Utapiamlo na uzito kupita kiasi unavyoathiri nchi maskini

Maelezo ya sauti, Utafiti wabaini kuwa utapiamlo na Uzito kupita kiasi unaathiri nchi za kipato cha chini

Utafiti uliochapishwa katika jarida la matibabu la Lancet unaonya kwamba idadi kubwa ya nchi zenye kipato cha chini zinakabiliwa na ukosefu wa lishe bora vile vile shida ya uzito kupita kiasi. Watafiti wanasema shida hii ya utapiamlo' inaweza kuwa na athari kwa vizazi vijavyo. Je, jamii inaweza kulindwa vipi kutokana na shida hii? wasiliana nasi kwenye ukurasa wa Fcebook BBCSwahili.