“Nimeingia kwenye madeni nikisaka muujiza''

G

Evarline Okello analia anaponieleza kuwa ana deni la mamia yad ola, paada ya kumlipa mchungaji amuombee.

Anaishi katika nyumba ndogo ya mabanda iliyopo Kibera , mtaa mkubwa wa mabanda uliopo jijini Nairobi nchini Kenya, na hawezi tena kukidhi mahitaji ya watoto wake wanne.

Bi Okello hajapata riziki yoyote kwa miezi kadhaa, ananiambia tulipozungumza kwa njia ya simu. Kwahiyi aliposikia kuhusu mchungaji ambaye maombi yake yanaweza kuyafanya maisha yake kuwa bora, alitaka kumuona.

Alimtaka ampe $115 (£96; sawa na shilingi 15,000 za Kenya).

Hii inafahamika kama ‘’mbegu ya sadaka’’: mchango wa sadaka kwa kiongozi wa dini, kwa lengo la kupata matokeo fulani kutokana nayo.

Bi Okello alikopa pesa kutoka kwa rafiki yake, amnaye alichukua mkopo kwa niaba yake. Alikuwa ameambiwa kuwa maombi ya mchungaji huyu yalikuwa na nguvu sana kiasi kwamba angeweza kumrudishia pesa yake katika kipindi cha wiki moja.

Lakini muujiza haukuwahi kuonekana. Badala yake mambo yalikuwa mabaya zaidi, anasema. Mkopo niliokopa kwa rafiki yangu umeongezeka kutokana na riba ambazo hazikulipwa. Sasa anadaiwa zaidi yad ola 300, na haelewi ni vipi ataweza kulipa deni hilo. Rafiki yake ameacha kuongea naye, na hana bado kazi.

"Mambo yamekuwa magumu sana nimepoteza matumaini yote," anasema.

'Suluhu za miujiza'

Kenya imekumbwa na mzozo mkubwa wa ongezeko la garama ya maisha. Bei za vyakula zimepanda kwa takriban 16% katika kipindi cha miezi 12 kabla ya septemba 22, kulingana na Taasisi ya taifa la Kenya ya takwimu, huku takwimu za dunia zikionyesha kuwa idadi kubwa ya Wakenya ambao hawana ajira imeongezeka mara dufu katika kipindi cha miaka saba iliyopita.

"Watu wanaishi maisha magumu sana," anasema Dkt Gladys Nyachieo, mwanasosholojia katika Chuo kikuu cha habari nchini Kenya - Multimedia University of Kenya.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kenya imeshuhudia maamdamano kuhsuu ongezeko la garama ya maisha
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hii imeongeza ari ya watu kutafuta suluhu za miujiza, anasema, na wengi sasa wako tayari kulipa pesa zao kwa ajili ya muujiza, hata kama watakopa pesa.

"watu wanambiwa kuwa Mungu hataki waendelee kuwa masikini. Kwahiyo wanapanda mbegu ," ananiambia.

Wanafaya kile kinachoitwa Injiri ya mafanikio, ambayo inafundisha kwamba Mungu huwazawadia utahiri na afya. Waumini wanaambiwa waonyeshe Imani yao kwa kutoa pesa, ambayo inadaiwa kuwa italipwa na Mungu mara nyingi.

Injili ya mafanikio ina mizizi yake nchini marekani, ambako ilishika kasi mwanzoni mwa karne ya 20. Kufikia miaka ya mwisho ya 1970 na 1980 wachungaji wa Nigeia walikuwa wakienda marekani kujifunza zaidi kuhusu injiri hiyo, na katika miaka ya mwanzo ya 2000 umaarufu wa injiri hii ulikuwa umesambaa kote Afrika, ikiongozwa kwa sehemu moja na wainjiristi kama vile Reinhard Bonnke, ambaye alikusanya umati mkubwa kuanzia Lagos hadi Nairobi. Umaarifu huo umeendelea kuongezeka hadi leo.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muinjilist Mmarekani Reinhard Bonnke, aliyefariki mwaka 2019, alikuwa maarufu sana nchini Nigeria

Dkt Nyachieo pia anabainisha sababu nyengine inayowarubuni watu kuingia katika madeni – nayo ni ofa mbalimbali za mikopo zinazojitokeza katika simu za Wakenya. “Watu huomba tu na kupata mikopo hiyo,” anaeleza.

Na hicho ndicho kilichokuta Dennis Opil, 26. Baada ya kukatishwa tamaa na hali ya kusaka ajira kwa miaka mitatu bila mafanikio, alimuomba ushauri na usaidizi rafiki yake.

"Alinishauri kuwa kuna kanisa ambalo ukienda wanakufanyia maombi. Unatoa kiasi Fulani cha sadaka kisha unafanyiwa maombi, baada ya hapo unaweza kupata ajira,” anaeleza Bw Opil.

Aliambiwa atoe mchango kila Jumapili kwa muda wa miezi mitatu, na kwa ujumla akatoa takribani dola 180. Baada ya kumaliza akiba yake yote, akakopa dola 120 kutoka kwa rafiki zake na mitandao ya simu.

"Niliamini kile ambacho mchungaji aliniambia, kuwa nitafanikiwa kupata ajira. Hivyo sikuwa na shida kukopa, kwa kuwa niliamini mwishowe ningeliweza kulipa pesa hizo.” Hatahivyo baada ya kuendelea kusota bila ajira, Bw Opil alianza kuhisi kuwa amelaghaiwa.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dennis Opili alikopa pesa kutoka kwenye programu (apps) za compyuta kumlipa mchungaji

Muda mfupi alianza kufuatwa na makampuni ya mkopo yakimdai malipo.

