Periodontitis: Matatizo ya ufizi yanayoathiri afya yako

Chanzo cha picha, Getty Images
Yaweza kuwa Yamesongamana, mpangilio mbaya, yana matundu na ufizi uliovimba, meno yetu ni maarufu kwa matatizo hayo.
Binadamu wa sasa wana shughuli na mwingiliano wa kila siku ambao unahitaji kuhakikisha meno na ufizi haupati magonjwa.
Badala ya kuwa na maumivu ya meno na ufizi, afya yetu ya kinywa huathiri kila kitu kuanzia katika lishe yetu hadi ustawi wetu wa jumla na hatari ya kifo kutokana na sababu yoyote.
Hii ni kwa sababu magonjwa ya kinywa huwa hayabaki mdomoni kila wakati.
Imeanza kuonekana kuwa kuna uhusiano wa karibu kati ya afya ya kinywa na baadhi ya magonjwa hatari zaidi duniani, ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa moyo na mishipa, kisukari na Alzheimer- ugonjwa unaoathiri ubongo, ikisisitiza jukumu la kinywa kama kioo cha afya na magonjwa na kama mlinzi wetu na ustawi wa jumla.
Kwa bahati mbaya, labda kipengele kinachojulikana zaidi cha afya ya kinywa mara nyingi hupuuzwa.
Kukua kwa Ugonjwa
Periodontitis, au ugonjwa wa ufizi, ni ugonjwa wa pili unaoenea zaidi wa kinywa baada ya kuoza kwa meno unaoathiri zaidi ya 47% ya watu wazima wenye zaidi ya umri wa miaka 30.
Kuanzia umri wa miaka 65, 64% wana periodontitis ya wastani au kali. Ulimwenguni ni ugonjwa wa kumi na moja unaojulikana zaidi ulimwenguni.
Periodontitis ni ugonjwa ambao haupatikani juu ya ufizi ambao unaweza kuona unapotabasamu, lakini hukaa chini kabisa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya awamu ya awali ya uvimbe wa juu juu katika sehemu inayoonekana ya ufizi (gingivitis), bakteria husafiri chini ya mstari wa fizi hadi kwenye mifuko iliyo karibu na mzizi wa jino ambapo humomonyoa miundo inayoshikilia jino.
Kutokana na hali ya kujificha ya ugonjwa wa periodontitis, wagonjwa wengi hawajui kuwa iko pale hadi utakapofika hatua za mbele zaidi ambapo huchangiwa na usafi wa mdomo pia.
Kwa wengi, ugonjwa huo hautambuliwi hadi wanapokuwa na umri wa miaka 40 au 50, anasema Sim K. Singhrao, mtafiti mkuu katika shule ya meno ya Chuo Kikuu cha Lancashire nchini Uingereza.
Wakati huo, uharibifu mkubwa unaweza kuwa tayari umepunguza usanifu wa jino na hatari ya kupoteza. Wakati huo huo, maambukizi hutuma bakteria wengi kama vile Treponema denticola na Porphyromonas gingivalis kupitia mkondo wa damu kwa miongo kadhaa.
Bakteria katika damu
Ni uwepo huu wa muda mrefu wa bakteria wanaosababisha magonjwa kwenye fizi na mkondo wa damu ambao hutengeneza afya zetu mbali zaidi ya mdomo.
"Kama utafikiria mtiririko wa damu kama basi, linalobeba abiria, vitu kama bakteria mdomoni na itaenda kila mahali kwenye mwili," anasema Singhrao. "Nyingine zitashuka kwenye ubongo, zingine kwenye mishipa, zingine kwenye kongosho au ini."
