Moja kwa moja, Marekani yaondoa ndege zake za kivita kutoka kambi ya Fairford Uingereza

Kwa mujibu wa Wall Street Journal, uamuzi wa kuondoa ndege hizo unahusishwa na hofu ya kiusalama katika Kambi ya Anga ya Fairford.

Ruka Video uendelee
  • Wicknell Chivayo
  • Kijanangoma
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx

Moja kwa moja

Na Lizzy Masinga

  1. Watu wote waliokuwa kwenye ndege iliyotoweka pwani ya Marekani wahofiwa kufa

    Raia wanne wa Canada na raia wawili wa Bermuda walikuwa ndani ya ndege hiyo, ambayo ilitoweka mapema saa za alfajiri ya Jumamosi.
    Maelezo ya picha, Raia wanne wa Canada na raia wawili wa Bermuda walikuwa ndani ya ndege hiyo, ambayo ilitoweka mapema saa za alfajiri ya Jumamosi.

    Watu sita waliokuwa ndani ya ndege ya usafiri wa kimatibabu iliyotoweka siku ya Jumamosi wakati ikisafiri kutoka Bermuda kwenda Boston wanahofiwa kufariki dunia, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msimamizi wa safari hiyo.

    Jioni ya Jumapili, Walinzi wa Pwani wa Marekani walitangaza kuwa wanasitisha operesheni ya kutafuta manusura katika eneo la bahari karibu na Nantucket, kisiwa kilichoko jimbo la Massachusetts.

    “Lazima sasa tukubali ukweli wa kusikitisha kwamba maafisa wanne wa timu yetu ya Latitude, mgonjwa wetu pamoja na mwanafamilia aliyekuwa akisafiri kumhudumia, waliokuwa ndani ya ndege ya Heartbeat 104, wanahofiwa kufariki dunia,” Latitude Air Ambulance ilisema katika taarifa iliyotolewa muda mfupi baadaye.

    “Fikra na maombi yetu yako kwanza kabisa kwa familia zao, wapendwa wao, marafiki na wafanyakazi wenzao.”

    Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA) ilipoteza mawasiliano na ndege aina ya Gulfstream G-100 muda mfupi baada ya saa 1:00 asubuhi kwa saa za eneo hilo (05:00 GMT) siku ya Jumamosi.

    Jumamosi jioni, mamlaka zilipata eneo lenye mabaki ya ndege ambalo lilithibitishwa kuwa ni sehemu za ndege hiyo iliyopotea.

    Kwa mujibu wa taarifa za safari za ndege kutoka FlightAware, ndege hiyo iliondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa L.F. Wade mjini Bermuda saa 23:40 usiku wa Ijumaa, na ilitarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Logan mjini Boston saa 01:30 asubuhi kwa saa za Mashariki mwa Marekani (05:30 GMT).

    Raia wanne wa Canada na raia wawili wa Bermuda walikuwa ndani ya ndege hiyo.

    “Huu ni msiba usioelezeka kwa familia yetu ya Latitude na kwa kila mtu aliyewapenda watu sita waliokuwa ndani ya ndege ya Heartbeat 104,” alisema Peter Byl, Rais wa Latitude Air Ambulance, Jumapili jioni.

    “Lengo letu kwa sasa ni kuzisaidia familia zao, kuwasaidia wafanyakazi wetu na kushirikiana na mamlaka husika katika uchunguzi. Tutawaheshimu wenzetu kwa kukumbuka huduma, weledi na kujitolea waliokuwa wakionesha katika kazi yao kila siku.”

    Latitude Air Ambulance ni kampuni ya Canada inayotoa huduma za usafiri wa wagonjwa kwa ndege za kitabibu kimataifa, ikiwasaidia wagonjwa kurejea katika nchi au makazi yao kwa ajili ya matibabu na uangalizi zaidi.

