Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 11.12.2023

Raphael Varane

Chanzo cha picha, Getty Images

Raphael Varane huenda akaondoka Manchester United mwezi Januari kwa vile beki huyo wa zamani wa Ufaransa, 30, hana uhusiano mzuri na kocha Erik ten Hag. (Nicolo Schira)

Tottenham sasa wanaongoza Newcastle katika mbio za kumsajili winga Mwingereza Samuel Iling-Junior, 20, kutoka Juventus. (Football Insider)

Fulham wanaimarisha mpango wao wa kumnunua kiungo wa Le Havre raia wa Senegal Arouna Sangante, 21. (Sun).

Fulham pia wameonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa Fluminense wa Brazil Andre, 22. (Nicolo Schira)

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Samuel Iling-Junior

Liverpool ni miongoni mwa klabu za Ligi ya Premia zinazomtaka mshambuliaji wa Kijerumani Maximilian Beier, 21, ambaye anatarajiwa kuondoka Hoffenheim msimu ujao. (Sky Sports Ujerumani)

Everton wako tayari kumuuza beki wa England Ben Godfrey, 25, kwa Tottenham mwezi Januari iwapo dau litawasilishwa. (Football Insider)

Manchester United wametoa ofa ya kuongeza mara dufu mishahara ya beki wa Barcelona Ronald Araujo, 24, ambaye hana nia ya kuhamia Bayern Munich ,wezi Januari mwakani. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Ben Godfrey

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Everton wako tayari kumuuza beki wa England Ben Godfrey

Mshambuliaji Mfaransa Mathys Tel, 18, ameamua kusalia Bayern Munich hadi msimu ujao, licha ya klabu kadhaa kutaka kumsajili kwa mkopo, ikiwa ni pamoja na Manchester United. (Sky Sports Germany)

Chelsea wamefanya mazungumzo na Palmeiras kuhusu dili la kumsajili winga wa Brazil Estevao Willian, 16, anayejulikana kama 'Messinho', ambaye pia amewavutia Barcelona. (Goal, via Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Mikel Arteta amemwalika gwiji wa Arsenal Dennis Bergkamp kurejea katika klabu kama sehemu ya wakufunzi wa chuo chao cha soka. (Football transfers)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi na kuhaririwa na Yusuf Jumah