Sehemu ambapo kuna udhaifu katika viungo hivi au wakati vijidudu havijauawa kwa ufanisi, husababisha kuvimba na kuanza au kuimarisha vichocheo vya magonjwa mengine.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa kweli, ugonjwa wa periodontitis unahusishwa na orodha ya baadhi ya magonjwa yasiyoambukiza yaliyoenea zaidi ulimwenguni: ugonjwa wa moyo na mishipa, kisukari, Alzeima , unene wa kupindukia , aina mbalimbali za saratani, magonjwa ya viungo vya mifupa, matatizo katika ubongo (Parkinson), nimonia, na matatizo ya ujauzito. .
Uhusiano wa pande mbili
Kwa masharti haya mengi, ni uhusiano wa njia mbili. Kwa mfano, ugonjwa wa periodontitis unaweza kuzidisha hali kama vile ugonjwa wa mishipa atherosclerosis,na ugumu wa kuta za mishipa.
Hata hivyo, bakteria wanaosababisha periodontitis ambao kwa kawaida hupatikana kwenye kinywa tu wamegunduliwa kwenye utando wa ndani wa mishipa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kati ya hali hizi zote sugu za afya, ugonjwa wa kisukari unauhusiano mkubwa zaidi kwa namna mbili na periodontitis. Watu walio na ugonjwa wa kisukari cha aina ya 2 wana hatari mara tatu ya kupata ugonjwa wa periodontitis kuliko watu wasio na ugonjwa huo. Kwa watu walio na ugonjwa wa kisukari cha aina ya 2 na ugonjwa wa periodontitis, maambukizi huzidisha uwezo wa mwili kudhibiti viwango vya sukari ya damu.
Lakini ni nini kiko nyuma ya uhusiano huu?
Kutoka kuwa ufizi hadi kutoa damu
Inahusiana na mtiririko wa mara kwa mara wa bakteria kutoka mifuko wa ndani wa ufizi hadi kwenye damu.
Mfumo wa kinga unapotambua bakteria au vimelea vingine vya magonjwa, seli za kinga hutoa molekuli zinazojulikana kama vichocheo. Alama hizi za vichocheo husaidia mfumo wa kinga kushambulia na kuua vimelea vya magonjwa vinavyovamia.
Uvimbe na uwekundu unaoonekana wakati mwingine karibu na jeraha ni matokeo ya majibu haya ya vichocheo. Kwa muda mfupi, dalili za vichocheo hufanya kama miongozo bora ya mfumo wa kinga kutambua mahali ambapo maambukizo yanawezekana. Lakini wakati walinzi hawa wanabaki mwilini, husababisha shida nyingi.
Hali nyingi zinazohusiana na periodontitis zina dalili za vichocheo vya kuvimba. Kwa mfano, karibu miaka 30 iliyopita, dalili ya kuvimba huitwa tumor necrosis factor alpha iliwekwa wazi ili kuongeza kinga ya insulini kwa wagonjwa wa kisukari

Chanzo cha picha, Getty Images
Hii ilifuatiwa ugunduzi wa hivi karibuni wa wimbi la dalili zinazochochea ambazo huzidisha ugonjwa wa uzito kupita kiasi na kisukari cha aina ya 2. Mtandao huu mnene wa dalili za vichocheo zimesababisha utafiti unaolenga kutibu ugonjwa wa sukari kwa kupunguza uvimbe sugu.
"Magonjwa yote ya uvimbe yanahusiana, yanaathiri kila mmoja," anasema Palle Holmstrup, profesa katika idara ya meno katika Chuo Kikuu cha Copenhagen. "Periodontitis ni mojawapo ya magonjwa ya kawaida, ikiwa sio ya kawaida, ya uvimbe wa mwili wa binadamu."
"Dalili za uvimbe ni sawa ambazo zinafanya kazi katika aina mbalimbali za magonjwa ya uvimbe, ugonjwa wa moyo, kisukari, nk. Ikiwa una periodontitis, utakuwa na kiwango cha juu cha mfumo wa chin iwa uvimbe."
