Faida za wanandoa kulala vitanda viwili tofauti

fdc

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Ni kawaida kwa wanandoa kulala vitanda tofauti nyakati fulani, mmoja wenu anaposafiri au kuugua.

Utafiti uliochapishwa katika mtandao wa relationshipsnsw.org.au -unaonyesha ikiwa wanandoa wanalala vitanda viwili tofauti au vyumba viwili - kuna faida za kiakili na kimwili.

Kuna faida nne za wanandoa kulala katika vitanda tofauti.

Pia unaweza kusoma

Usingizi mzuri

dscx

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Wanandoa kulala vitanda tofauti kunaweza kuboresha usingizi wao. Kulala kitanda kimoja kunaweza kuleta changamoto na usumbufu, ikiwa mpenzi wako anakoroma sana - lakini kulala peke yako unapata usingizi mzuri na kupumzika vizuri zaidi.

Na hii ni habari njema, kwa sababu usingizi usiokatishw katishwa ni muhimu kwa afya jumla ya mtu.

Ukosefu wa usingizi huongeza hatari ya kupata matatizo ya kiafya, ikiwa ni pamoja na unene, ugonjwa wa kisukari na ugonjwa wa moyo, kulingana na Harvard Medical School.

Mabishano ya Wanandoa

dsx

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Wanandoa kulala katika vitanda viwili tofauti au vyumba viwili tofauti kunaweza kupunguza mabishano.

Wanandoa wengi hukutana baada ya siku ndefu ya kazi na kuchoka. Lakini ikiwa umekuwa na siku mbaya au umechoka na huko tayari kuzungumza na mpenzi wako, kulala kitanda au chumba tofauti kutaepusha mabishano.

Nafasi zaidi

dc

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Baadhi ya watu hupenda kulala peke yao na kujitandaza kitandani lakini wanapokuwa na wenzi wao hujihisi kubanwa na kukosa raha, hivyo huhitaji kuwa na nafasi ya kutosha kitandani.

Kwa maneno mengine, wanataka nafasi ambayo itawawezesha kujifurahisha na kujitanafasi.

Pia unaweza kusoma

Usumbufu wa Asubuhi

wdc x

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Wanandoa wengi huwa na ratiba tofauti za kazi. Huamka asubuhi mapema na kumsumbua mwenza wake ambaye bado amelala.

Kwa hiyo ikiwa wana ndoa wanalala katika vyumba viwili tofauti, wataepuka usumbufu wa namna hii.

Zingatia haya kabla ya kufanya maamuzi

Wanandoa wanapaswa kuzingatia mambo haya kabla ya kuamua kulala vitanda au vyumba viwili tofauti:

Ikiwa usingizi wako unaathiriwa na kulala kitanda kimoja na mpenzi wako. Ikiwa mnagombana mara kwa mara ama ikiwa mmoja anakoroma sana.

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdalla na kuhaririwa na Dinah Gahamanyi