    Unaweza kusoma:

  2. Real Madrid yaingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili Scott

    Scott

    Real Madrid inafikiria kujiunga katika mbio za kumsajili kiungo wa Bournemouth na England, Alex Scott,23, baada ya kumfuatilia kwa wiki za karibuni.

    Chelsea inaonekana kuwa mbele katika mbio za kumchukua Scott kutoka Bournemouth, huku Liverpool na Arsenal nazo zikionesha nia ya kumsajili.

    Arsenal inatafuta kumsajili winga wa Uturuki Kenan Yildiz (miaka 21) kutoka Juventus, lakini inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Bayern Munich na Real Madrid.

    Real Betis imesisitiza kuwa haitakubali ofa yoyote kwa mshambuliaji Troy Parrott, ambaye ana kipengele cha kuvunja mkataba chenye thamani ya pauni milioni 85. Kauli hiyo imekuja kufuatia uvumi wa kurejea kwa mshambuliaji huyo wa Jamhuri ya Ireland mwenye miaka 24 katika klabu ya Tottenham Hotspur.

    Wakati huo huo, klabu kadhaa za Premier League zinafuatilia hali ya kiungo mkabaji wa Sevilla, Lucien Agoume,24, huku kipengele chake cha kuvunja mkataba kikitajwa kuwa karibu pauni milioni 35.

    Liverpool na Chelsea zimeingia katika mbio za kumsajili beki wa Nottingham Forest, Murillo, lakini klabu hiyo haitaki kumuuza katika dirisha la usajili la Januari.

    Mshambuliaji wa Monaco, Folarin Balogun, bado ana nia ya kucheza katika Premier League, licha ya mpango wake wa kujiunga na Everton kuvunjika siku ya mwisho ya usajili.

    Nyota huyo wa timu ya taifa ya Marekani anaendelea kuvutia klabu za England.

    Klabu za Barcelona na Inter Milan ni miongoni mwa vigogo wa Ulaya wanaomfuatilia beki wa Bosnia mwenye miaka 23, Tarik Muharemovic. Hata hivyo, Leeds United haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka Sassuolo kwa takribani pauni milioni 34.

    AC Milan inaweza kujaribu kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Brazil wa Real Madrid, Endrick (miaka 20), mwezi Januari. Hata hivyo, makubaliano hayo hayatahusisha kipengele cha kumnunua moja kwa moja baada ya kipindi cha mkopo.

    Kocha wa zamani wa Chelsea na Tottenham Hotspur, Antonio Conte, anaripotiwa kufurahia mapumziko yake nje ya soka kwa sasa, licha ya kuhusishwa na kurejea kufundisha katika klabu za Manchester United na Juventus.

    Unaweza kusoma:

  3. Iran yaanzisha kambi ya kuwafunza wanawake matumizi ya silaha

    Wanawake wa Iran

    Kambi maalum ya kuwafundisha wanawake matumizi ya silaha na utoaji wa huduma ya kwanza imeanzishwa mjini Tehran, huku viongozi wa Iran wakiendelea kuhimiza wananchi kuwa tayari "kuyatoa maisha yao kwa ajili ya kuilinda nchi."

    Siku ya Jumapili, Uwanja wa Imam Hussein katika mji mkuu wa Tehran ulikuwa mwenyeji wa kambi hiyo ya kwanza ya aina yake inayowalenga wanawake.

    Makumi ya wanawake walishiriki mafunzo hayo wakiwa wamevalia chador, vazi la kitamaduni linalofunika mwili mzima isipokuwa uso.

    Hatua hiyo inakuja wakati mvutano ukiongezeka katika eneo la Mashariki ya Kati, huku bei za mafuta zikiendelea kupanda katika masoko ya kimataifa.

    Iran imeapa kuendelea kuufunga Mlango wa Bahari wa Hormuz hadi Marekani itakapotekeleza masharti yake.

    Maafisa wa Iran wanasema mafunzo hayo yanalenga kuwaandaa wananchi kukabiliana na hali za dharura na kuimarisha uwezo wa jamii kujilinda endapo kutatokea tishio kwa usalama wa taifa.

