Salman Rushdie: Mwandishi wa vitabu anayesaidiwa kupumua na hana uwezo wa kuzungumza, anasema wakala

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakala wa Salman Rushdie alisema kuwa"habari sio njema" baada ya mwandishi kudungwa kisu katika tukio katika jimbo la New York.
Alishambuliwa jukwaani, na sasa anasaidiwa kupumua na mashine ya ventilator na hawezi kuzungumza, Andrew Wylie alisema katika taarifa, akiongeza kuwa mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 75, anaweza kupoteza uwezo wa kuona wa jicho moja.
Bw Rushdie ameumia na miaka ya vitisho vya Waislamu baada ya kuandika Aya za Shetani, zilizochapishwa katika mwaka 1988.
Polisi walimkanmata mshukiwa aliyetajwa kwa jina la Hadi Matar, 24, kutoka Fairview, New Jersey.
Polisi ya jimbo la New York State ilisema kuwa mshukiwa alikimbia kwenye jukwaa na kumshambulia Bw Rushdiena na mtu aliyekuwa akihojiwa katika taasisi ya Chautauqua mwagharibi mwa jimbo la New York.
"Salman huenda akapoteza uwezo wa kuona wa jicho moja; neva kwenye mkono wake ziliumia, na ini lake lilidungwa kisu na kuharibika,"alisema wakala wake.
Hakuna sababu au mashitaka yaliyothibitishwa na polisi , ambao wako katika mchakato wa kutafuta vibali vya kuchunguza vifaa vya kielekroniki vilivyopatikana katika kituo aliposhambuliwa.
Bw Rushdie alidungwa kisu walau mara moja kwenye shingo na tumboni, walisema maafisa. Alipelekwa katika hospitali katika Erie, Pennsylvania, kwa helikopta.

Chanzo cha picha, Reuters
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mtu aliyekuwa akihojiwa ambaye alikuwa pamoja naye kwenye jukwaa, Henry Reese, alipata jeraha dogo kichwani na akapelekwa katika hospitali iliyopo karibu. Bw Reese ni muasisi mwenza wa shirika linalotoa hifadhi kwa waandishi walioko mafichoni kutokana na tisho la kuuawa.
Polisi waliuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba mhudumu na mmoja wa watu katika hadhira alikuwa wamemkumbiza mshambuliaji na kumpeleka kwenye uwanja, halafu akakamatwa.
Linda Abrams, ambaye alitazama tukio la shambulio hilo kutoka mji wa Buffalo, aliliambia gazeti la The New York Times kwamba mshambuliaji aliendelea kujaribu kumshambulia Bw Rushdie hata baada ya kuzuiliwa.
"Ilichukua kama wanaume watano kumvuta mbali na alikuwa bado anataka kumdunga kisu - ," alisema Bi Abrams . "Alikuwa na hasira, hasira. Alikuwa mwenye nguvu na mwepesi."
Mtu mwingine aliyeshuhudia tukio hilo, Rita Landman, aliliambia gazeti hilo kwamba Bw Rushdie alionekana kuwa hai mara baada ya kushambuliwa.
"watu walikuwa wanasema, 'Ana mapigo ya moyo, ana mapigo ya moyo, ana mapigo ya moyo '," alisema.
Video iliyotumwa kwenye mtandao inaonyesha wakati watu walipokimbia kwenye jukwaa kumzuia mshambuliaji na kuwasaidia wanaume waliojeruhiwa. Polisi walisema daktari aliyekuwa miongoni mwa hadhira alimpatia Rushdie huduma ya kwanza.
Mwandishi wa riwaya mzaliwa wa India Rushdie alipata umaarifu kwa kitabu chake kilichojulikana kama Midnight's Children katika mwaka 1981, ambacho kiliuza nakala zake zaidi ya milioni moja nchini Uingereza pekee.
Lakini kitabu chake cha nne, kilichochapishwa mwaka 1988 - The Satanic Verses – (Aya za Shetani) kilimlazimisha kwenda mafichoni kwa karibu miaka kumi.
