Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 17.12.2022

Antoine Griezmann

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United inafkiria kumuwania mchezaji wa kiungo cha mbele Antoine Griezmann mwenye umri wa miaka 31 kutoka Atletico Madrid, aliyechangia ushindi wa Ufaransa katika kombe la Dunia 2018 na kuisukuma timu hiyo ya taifa katika fainali za 2022. (Mediafoot)

Real Madrid zimejiunga katika kinyanganyiro cha kumsajili mchezaji mwenye umri wa miaka 23 wa PSV Eindhoven na winga wa Uholanzi Cody Gakpo, anayehusishwa na Manchester United na Newcastle. (Mirror)

Manchester United inataka kumsajili Gakpo, aliyefunga mabao matatu katika kombe la dunia 2022, ifikapo Januari akitarajiwa kuichukua nafasi ya Cristiano Ronaldo. (Telegraph)

Cody Gakpo

Chanzo cha picha, SNS

Wolves wanajaribu kumsajili mshindi mara tano wa ligi ya mabingwa Isco kutoka Sevilla. Mchezaji huyo wa miaka 30 aliyekuwa akicheza kiungo cha kati kwa Real Madrid pia anasakwa na Juventus, Napoli na Aston Villa. (Todofichajes)

Huenda ikawa Januari yenye shughuli nyingi za uhamisho kwa Wolves, wanaotaka kuwasajili hadi wachezaji sita wapya wakati dirisha la uhamisho litafunguliwa. Meneja mpya Mhispania wa klabu hiyo Julen Lopetegui ameashiria anataka kuongeza wachezaji zaidi kutoka timu ya taifa ya Uingereza. (Times)

Wolves wanataka kumsajili beki wa kulia wa Manchester United Aaron Wan-Bissaka, mwenye umri wa miaka 25. (Express & Star)

Sofyan Amrabat

Chanzo cha picha, Getty Images

Mchezaji anayeripotiwa kusakwa na Liverpool na Tottenham Sofyan Amrabat, mwenye umri wa miaka 26, ameziamsha klabu kuu za Ulaya kwa umahiri alioonesha kwenye timu ya Morocco katika kombe la dunia, kwa mujibu wa kakake. Amrabat anaichezea Fiorentina. (De Telegraaf, kupitia Talksport)

Everton itajiunga katika kumwania kumsajili mchezaji wa Ajax mwenye umri wa miaka 22 raia wa Ghana Mohammed Kudus katika dirisha la uhamisho Januari. (Ekrem Konur kwenye Twitter)

Mshambuliaji wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa Adrien Rabiot, mwenye umri wa miaka 27, ameelezea matamanio yake kujiunga na Barcelona. (Sport)

Cristiano Ronaldo, mwenye umri wa miaka 37, huenda anajitayarisha kutangaza kustaafu anasema Patrice Evra, aliyewahi kucheza na mshambuliaji huyo wa Ureno katika klabu ya Manchester United. Ronaldo hajasajiliwa katika klabu yoyote baada ya kuondoka United mnamo Novemba. (Sky Sports)

Christiano Ronaldo

Chanzo cha picha, Getty Images

Newcastle, Middlesbrough na Sunderland zote zina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Birmingham City Jobe Bellingham, mchezaji huyo wa miaka 17 kakake mdogo wa mchezaji kiungo cha kati wa timu ya taifa ya Uingereza Jude. (Teamtalk)

Leicester, Wolves na West Ham ni miongoni mwa pande zinazomtaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Morocco mwenye umri wa miaka 22 Azzedine Ounahi baada ya kuwavutia katika kombe la dunia. Ounahi anaichezea Angers katika Ligue 1. (Sky Sports)

Ethan Mbappe, kakake mdogo mwenye umri wa miaka 15 wa nyota wa timu ya taifa ya Ufaransa Kylian, alianza kuichezea Paris St-Germain katika mechi ya kirafiki dhidi ya Paris FC na kushinda kwa 2-1 siku ya Ijumaa. (Athletic)