Urusi na Ukraine: Mifumo ya ulinzi wa anga ya Magharibi kwa Ukraine na jinsi itakavyobadilisha vita

Mwezi uliopita, orodha ya silaha ambazo nchi za Magharibi zinapangwa kusafirishwa au kuuzwa kwa Ukraine ilibadilika. Mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga ilionekana hapo.

BBC inaelezea jinsi mifumo hiyo inavyoweza kubadilisha hali ya vita siku za usoni.

Hapo awali, Ukraine ilipewa hasa mifumo ya makombora ya kubebeka au mifumo ya makombora ya kupambana na ndege kama vile American Stinger au British Starstreak. Usambazaji wa mara moja pekee wa mfumo mkubwa wa ulinzi wa anga wa S-300 ulikuwa mwezi wa Aprili, ulikabidhiwa kwa Ukraine kutoka Slovakia.

Hivi majuzi, Pentagon iliahidi kuipatia Ukraine mifumo mipya ya kombora ya kupambana na ndege ya NASAMS, ambayo Marekani ilikuwa pamoja na Norway. Hivi sasa, kuna mifumo miwili.

Tovuti ya Defence News ilinukuu chanzo katika duru za ulinzi za Marekani, inaripoti kwamba itachukua wiki kadhaa hadi miezi kadhaa kukubaliana kuhusu kandarasi hiyo. Baada ya hapo, wataalamu Ukraine lazima wajue namna ya kuzitumia.

Hii ni aina mpya ya kombora la kukabliana ndege, uundaji wake ulianza mwaka 1989, utengenezaji ulianza mwaka 1994, mzunguko mzima wa majaribio ulikamilishwa mwishoni mwa miaka ya 1990. Mwaka 1999 toleo lililoboreshwa la mfumo wa ulinzi wa anga wa NASAMS II ulionekana.

Haijulikani ni mfumo gani hasa utakaotolewa kwa Ukraine, lakini mfumo wa ulinzi wa anga wa kizazi kwanza unatumia rada ya AN/MPQ-64 Sentinel na hii ndiyo ilionekana kwenye orodha ya usambazaji ambayo Marekani ilitoa Mei 2022.

Kwa hali yoyote, huu ni mfumo wa ulinzi wa anga wenye nguvu ambao unaweza kulenga shabaha kwa umbali wa hadi kilomita 25 na kwa urefu wa hadi 16 km.

Sifa ya kipekee ya NASAMS ni kwamba inafanya kazi na makombora ya anga hadi anga ya AMRAAM AIM-120. Kombora hili lina maboresho mengi tofauti ambayo yanaboresha sifa zake haswa.

Moja ya faida kuu za makombora haya ya ndege ni kwamba zaidi ya makombora 13,000 kati yake yametolewa. Hii ni muhimu sana, kwa sababu katika hali ya mzozo mkali wa kijeshi, gharama ya risasi kwa mifumo ya ulinzi wa anga ni muhimu na msingi wa mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine bado ni muundo wa mtindo wa Soviet.

Usambazaji wa NASAMS sio mara ya kwanza ambao Ukraine inapanga kusambaza mifumo yenye nguvu ya ulinzi wa anga ya Magharibi. Mwanzoni mwa Juni, Ujerumani ilitangaza utoaji wa mifumo ya ulinzi wa anga ya Iris-T SLM ya masafa ya kati kwa Ukraine. Kama Balozi wa Ukraine nchini Ujerumani Andrii Melnyk alisema katika mahojiano na Ukrinform, Kyiv inakusudia kununua vifaa 10 vya kuanzisha makombora hayo..

Mfumo huu wa ulinzi wa angani hutumia makombora ya kuzuia ndege ya IRIS-T SL yaliyorekebishwa kwa matumizi ya ardhini. Wavuti ya mtengenezaji wa kombora Diehl Defense inaonyesha kuwa jaribio la kwanza la Iris-T SLM lilifanyika mnamo 2014.