"Wakati mwingine ninakuaga nimekaa mahali fulani, nimetulia, nikifikiria kuhusu mambo. Halafu unasikia mtu anakupigia simu, anataka umlipe pesa yake, na hauna chochcote cha kuwalipa," anasema

"Niliogopa kwasababu hujui ni hatua gani wanaweza kuichukua iwapo hautawalipa. Hujui kama watakushitaki, au labda watakupeleka katika mahabusu ya polisi ."

Kwa bahati nzuri sasa ameweza kupata kibarua, ambacho kimemuwezesha kulipa deni hilo la pesa, kwa makampuni yaliyomkopa na marafuiki zake.

"Bado ninamuamini sana Mungu," anasema. "Kile ninachoweza kukifanya ni kuwa tu mwangalifu zaidi."

Nilishinikizwa kutoa

Sio Kenya peke yake ambako watu waningia katika madeni kwa matumaini ya kupata muujiza. Mwanamke ambaye alikuwa akihudhuria kanisa la Nigeria nchini Marekani na mume wake walijipata katika masharti meni ya kifedha - mkiwemo matarajio ya kutoa safaka ya mbegu, au "kupanda mbegu".

"Sarah", kama ninavyoweza kumuita, aliniomba nisitumie jina lake, au kusema anaishi katika jimbo gani la Marekani, kwa hifu ya vitisho kutoka kwa kanisa lake au mawakili wake.

Anasema waumini wote na wachungaji wa eneo katika kanisa lake la awaliwalitarajiwa kutoa "fungu la kumi" asilimia 10 ya kipato chao cha pesa cha kila mwezi kugaramia kanisa na uongozi wake nchini Nigeria. Na hiyo ilikuwa ni nyongeza kwa kile kilichoitwa "tunda la kwanza" – mshahara wao wote wa kwanza wa kila mwaka.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muinjilisti wa Marekani Oral Roberts (1918-2009) anafahamika kama baba wa Ijili ya Mafanikio

Viongozi wa ngazi ya chini walipangiwa kima cha kukusanya kila mwezi, jambo ambalo anasema liliwalazimu kuwashinikiza waumini wao kupanda mbegu. Wafuasi waliambiwa kuwa watabarikiwa na mchungaji mkuu aliyepo Nigeria.

Sarah anasema aliona watu wakilipa “pesa za mbegu” kwa kutumia kadi zao za benki kanisani.

"Nakumbuka mara moja kuna mwanamke kanisani alisema:’Nimekuwa nikitoa fungu la kumi, lakini bado nabaki bila pesa za kutosha inapofika mwisho wa mwezi.'"

Jibu la mchungaji kwa mujibu wa Sarah lilikuwa ni kuwaambia watu kuwa ilikuwa ni muhimu zaidi kutoa pesa zao kanisani kuliko hata kulipa kodi. Na anasema kuwa kwa yeyote ambaye aliuliza inakuwaje muujiza hautokei aliambiwa: "Haukufanya maombivya kutosha, haukupanda mbegu za kutosha. Haukuwa na imani ya kiwango cha kutosha."

Anasema mumewe alishinikizwa amuache kwa kuwa alikazana kuuliza maswali – lakini hatimaye wote wawili walilikacha kanisa hilo.

Sasa kwa nini watu wengine wanasalia kwenye makanisa ya sampuli hiyo?

Dkt Jörg Haustein, ambaye ni profesa mshiriki wa masomo ya wakristo duniani katika Chuo Kikuu cha Cambridge, anasema inawezekana kuelewa kwanini watu wanaendelea kutoa wakati "ahadi hazilipi kama vile walivyotangaziwa awali".

Kwa watu wa kipato cha kati na kelekea juu, kama walio wengi katika kanisa la Sarah, Dkt Haustein anasema Injili ya mafaniki inawapa ”matumaini ya kufanikiwa kiuchumi na kukua kifedha, na hicho ndicho kinachowavuta watu."

Maelezo ya video, Africa Eye: Wachungaji walaghai wanaowatapeli waumini Uganda

Lakini inaweza kuwavuytia pia wale wanaoishi katika umasikini, anasema.

"Kanisa ambalo linasema: 'Tunafahamu kuwa unaumia, na tunasuluhu la kivitendo na linaloweza kufikiwa kwa ajili yako,' litavutia zaidi kuliko lile linalohubiri will be more attractive than one that preaches mambo mengine ambayo hayaeleweki na mabadiliko ya kimfumo."

Lakini ni kwanini, nauliza, watu wanaendelea kutoa pesa zao hata kama ikiwalazimu wanajiingiza katika madeni?

"Si ni kama kucheza mchezo wa bahati nasibu wakati haiuna pesa yoyote ?" Dkt Haustein ananiuliza.

"Ni kitu fulani ambacho kinaonekana kwa mbali kuwa rahisi kwasababu unaweza kuazima pesa mia kadhaa za kenya kwenye kwa njia ya simu, uwekeze na kuona iwapo inasaidia.

"Bilas haka, kuna hali ya kutafuta suluhu ya matatizo pia, linaweza kuwa ni tumaini la mwisho alilonalo mtu.

Nchini Kenya Evarline Okello anasema uzoefu alioupata haujamfanya aache Imani yake.

"Siwezi kusema kuwa kanisa ni baya. Kanisa ni zuri. Ni wachungaji wanaofanya makosa. Ni wao wanaoomba pesa ."