    Hata hivyo, hatua hiyo imechukuliwa na wengi kama ishara ya maandalizi ya kukabiliana na mazingira ya mvutano unaoendelea katika kanda hiyo.

    Wanawake wa Iran
  4. Pande zinazoshiriki Mkataba wa Mecca kukutana mjini Riyadh, Yemen, Houthi zatekeleza operesheni za kijeshi

    Mashambulizi

    Mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh, utakuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi wanachama wa “Mkataba wa Mecca wa Ulinzi wa Pamoja” siku ya Jumatatu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imetangaza.

    Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo, mkutano huo utahudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, Waziri wa Ulinzi Yaşar Güler, na Mkuu wa Majeshi Selçuk Bayraktaroğlu, pamoja na wawakilishi wa Saudi Arabia na Pakistan, ambazo pia ni nchi zilizotia saini mkataba huo.

    Taarifa hiyo ilisema kuwa mkutano utajadili maendeleo ya hivi karibuni katika eneo hilo na hatua iliyofikiwa katika juhudi za kuimarisha muungano huo na kuupa mfumo rasmi wa kiutendaji.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan alisema Ijumaa kuwa Iran imeonesha utayari wa kushiriki katika juhudi za upatanishi wa kisiasa na waasi wa Houthi, suala ambalo linatarajiwa kujadiliwa wakati wa mkutano huo.

    Mkutano huo unafanyika wakati serikali ya Yemen, inayoungwa mkono na Saudi Arabia, imetangaza kuanza kwa operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya kundi la Ansar Allah (Houthi) linaloungwa mkono na Iran, kwa lengo la kurejesha ushawishi na udhibiti katika maeneo yaliyo chini ya kundi hilo.

    Unaweza kusoma:

  5. Mwanajeshi wa Marekani akamatwa kwa tuhuma za mauji nchini Japan

    .

    Mwanajeshi wa Jeshi la Majini la Marekani (US Marine) amekamatwa kwa tuhuma za kumuua mwanamke mmoja baada ya mwili wake kupatikana katika hoteli kwenye kisiwa cha Okinawa, kusini mwa Japan, kwa mujibu wa mamlaka za eneo hilo.

    Waziri wa Japan, Sanae Takaichi, alilaani tukio hilo, akilielezea kuwa ni tukio la uporaji na mauaji ya "kikatili na ya kutisha". Alisema ameitaka Marekani kuimarisha usimamizi na nidhamu miongoni mwa wanajeshi wake waliopo nchini Japan.

    Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la NHK, marehemu ametambuliwa kuwa Yagi Anna, mwenye umri wa miaka 39, huku mtuhumiwa akitajwa kuwa Devin Jacob Ballard, mwenye umri wa miaka 20. Ballard anahudumu katika Kituo cha Anga cha Jeshi la Majini la Marekani cha Futenma, kilichoko Okinawa.

    Kamandi ya Jeshi la Majini la Marekani ilisema inashirikiana kikamilifu na mamlaka za Japan katika uchunguzi wa tukio hilo, huku pia ikitoa salamu za pole kwa familia ya marehemu.

    Waziri wa Ulinzi wa Japan, Shinjiro Koizumi, alisema mwili wa mwanamke huyo ulipatikana mapema Jumamosi katika hoteli moja jijini Naha, mji mkuu wa Mkoa wa Okinawa.

    "Tukio kama hili halikubaliki kabisa na linanikasirisha sana," Koizumi aliandika kwenye mitandao ya kijamii. "Matukio na ajali zinazohusisha vikosi vya Marekani husababisha wasiwasi mkubwa miongoni mwa wakazi wa eneo hili na hayapaswi kujirudia."

    Ubalozi wa Marekani mjini Tokyo ulisema unaendelea kushirikiana kwa karibu na serikali ya Japan pamoja na polisi wa eneo hilo katika uchunguzi wa kesi hiyo.

