Kampuni ya mazishi yatishia kumshtaki mchungaji kwa 'kumfufua maiti' Afrika kusini

Chanzo cha picha, Alph Lukau/Facebook
Kundi la wasimamizi wa mazishi nchini Afrika kusini wanasema watamshtaki mchungaji anayejiita mtume anayedai 'kumfufua maiti'.
Video iliyosambaa ya mchungaji Alph Lukau inamuonyesha akipiga kelele akisema 'inuka' kwa anayeonekana kuwa maiti ndani ya jeneza ambaye baada ya hapo anainuka nakukaa wima huku waumini na wafuasi wakisherehekea.
Kampuni hiyo ya mazishi inasema ilihadaiwa katika kuhusika kwenye tukio hilo.
Kioja hicho, kilichofanyika nje ya kanisa la mchungaji Lukau karibu na Johannesburg, kimeshutumiwa na kukejeliwa na watu wengi.
"Hakuna miujiza yoyote," tume inayohusika na kuendeleza na kulinda utamaduni, dini na lugha au makabila ya jamii mbali mbali (CRL Rights Commission) imeliambia shirika la habari nchini..
"Hufanywa ili kuwahadaa watu wanyonge watoe pesa."
'Kuzihadaa' kampuni 3
Kampuni tatu za mazishi zinazosema zilihaidawa na 'mpango huo' sasa zinawasilisha kesi kwa kuharibiwa sifa.
Kingdom Blue, Kings & Queens Funeral Services na Black Phoenix zimeviambia vyombo vya habari nchini kwamba wawakilishi wa kanisa hilo waliwahadaa katika namna tofuati.
"Wanaotuhumiwa kuwa jamaa za maiti" wameiambia kampuni ya Kings & Queens Funeral Services kwamba wamekuwa na "mzozo na kampuni nyingine ya mazishi".
Inadaiwa kwamba wateja hao walibandika kibandiko cha nembo ya "Black Phoenix kwenye gari lao binafsi" kuonekana kuwa wa kuaminika kwa Kings & Queens Funeral Services walipokwenda kukodi gari la kusafirisha maiti kutoka kwao.
Mjadala wa kitaifa
Jeneza hilo, wakurugenzi wa kampuni hiyo ya mazishi wamesema lilipatikana kutoka kwa Kingdom Blue.
Kanisa la mchungaji Lukau, Alleluia Ministries International, bado halijajibu ombi la BBC kutoa tamko kuhusu mkasa huu.
Mtandao wa The Sowetan unaripoti kwamba kanisa hilo limegeuza kauli yake kuhusu kufufua maiti tangu shutuma zizuke, likieleza kwamba mwanamume "aliyefariki" "yuko hai" alipoletwa kwenye eneo hilo la Kramerville.
Mchungaji Lukau "alikamilisha tu, miujiza ambaye Mungu ameanza", Alleluia International Ministries imenukuliwa na mtandao wa The Sowetan.
Video hiyo imezusha mjadala wa kitaifa kuhusu wachungaji bandia na ulioshutumiwa na viongozi wa kidini wanoatambulika.
Hatahivyo baadhi ya Waafrika Kusini wamelizungumzia suala hilo katika mitandao ya kijamii kwa kutumia hashtag #ResurrectionChallenge katika kudhirisha ucheshi kuhusu suala hilo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1

Mwisho wa X ujumbe, 2

Mwisho wa X ujumbe, 3

Ni mkasa wa hivi karibuni wa kiwango cha juu kuhusu viongozi wa kidini nchini humo wanaotuhumu kufanya miujiuza kwa waumini.
Mwaka jana, Mchungaji Afrika kusini alipatakiana na hatia kwa kuwapuliza wafuasi wake kwa dawa ya wadudu ambayo alituhumu kwa uongo kwamba ni tiba kwa saratani na HIV.