Kitabu chake kiliibua malalamiko miongoni mwa baadhi ya Waislamu, ambao walichukulia maudhui yake kama kukufuru Uislamu, na kikapigwa marufuku katika baadhi ya nchi.
Watu kadhaa waliuawa katika ghasia za kumpinga -Rushdie nchini India na ubalozi wa ubalozi wa Uingereza katika mji mkuu wa Iran, Tehran, ulipigwa mawe.
Mwaka 1991 Mjapan aliyekiandika kitabu hicho kwa lugha ya Kijapan alidungwa kisu hadi kufa, huku mtu mwingine aliyekibadilisha kitabu kwa lugha ya Kiitalia pia akidungwa kisu hadi kufa, na mchapishaji wa kitabu hicho wa Norway, William Nygaard, alipigwa risasi – lakini akanusurika.
Akizungumza kuhusu shambulio la Ijumaa, Bw Nygaard alisema Bw ushdie ni "mwandishi mkuu ambaye amekuwa na maana kubwa sana kwa fasihi" ambaye amelipa "gharama ya juu" kwa kazi yake.
Mwaka mmoja baada ya kutolewa kwa kitabu hicho, Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Khomeini alitoa wito wa Bw Rushdie kunyongwa. Aliyoa kiasi cha dola milioni 3 (£2.5m) kama zawadi katika fatwa – amri ya kisheria inayotolewa na kiongoni wa dini ya Kiislamu.
Zawadi hiyo kwa mtu atakayepata kichwa cha Bw Rushdie bado imesalia kuwepo na ingawa serikali ya Iran imejitenga na agizo kutoka kwa Khamanei , maafisa wa wakfu wa kidini wa Iran waliongeza $500,000 kwenye malipo ya zawadi katika mwaka 2012.
Bw Rushdie mwenye uraia wa Uingereza na Marekani ambaye alizaliwa kwa wazazi ambao sio Waislamu na ambaye binafsi hamuamini Mungu – amekuwa mtetezi wa uhuru wa kujieleza, akitetea kazi yake katika matukio kadhaa.
Wakati Bw Rushdie alipotuzwa tuzo ya heshima na Malkia mwaka 2007, iliibua maandamano katika mataifa ya Iran na Pakistan, ambako Waziri mmoja alisema tuzo hiyo "inahalalisha mashambulio ya kujitoa muhanga".
Matukio kadhaa ya fasihi yaliyohudhuriwa na Bw Rushdie yamekumbwa na vitisho vya mashambulizi na ususiwaji – lakini anaendelea kuandika
Riwaya yake ijayo Victory City, inatarajiwa kuchapishwa February 2023.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson alituma ujumbe wa Twitter : "Nimeshtushwa na kwamba Sir Salman Rushdie amedungwa kisu wakati akitekeleza haki yake hatupaswi kukoma kulinda."
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliandika kwamba Bw Rushdie "alijumuisha uhuru na mapambano dhidi ya kupinga ukweli" na alikuwa mhanga "wa shambulio la wogo lililofanywa na vikosi vya chuki na ukatili".
Mwandishi na mbunifu wa michoro ya riwaya Neil Gaiman alisema "alishitushwa na kusikitishwa " na shambulio dhidi ya rafiki yake na mwandishi mwenzake.
"Ni mtu mwema na mwenye akili na ninatumaini yuko sawa," Gaiman aliandika kwenye Twitter.
Katika taarifa yao, wachapishaji wa vitabu vya Bw Rushdie katika Penguin Random House walisema : "Tunalaani ghasia hii ya shambulio lililofanyika katika umma, na tunaungana na Salman na familia yake katika kipindi hiki cha huzuni ."
Mwandishi mwenzke Taslima Nasreen, ambaye alilazimika kuikimbia nyumba yake mjini Bangladesh baada ya mahakama kusema kuwa riwaya yak, Lajja ilitusi imani ya dini ya Waislamu, alisema sasa anahofia usalama wake kutokana na shambulio la Bw Rushdie.












