Wadau wa soka na serikali visiwani Zanzibar waanza kuhamasisha soka la ufukweni

Wadau wa soka na serikali visiwani Zanzibar wameanza jitihada za kuhamasisha mchezo wa soka la ufukweni kwa kuandaa mashindano mbalimbali.
Licha ya kuzungukwa na fukwe za kuvutia, mchezo huo haukuwa unapewa kipaumbele visiwani humo.
Hata hivyo, siku za hivi karibuni kumeripotiwa kuongezeka kwa mashindano sambamba na vijana wengi kupata muamko wa kushiriki katika kusakata kabumbu pembezoni mwa bahari ya Hindi.
Mwandishi wa BBC, Alfred Lasteck ameandaa taarifa hii akiwa Zanzibar…









