Je, unaujua mtindo mpya wa maisha wa kufanya kazi kidogo na kupumzika sana?

fd

Chanzo cha picha, Alamy

    • Author, Holly Williams
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Wazo la kutofanya chochote kwa mwaka mzima limekaaje? Yaani hakuna kufanya kazi, hakuna kutuma au kupokea barua pepe, hakuna kujiendeleza kitaaluma, hakuna kujitahidi au kujituma au kusaka mafanikio.

Kwa wengi wetu, wazo hilo ni la ajabu. Kwani tunajua kazi hukupa hadhi, kupata pesa ni mafanikio, na kuwa na shughuli nyingi ni jambo la kujivunia!

#SlowLiving – hashtagi hiyo imetumika zaidi ya mara milioni sita kwenye Instagram. Na wapo wanaotaka kufanya kazi nyepesi kwa muda mfupi, na kutumia sehemu kubwa ya muda wao kwa vitu vya kufurahisha, uhusiano, au kujitunza.

Na watu katika vizazi vyote wameungana kutaka wafanye kazi kidogo. Nchini Uingereza kwa mfano, dhana ya wiki iwe siku nne inapata nguvu kubwa kila uchao.

Pia unaweza kusoma

Wapinzani wa kazi bila mapumziko

sd

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na vitabu vingi vinavyochunguza maisha ya kupumzika zaidi kuliko ya kufanya kazi

Mjasiriamali na mwandishi Emma Gannon, katika kitabu chake cha: The Success Myth: Letting Go of Having It All, ambacho kinazungumzia jinsi kupambana bila kuchoka kusaka mafanikio kusivyoleta furaha ya kweli. Kulikuwa kunampa uchovu ambao, ulimlazimisha kukabili umuhimu wa kupumzika.

"Nikiangalia nyuma, kulikuwa na matatizo mengi - nikihisi kuchanganyikiwa, maumivu ya kichwa, kutoweza kuzingatia," anasema.

Ghafla, 2022, mwili wake uliingia katika hali ya kulazimishwa kupumzika. "Sikuweza kutazama simu, sikuweza kutazama skrini, sikuweza kutembea barabarani bila kuhisi uchovu."

Kitabu cha How to Do Nothing: Resisting the Attention Economy, kilichoandikwa na Jenny Odell mwaka 2019. Pia ni sehemu ya wimbi la waandishi wanaohimiza upinzani mkali wa kufukuzia mafanikio bila mapumziko, katika ulimwengu ambapo thamani yetu inaamuliwa na uzalishaji wetu.

Katika kitabu cha Oliver Burkeman cha 2021 cha Four Thousand Weeks - ambacho kinatukumbusha kuwa maisha ni mafupi, na hatuwezi kufanya kila kitu kwenye orodha yetu ya mambo ya kufanya.

Badala ya kutafuta kuwa na ufanisi zaidi, anasema tunapaswa kuzingatia kile ambacho ni muhimu, tuachane na kusaka ukamilifu na ukamili, na tuuwishi vizuri wakati tulionao.

Waandishi wa vitabu hivi na vingine, wanatetea muda wa kupumzika kwa manufaa ya afya yetu ya akili, ustawi wetu wa kiroho, kuleta usawa wa maisha ya kazi, na hata kwa ajili ya kujifurahisha tu.

'Kila mtu amechoka sana'

f

Chanzo cha picha, Paul Storrie

Maelezo ya picha, Emma Gannon ni mwandishi wa 'A Year of Nothing'
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa hivyo ni kwa nini kumekuwa na mabadiliko haya katika ulimwengu wa Magharibi? "Kila mtu amechoka sana. Sote tunajitahidi kwa namna fulani kupumzika. Tuna mwili na akili ambazo zinahitaji kuangaliwa, na sidhani kama tunafanya [hilo], kwa kweli," anasema Gannon.

Janga la uviko 19 lilibadili mambo, kazi zilisitishwa, au zilifanywa nyumbani kwa mara ya kwanza. Safari zilitoweka. Wengi hawakuwa na chaguo ila kupunguza safari. Na watu wengi hawakutaka tena kurudi nyuma na maisha hayo ya mapumziko.

Inaweza pia kuwa ni mabadiliko ya kizazi. Maisha ya kukuwa ili ufanye kazi kwa bidii ili kufanikiwa, na kisha uhitimu na mlima wa deni katika ulimwengu usio na utulivu wa kifedha, imekuwa ni changamoto kubwa kwa wengi.

Vitabu vya kupunguza kufanya kazi vinauza sana katika miaka ya hivi karibuni. Kitabu cha Anne Helen Petersen, Can't Even: How Millennials Became the Burnout Generation - ambacho kilichunguza jinsi ubepari na kusaka faida ulivyoingiza kizazi hiki kwenye uchovu.

xc

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Kitabu cha Oliver Burkeman cha Four Thousand Weeks kinasema maisha ni mafupi, na tunapaswa kuzingatia kile ambacho ni muhimu zaidi

Gannon anaeleza jinsi alivyoweza kuacha kufanya kazi, lakini anadokeza kwamba ni mabadiliko ya akili. Na anasisitiza, inafaa kukumbuka msemo hu wa zamani kwamba; vitu bora zaidi maishani ni vya bure.

Anakumbuka siku ambayo alikuwa akihangaika na uchovu, na alichoweza kufanya ni kutembea. Kitendo rahisi cha kunyoosha miguu yake, na kisha kuweka maua ya manjano ya kupendeza kwenye bakuli, kilitosha kumfanya ajisikie vizuri siku nzima.

Kwa kweli sio kuhusu unapoenda au kile unachokiona - ni kufanya kitu ambacho kitainua roho yako. Sote tunajua hiyo haigharimu pesa.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na Kuhaririwa na Yusuf Jumah