati ya Ukombozi ya Aceh zote zilitangaza usitishaji vita ili kuruhusu misaada kufika maeneo ambapo walikuwa wakipigana.
Pia kunaweza kuwa na makubaliano ya kusitisha mapigano katika eneo maalum, yanayoitwa usitishaji vita wa kijiografia. Mnamo 2018, Umoja wa Mataifa ulijadili makubaliano kati ya serikali ya Yemen na Wahouthi kusitisha mapigano karibu na bandari ya Hodeida ya Bahari Nyekundu ili kulinda wakazi.
Tunasubiri kuona kama ni kweli vita vya Iran na Israel vimesitishwa, vitakoma au ni danganya toto?