Majaribio kwa panya
Kwa binadamu, ni vigumu kuchunguza moja kwa moja jinsi kutibu periodontitis kunaweza kupunguza hali kama vile kisukari, kwa sababu sawa na atherosclerosis: huwezi kukataa matibabu ya mgonjwa kwa ugonjwa wao, hasa ikiwa unashuku kuwa inaweza kuwa mbaya zaidi hali zao.
Hiyo imefanya utafiti huu kuwa changamoto ya magonjwa ya uvimbe kuwa ngumu sana na uhusiano wa kisababishi kuwa mgumu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hata hivyo, Holmstrup walipima athari za periodontitis kwenye ugonjwa wa kisukari kwa panya. kiliabgalia tofauti ya mwitikio wa sukari katika damu kwa panya wenye kisukari walio na periodontitis. Periodontitis ilisababisha ongezeko la 30% katika kiwango cha sukari kwenye damu baada ya chakula.
Athari ya kupoteza meno
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Hitimisho la mwisho la periodontitis, ikiwa itaachwa bila klitibiwa ni kupoteza jino. Mbali na miongo kadhaa ya kuvimba kwa muda mrefu, kupoteza jino hubeba hatari mpya za kiafya pamoja na kupungua kwa utambuzi na shida ya akili.
Katika uchunguzi mkubwa zaidi wa aina yake, Wu alichunguza takwimu za afya ya wagonjwa 34,000 nchini Marekani na kugundua kuwa kwa kila jino mtu anapoteza, wana hatari ya 1.4% ya kupungua kwa utambuzi na ongezeko la 1.1% ya hatari ya shida ya akili.
Kwa ujumla, wale ambao walikuwa wamepoteza meno walikuwa na hatari ya kuongezeka kwa 48% ya kupungua kwa utambuzi na 28% iliongeza hatari ya shida ya akili, ikilinganishwa na watu kama hao ambao walikuwa na meno yao yote.
Kupoteza meno kumepuuzwa kwa kiasi kikubwa kama sababu ya hatari ya shida ya akili na Wu anasema mara nyingi anatazamwa kwa mshangao anapoonyesha uhusiano kati ya wawili hao. "Afya ya kinywa ni sehemu inayokosekana," anasema Wu. "Tunajaribu kutoa ushahidi kuonyesha kwamba inapaswa kuwa sehemu ya mlingano."
Ingawa periodontitis inaweza kuwa sababu ya kawaida ya kupoteza jino, kunaweza kuwa na sababu nyingine nyuma ya athari hizi kando na kuvimba. Hadi sasa, tafiti za upotezaji wa jino za Wu zimechunguza tu uhusiano na sio sababu, lakini anataka kuchunguza kazi ya lishe katika uhusiano huu tofauti na mambo mengine.
Usafi wa mdomo
Uhusiano unavyojitokeza kati ya afya ya kinywa na hali hii nyingi vina jibu moja muhimu sana: ni rahisi kupunguza hatari yako ya kupata periodontitis na kutibu kwa ufanisi ikiwa tayari unayo.
"Ikiwa tutapiga mswaki vizuri na kufanya usafi wa mdomo, tunaweza kuzuia mwanzo wa periodontitis," anasema Wu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ikiwa ugonjwa utatokea, katika hatua za mwanzo inaweza kutibiwa kwa kuongeza na kupanga mizizi, ambayo hukwangua vijidudu kutoka chini ya jino na chini ya mstari wa ufizi.
Ikiwa una periodontitis kali, suluhisho linaweza kujumuisha matibabu ya upasuaji , "ambayo ilihusisha kufuta tishu laini ya ufizi na kusafisha nyuso za mizizi na kuweka upya tishu," anaelezea Holmstrup.
Shida ni kugundua, kwa sababu ya hali ya kawaida ya ugonjwa, pamoja na maoni potofu ya kawaida kwamba usipokuwa na maumivu makali ya meno, hauhitaji kwenda kwa daktari wa meno. Suluhisho hapo ni rahisi tena: ikiwa una miadi na mtaalamu wa afya, usicheleweshe.















