Unakosa usingizi? Kuandika orodha ya mambo ya kufanya kutakusaidia

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Claudia Hammond
- Nafasi, BBC News
- Muda wa kusoma: Dakika 4
Ikiwa una tatizo la kupata usingizi, basi suluhisho ni haraka-kuwa na kalamu na karatasi.
Ukipata shida ya kupata usingizi, utagundua kinachokunyima usingizi ni kufikiria sana mambo ambayo unatarajia kuyafanya siku inayofuata,hasa kazi ambazo umeanza lakini bado hujamaliza.
Katika utafiti uliofanyiwa wafanyikazi katika kampuni ya TEHAMA ya Ujerumani, wale ambao walikuwa na kazi ambazo hazijakamilika zilizosalia mwishoni mwa juma la kazi walikuwa na uwezekano zaidi wa kufikiria matatizo yao ya kazi mwishoni mwa juma ikilinganishwa na wale ambao walikuwa hawana kazi nyingi walizobakisha.
Mtafiti Christine Syrek kutoka Chuo Kikuu cha Trier aliandika kwamba matokeo yao yalionyesha kwamba "hali ya kutokamilisha kazi za wiki huathiri afya ya wafanyikazi na kusababisha kutopata usingizi hasa wikendi, na pia athari za kutokuwa na muda huchangia hili".
“Muendelezo wa kiakili”ni kufikiria sana mambo mabaya yaliyowahi kukutokea au unatarajia yatokee siku za usoni.Watu wakiwa katika hali hii pia hujipata wakitatizika kupata usingizi wa kutosha katika likizo ya wikendi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Usiku wa Jumapili huwa una changamoto zake.
Iwapo unashughuli asubuhi inayofuata unaweza kukosa usingizi.Unawaza majukumu yaliyo mbele yako unayotarajia kuyatekeleza na mapya ambayo pia hujayamaliza.
Je ni kipi unapaswa kufanya ili upate usingizi mnono na kutofikiria sana?
Unaweza hesabu kama vile kondoo.Ama usome kitabu kwa muda ,au ufikirie mambo ambayo hayazunguki mazingira yako ya kawaida.Unawaza ukiwa makini ,na kusikiliza mapigo ya moyo wako na hisia ambazo zinakuzunguka.Ama uamke na uandike mambo yote unayotarajia kufanya siku ifuatayo ili akili itulie.
Yamkini,hatua hii ya kuorodhesha mambo unayopanga kuyafanya husaidia sana na imepatiwa uzito baada ya utafiti kufanywa Marekani nakubainika husaidia kutuliza ubongo na kupata usingizi kwa haraka.
Kwa mfano , mkurugenzi wa Maabara ya Neuroscience na Utambuzi wa Usingizi katika Chuo Kikuu cha Baylor nchini Marekani, Michael Scullin, aliuliza kikundi kimoja cha watu waliojitolea kuandika orodha kabla tu ya kulala ya kila kitu ambacho wamefanikiwa kufanya , na kikundi cha pili kuandika orodha, kuhusu kazi walizopaswa kufanya kukamilisha majukumu yao hapo kesho , ni kundi hili la pili ambalo baadaye lilipata usingizi kwa haraka zaidi.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Badala ya kuwa na kazi zinazozunguka kichwani mwako bila mpangilio, zinawekwa katika mpangilio wa aina fulani.
Na ni haraka kiasi gani? Ni chini ya Dakika tisa.
Wanasayansi hawakutegemea tathmini ya watu waliojitolea kuhusu usingizi wao (ambayo si sahihi kila wakati), lakini ilithibitishwa walipokuwa wameamka na kulala kupitia aina ya utafiti wa usingizi unaojulikana kama polysomnografia. Hii inahusisha kuambatisha vitambuzi kwenye kichwa cha mtu na sehemu nyingine za mwili ili kufuatilia mawimbi ya ubongo, kupumua na mienendo yao.
Kushughulikiwa kwa wakati unaofaa. Kama bonasi sio lazima kuwa na wasiwasi juu ya kuzisahau.
Ni kweli kusema utafiti wa Scullin’s sio mpana ,lakini kuna utaratibu wa kisaikolojia ambao unaweza kueleza kwa nini alipata matokeo aliyoyafanya. Inaitwa "cognitive offloading" na hutokea wakati mtu anachukua hatua ya kimatendo ili kupunguza mzigo wa akili.
Ukigeuza ramani ili kuifanya ilingane na mpangilio wa barabara ilio mbele yako, huo ni mfano wa upakiaji wa utambuzi. Unaondoa baadhi ya kazi ya kiakili unayohitaji kufanya ili kujielekeza, na hivyo kupunguza mkazo kwenye ubongo wako na kufanya kazi ya kwenda katika mwelekeo sahihi iwe nafuu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa upande wa orodha iliyoandikwa ya mambo ya kufanya kesho yake kabla ya kulala, unapakua majukumu yako kutoka akilini mwako hadi kwenye kipande cha karatasi (au simu ukipenda na ikiwa una uhakika hutavutiwa kwenye mitandao ya kijamii au yako. barua pepe) kwa njia ambayo inapunguza hitaji la wewe kuzifikiria unapojaribu kulala.
Na badala ya kuwa na kazi zinazozunguka kichwani mwako bila mpangilio, zinawekwa katika mpangilio wa aina fulani.Zimehifadhiwa , kana kwamba ziko tayari kushughulikiwa kwa wakati unaofaa. Ufanisi unaokuwa nao ni hutakuwa na muda wa kufikiria sana iwapo utasahau.
Ni vyema kuorodhesha majukumu mahususi , badala ya kuandika kwa ujumla, ingawa itafanya orodha yako kuwa ndefu zaidi.
Utafiti wa Profesa Scullin uligundua kuwa watu wenye shughuli nyingi ambao waliunda orodha ya kazi zaidi ya 10 walilala kwa wastani wa dakika 15 haraka kuliko watu ambao hawakuandika orodha za kazi. Pia walilala kwa dakika sita haraka kuliko wale ambao walikusanya orodha fupi tu. Kwa hivyo, fanya kuwa pana.
Kufanya haya yote kunaweza kuonekana kama kazi ngumu wakati umechoka na unajipanga kulala. Lakini inaweza kuwa na thamani yake.
Kuandika orodha yako ya mambo ya kufanya kabla tu ya kuingia hakutafanya maisha yako kuwa na shughuli nyingi, lakini kunaweza kukusaidia tu kupata usingizi na kuwa na wasiwasi kidogo. Na ukiamka siku inayofuata ,tayari umejipanga kwa sababu unayo orodha ya kila kitu unachohitaji kufanyam siku hiyo.
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid












