Kwa nini wanandoa wengi huchagua kulala vitanda tofauti?

FDC

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Cecilia na mpenzi wake waliamua kulala vitanda tofauti
    • Author, Fernanda Paul
    • Nafasi, BBC

Yote yalianza baada ya kusambaa kwa virusi vya Corona. Mkoromo ukawa hauvumiliki na Cecilia 35 hakupata usingizi. Alikuwa akimsukuma mwenzake, akijaribu kumfanya ageuke ili aache kukoroma, lakini jitihada hizo zilishindikana.

Hakuweza kuvumilia tena, kwa hiyo yeye na mpenzi wake wa umri wa miaka 43 walipitisha uamuzi; hawatalala katika chumba kimoja. Anaishi London, ambako ameishi kwa miaka miwili.

Pia unaweza kusoma

Talaka ya Usinginzi

FDVC

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Kulingana na utafiti uliofanywa Marekani, zaidi ya theluthi moja ya washiriki waliripoti kwamba wakati mwingine au mara kwa mara hulala katika vyumba tofauti.

Stephanie Collier, daktari wa magonjwa ya akili katika Hospitali ya McLean nchini Marekani, anasema, ''wanandoa wanahisi wanalala vizuri zaidi wanapokuwa peke yao, na kwa kawaida sababu hizo huhusiana na afya, kukoroma, au kupigana miguu au kuweweseka.''

Anasema "talaka za usingizi" zimekuwa maarufu sana.

Mwishoni mwa mwaka jana, mwigizaji maarufu wa Marekani Cameron Diaz alisema katika kipindi cha mtandaoni, yeye na mumewe hawalali katika chumba kimoja.

Kauli hiyo ilizua maelfu ya majibu kwenye mitandao ya kijamii, na makala mbalimbali ziliandikwa kuhusu hilo kwenye vyombo vya habari. Lakini nyota huyo wa Hollywood si pekee anayefanya hivyo.

Kwa mujibu wa utafiti wa 2023 uliofanywa na American Academy of Sleep Medicine (AASM), zaidi ya theluthi moja ya washiriki nchini Marekani waliripoti, wakati mwingine au mara kwa mara hulala katika vyumba tofauti ili kuboresha usingizi.

Utafiti unaonyesha tabia hii imeenea miongoni mwa kizazi cha sasa. Kizazi cha umri kati ya miaka 28 na 42. Karibu nusu (43%) walijibu wanalala vitanda tofauti na wenzi wao.

Kizazi cha waliozaliwa kati ya 1997 na 2012 - 28% walisema hulala vitanda tofauti. Waliozaliwa kati ya 1946 na 1964 ni 22%.

Kuna faida?

FV

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Wanahistoria wanasema ilikuwa kawaida katika siku za nyuma kwa wanandoa kulala katika vyumba tofauti
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wanahistoria wanasema "kitanda cha ndoa" (au kitanda cha watu wawili) ni dhana ya kisasa na matumizi yake yameongezeka kutokana na Mapinduzi ya Viwanda.

Kabla ya karne ya 19, ilikuwa kawaida kwa wanandoa kulala tofauti. Wataalamu wanakubali kuna faida nyingi kwa wanandoa ambao wanaamua kulala katika vyumba tofauti.

"Faida ni kupata usingizi mzuri ambao ni muhimu kwa afya," anasema Stephanie Collier, daktari wa magonjwa ya akili katika Hospitali ya McLean nchini Marekani.

"Ikiwa mtu hawezi kulala, kinga yake ya mwili hadi kazi zake huathirika, pamoja na milipuko ya hasira na matukio ya huzuni."

Daktari wa magonjwa ya akili anaamini "talaka ya usingizi" inaweza pia kusaidia kudumisha uhusiano "wenye afya."

"Wanandoa wasipopata mapumziko ya kutosha, hugombana zaidi, hukasirika zaidi na kupoteza huruma miongoni mwao. Kunaweza kuwa na chuki kwa mtu anayesababisha usumbufu wa kulala jambo ambalo linaweza kuathiri uhusiano wao," anasema Collier.

Kwa Cecilia, kulala katika chumba tofauti na mpenzi wake wa sasa “kumebadilisha maisha yake.”

"Ni vizuri zaidi, sasa ninaweza kulala vizuri, nikiwa na nafasi zaidi kitandani, na kuweza kujigeuza bila kuwasumbua wengine."

“Pia, hutakiwi kuamka wakati mmoja na mwenzako, bali amka unapotaka au unapohitaji,” anaongeza.

Kuna hasara gani?

FV

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Watu wengine hupata usingizi mzuri zaidi wanapolala peke yao

Lakini utaratibu huu huhitaji chumba cha ziada na kitanda cha ziada, hivyo kwa wanandoa wengi hili sio chaguo linalowezekana.

Lakini hata kama hilo litawezekana, uamuzi huu unaweza pia kuwa na athari, kwani wataalam wanasema wanandoa wengi wana wasiwasi juu ya kupoteza hamu na mwenza wake.

Cecilia anasema: “Nafikiri katika ngazi ya mawasiliano na mwenzi wangu kuna jambo limebadilika. Kuna changamoto katika uhusiano wetu wa karibu, lakini si jambo baya sana, na nadhani faida ni kubwa zaidi.”

Dkt. Collier anaeleza kwamba kwa watu wengi wanaofanya kazi masaa mengi, muda wa kuwasiliana na wapenzi wao ni wakati wa kulala.

Dkt. Brockman anasema "talaka ya usingizi" sio kitu kinachofaa kwa wanandoa wote. "Kuna faida fulani za kibayolojia za kulala kama wanandoa.''

"Kuna tafiti zinazoonyesha kuna wanandoa ambao wamekuwa wakilala pamoja kwa miaka mingi na wanaweza kuongeza ubora wa usingizi wao."

Mambo muhimu ya Kuzingatia

EFV

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Uchunguzi unaonyesha tabia hii inakuwa katika baadhi ya nchi.

Hata hivyo, ikiwa wanandoa wanaamua kujaribu "talaka ya usingizi," kuna baadhi ya mapendekezo ya kufuata, wataalamu wanasema.

“Ni lazima kuwe na makubaliano ya wote wawili,” anasema Dkt. Collier.

"Baadhi ya watu hawataki kulala peke yao na hiyo inawafanya wajisikie kuchanganyikiwa, hivyo wanandoa wanapaswa kukubaliana, na uwe uamuzi wa pamoja kati yao."

Uchunguzi unaonyesha utamaduni huu unakua, katika baadhi ya nchi.

Nchini Uingereza, Shirikisho la Kitaifa la Familia liligundua kuwa mwaka 2020, 15% ya wanandoa wa Uingereza wanaoishi pamoja sasa wanalala tofauti.

Utafiti wa Sleep Council wa mwaka 2009 ulibaini kuwa 7% ya wana ndoa hulala vitanda tofauti.

"Hii inaonyesha kwamba kiwango cha kulala vyumba tofauti kimeongezeka karibu mara mbili katika muongo uliopita," Shirikisho la Kitaifa la Familia linasema.