Chelsea 4-4 Man City: Je, Ligi Kuu ya Uingereza iko katika ubora wake?

WQ

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Meneja wa Chelsea Mauricio Pochettino katika uwanja wa nyumbani Stamford Bridge

Chelsea na Manchester City zilicheza mechi iliyokuwa na msisimko mkubwa na mabao nane yakapatikana – wakigawana 4-4. Mechi hiyo imekuwa gumzo katika ulimwengu wa soka.

Baada ya bao la kwanza la Haaland. Goli la Thiago Silva, 39, lilimfanya kuwa mfungaji mwenye umri mkubwa zaidi wa Chelsea na Raheem Sterling alifunga la pili dhidi ya klabu yake ya zamani.

Manuel Akanji aliisawazishia City muda mfupi kabla ya muda wa mapumziko. Haaland alifunga bao la tatu – likiwa ni bao lake la 49 katika Ligi Kuu ya Uingereza katika mchezo wake wa 47.

Nicolas Jackson, baada ya kufunga mabao matatu dhidi ya Tottenham, aliisawazishia Chelsea tena - lakini Rodri alifunga bao lililoonekana kama bao la dakika za mwisho kwa City.

Hata hivyo, dakika za lala salama, Chelsea walipata mkwaju wa penalti ambao Cole Palmer - aliyesajiliwa majira ya kiangazi kutoka City - alifunga kwa shuti kali.

Wachambuzi wanasemaje?

Mlinzi wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza, Jamie Carragher aliiita "Ligi ya Uingereza katika ubora wake," alisema kwenye runinga ya Sky Sports:

"Ni mechi ya kuvutia na Chelsea walipata bao la kusawazisha mwishoni. Najua mashabiki wa Man City watasikitika lakini kukosekana mshindi katika mchezo huu kulivutia sana."

Kipa wa zamani wa Chelsea Mark Schwarzer, alipozungumza na BBC Radio 5 Live, alisema: "Ulikuwa mchezo wa kustaajabisha. Tangu mwanzo, mchuano ulikuwa mkali sana. Walicheza vizuri dhidi ya timu bora zaidi duniani kwa sasa."

Beki wa zamani wa City, Micah Richards alisema: "Ni mechi ya kuvutia – ilikuwa na kila kitu - mabao, ulinzi mbovu na uzembe katika ukabaji.’’

Ajabu ya Ligi Kuu ya Uingereza

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mabao nane, penalti mbili na mambo mengine - ikiwa ni pamoja na wachezaji kufunga dhidi ya vilabu vyao vya zamani - haishangazi kuona wachambuzi walikuwa wakifuatilia pambano hilo.

Kocha wa Chelsea Mauricio Pochettino aliitaja kuwa "jioni ya kustaajabisha" licha ya kupata sare akiwa nyumbani. "Ndiyo maana Ligi Kuu ya Uingereza ndiyo ligi ajabu zaidi duniani," aliongeza.

"Ni vigumu kuzungumza kwani kila mmoja anataka kusema jinsi mchezo ulivyokuwa wa kusisimua. Manchester City ni timu bora zaidi duniani na Chelsea walikuwa jasiri na walijaribu kutafuta pointi tatu."

Mpinzani wake Pep Guardiola amefurahia mechi hiyo muhimu akiwa kocha wa Manchester City, na hakuweza kuficha kuvutiwa kwake na kile timu zote mbili zilizalisha.

Ilikuwa ni mechi ya tano katika historia ya Ligi Kuu ya Uingereza kuwa na sare ya mabao manne- na ya kwanza tangu 2009.

"Ulikuwa mchezo mzuri na wa kuburudisha katika Ligi Kuu," alisema Guardiola. "Timu zote zilitaka kushinda. Chelsea wana timu na wachezaji wa wazuri."