Tetesi za soka Ulaya Jumatano 18.01.2023

Kampuni ya bilionea wa Uingereza Sir Jim Ratcliffe ya Ineos imetangaza rasmi nia ya kuinunua Manchester United.
Wamiliki wa United, familia ya Glazer walisema mnamo Novemba kwamba walikuwa wakifikiria kuuza klabu hiyo huku "wakitafuta njia mbadala za kimkakati".
Ineos ilisema kampuni hiyo "ilijiweka rasmi katika mchakato".
Ratcliffe alitoa ofa ya mwisho ya pauni bilioni 4.25 bila kufanikiwa kuinunua Chelsea mwaka jana baada ya mmiliki wa Urusi Roman Abramovich kuiuza klabu hiyo ya London.

Chanzo cha picha, EPA
West Ham wanatafuta kufanya uhamisho wa kumnunua beki wa kati wa Uingereza Harry Maguire, 29, kwa mkopo kutoka Manchester United. (Mirror)
Winga wa Manchester United Alejandro Garnacho bado hajasaini mkataba mpya katika klabu hiyo ya Old Trafford, huku wawakilishi wa Muargentina huyo wakitaka zaidi ya pauni 20,000 kwa wiki ambayo imekuwa ikitolewa. Real Madrid na Juventus wanafuatilia hali ya kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye mkataba wake utaendelea hadi 2024 na ana chaguo la kuongezwa kwa mwaka mmoja. (Independent)
Arsenal wamefanya mawasiliano ya awali na Bayer Leverkusen kuhusu winga wa Ufaransa Moussa Diaby lakini klabu hiyo ya Ujerumani haitaki kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 mwezi Januari. (Sky Sports)
Barcelona wana nia ya dhati ya kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan kwa uhamisho wa bila malipo msimu wa joto wakati mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 na Manchester City utakapokamilika. (Telegraph - usajili unahitajika)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wanafuatilia mustakabali wa fowadi wa Brighton Leandro Trossard, ambaye amekuwa akihusishwa na Arsenal na Tottenham, huku Seagulls wakitarajiwa kupokea chini ya pauni milioni 25 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, 28. (Mirror)
Leicester City imekuwa na ofa ya pauni milioni 30 kumnunua mshambuliaji wa Argentina Nicolas Gonzalez, 24, iliyokataliwa na klabu ya Italia Fiorentina. (90 Minutes)
Southampton wanakaribia kupata mkataba wa kudumu kwa mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 21, ambaye thamani ya Villarreal ni euro 20m (£17.7m). (Usajili unahitajika)

Chanzo cha picha, Getty Images
Crystal Palace wana nia ya kumrejesha kiungo wa kati wa Chelsea Conor Gallagher katika klabu hiyo, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 22 alionyesha kiwango kizuri kwa mkopo na The Eagles msimu uliopita. (Sky Sports)
Mkurugenzi wa michezo wa Napoli Cristiano Giuntoli anasema ana "matumaini" klabu inaweza kumsajili kiungo wa kati wa Angers na Morocco Azzedine Ounahi, 22, ambaye pia amekuwa akihusishwa na Aston Villa na Leeds United. (Sport Mediaset, kupitia Football Italia)
Ajenti wa winga wa Ubelgiji Yannick Carrasco anasema kuwa mazungumzo yanafanyika kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kwenda Barcelona kutoka Atletico Madrid, huku fowadi wa Uholanzi Memphis Depay, 28, akielekea kinyume. (Nieuwsblad - kwa Kiholanzi)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kipa wa Ujerumani h, 29, anatarajiwa kuongeza mkataba wake na Newcastle United zaidi ya Januari huku mazungumzo yakifanyika kati ya pande hizo mbili. (Mail)
Bayern Munich wamekuwa na ofa ya euro 8m (£7m) na euro 1m (£885,000) kama nyongeza kwa mlinda lango wa Uswizi Yann Sommer, 34, iliyokataliwa na Borussia Monchengladbach. (Florian Plettenberg)
Aliyekuwa meneja wa Leeds United , Marcelo Bielsa ndiye mgombea anayependekezwa na Shirikisho la Soka la Mexico kuchukua nafasi ya bosi wa timu yao ya taifa ya wanaume. (ESPN)