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan ilisema ilimwita Balozi wa Marekani nchini humo, George Glass, kwa mazungumzo kuhusu tukio hilo siku ya Jumapili.

    Okinawa ni makazi ya idadi kubwa ya vituo vya kijeshi vya Marekani na maelfu ya wanajeshi wa Marekani, huku matukio yanayohusisha wanajeshi hao mara kwa mara yakizua mjadala na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo.

  6. Marekani yaondoa ndege zake za kivita kutoka kambi ya Fairford Uingereza

    .

    Marekani imeondoa ndege zake zote za kivita kutoka Kambi ya Anga ya RAF Fairford nchini Uingereza, kituo cha kijeshi kilichokuwa katikati ya uchunguzi wa polisi wa kukabiliana na ugaidi.

    Afisa mmoja wa Marekani alithibitisha Jumapili kuwa ndege zote za kivita zilizokuwa zimepelekwa katika kambi hiyo zimerejeshwa katika vituo vyake vya kudumu nchini Marekani.

    Marekani haikutoa sababu rasmi ya hatua hiyo. Hata hivyo, uamuzi huo umefuatia tukio la kiusalama lililotokea Septemba 27, wakati polisi walipopokea taarifa kuhusu magari matatu yaliyokuwa yakitiliwa shaka karibu na kambi hiyo ya anga iliyoko Gloucestershire.

    Taarifa hiyo iliripotiwa awali na gazeti la Wall Street Journal kabla ya Pentagon kutoa uthibitisho rasmi saa chache baadaye.

    "Kutokana na sababu za kiusalama, haikuwezekana kuthibitisha uhamishaji wa vifaa na wanajeshi. Hata hivyo, sasa tunaweza kuthibitisha kuwa ndege zote za Marekani zilizokuwa zimepelekwa RAF Fairford zimerejea katika vituo vyake vya kudumu nchini Marekani," Pentagon ilisema.

    Katika taarifa yake, wizara hiyo ilisisitiza kuwa Jeshi la Anga la Marekani linaendelea kuwa tayari kutekeleza operesheni za mashambulizi ya usahihi wa hali ya juu popote duniani.

    "Kikosi kinachosimamia ndege za B-1, B-2 na B-52 kina uwezo wa kutekeleza operesheni za masafa marefu kutoka Marekani na kurejea nchini. Uwezo huu upo tayari kutumika wakati wowote na mahali popote," ilisema taarifa hiyo.

    Kwa mujibu wa Wall Street Journal, uamuzi wa kuondoa ndege hizo unahusishwa na wasiwasi wa kiusalama katika Kambi ya Anga ya Fairford. Wiki iliyopita, watu kadhaa walikamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika kile kilichoelezwa kuwa njama inayoweza kuhusishwa na ugaidi karibu na kambi hiyo.

    Hata hivyo, washukiwa hao baadaye waliachiliwa kwa dhamana. Polisi wa Uingereza walisema hawakupata vilipuzi wakati wa upekuzi wa magari matatu ya aina ya van, bali walikuta kiasi kidogo cha petroli pekee.

    Baada ya tukio hilo, Israel, Marekani na Uingereza ziliituhumu Iran kuhusika na mpango huo. Tehran ilikanusha vikali madai hayo, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi, akisema kuachiwa kwa washukiwa hao kunatoa picha ya udhaifu wa tuhuma zilizokuwa zikitolewa dhidi yao.

    Mvutano huo unakuja miezi kadhaa baada ya Iran kuikosoa Uingereza kwa kuruhusu Marekani kutumia Kambi ya Anga ya RAF Fairford kufanya mashambulizi dhidi ya maeneo ya Iran. Wakati huo, Tehran ilisema inahifadhi haki ya kulenga vituo vya kijeshi vinavyotumiwa na Marekani.

    Soma Pia:

  7. Karibu kwa matangazo ya moja kwa moja.