Je, mwangaza huathiri usingizi au ni dhana tu?
Wajua kwamba wazo kuwa taa wakati wa usiku huzuia usingizi ni uongo? Wanasayansi ambao wamekuwa wakichunguza mwangaza bora zaidi kuleta usingizi wamesema. Kulingana na watafiti kutoka chuo kikuu cha Manchester, mwangaza wa rangi ya samwati sio shida. Matokeo hayo tata yanaonyesha kuwa mwangaza utaadhiri usingizi kulingana na joto au baridi kutoka kwa mwangaza huo. Je wewe hulala ikiwa taa zimewaka?