Masafa ya kombora katika toleo la mfumo wa ulinzi wa anga wa masafa ya kati, ambayo ni kwamba, kile Ukraine inaweza kupata ni kilomita 40 na urefu wa juu wa kulenga shabaha ni kilomita 20.

Mojawapo ya tatizo kubwa ambalo jeshi la Ukraine linaweza kukumbana nalo ni kuunganishwa kwa majengo haya mawili ya Magharibi katika mfumo wake wa ulinzi wa anga.

Mtaalamu wa jeshi wa Urusi Oleksandr Khramchikhin alisema katika mahojiano na BBC kwamba haoni matatizo yoyote hasa katika hili: "Ikiwa unataka, unaweza kuunganisha kila kitu na kila kitu."

Mtaalamu mwingine David Handelman kutoka Israel hakubaliani na hili.

"Suala la kuunganishwa katika mfumo wa ulinzi wa anga wa nchi ni muhimu sana, kwa sababu NASAMS imewekwa kwa usahihi kama chombo cha mtandao (network) kwa ushirikiano wa juu iwezekanavyo na zana nyingine, hivyo itakuwa na ufanisi zaidi. IRIS-T SLM complexes, ambayo imeahidi Ujerumani, inaweza kuunganishwa kupitia mtandao wa kubadilishana data kulingana na viwango vya NATO, kisha ushirikiano na mifumo ya ulinzi wa anga ya Kiukreni ya maendeleo ya Soviet pengine itahitaji ufumbuzi wa ziada wa kiufundi," alielezea.

Ujumuishaji wa mifumo ya kigeni ya kupambana na ndege kwenye mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine ni kazi muhimu, ukizingatia ulinzi wa anga ni mzuri katika mfumo ambao vifaa vyote vimeunganishwa kwenye mtandao mmoja.

Kwa nini ulinzi wa anga ni muhimu kwa Ukraine

Tatizo la ulinzi wa anga katika mzozo wa Ukraine ni moja ya matatizo makubwa zaidi kwa jeshi la Urusi.

Ulinzi wa anga wa Ukraine hauna silaha za kisasa zaidi, zenye nguvu zaidi zilikuwa mifumo ya makombora ya masafa ya kati ya S-300PS na S-300PT, ambayo ilitengenezwa miaka ya 1980. Kwa kuongezea, Buk-M1 ya kati, Tor-M ya masafa mafupi, S-125 na mifumo mbali mbali ya ulinzi wa anga na ya kivita katika uwanja wa mapambano ziko kwenye operesheni.

Moja ya njia za kushinda mifumo ya masafa marefu na ya kati ni kuruka kwa urefu wa chini, lakini MANPADS na silaha za masafa mafupi zinaweza kuleta hatari kubwa hapa.

Ni vigumu kusema jinsi mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine ulivyo na ufanisi, kwa kuwa hakuna taarifa ya wazi kuhusu idadi ya shabaha zilizopunguzwa na kukoswa. Haijulikani ni silaha ngapi za kupambana na ndege zilizoachwa kwenye safu ya jeshi la Ukraine tangu Februari 24.

Hatahivyo, inaweza kudhaniwa mapema au baadaye Ukraine itaanza kupata uhaba wa makombora na mifumo ya ulinzi wa anga, ambayo inaweza pia kushindwa kwa sababu ya utendajikazi na mashambulizi ya ndege na makombora ya Urusi.

Tatizo kwa Urusi

Ulinzi wa anga wa Ukraine unapunguza sana uwezo wa anga wa Urusi, ambayo, kwa kuzingatia taarifa katika vyanzo mbamlimbali, inaweza kufanya kazi haswa ndani ya kina cha mipaka ya mstari wa mbele bila kuthubutu kuruka nyuma sana ya askari wa Ukraine.

Hali hii iliibuka kutokana na ukweli kwamba anga ya Urusi haikuweza kamwe kukandamiza mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine.

Kama Ilya Kramnyk, mtaalam wa jeshi wa Urusi na mtafiti wa Chuo cha Sayansi cha Urusi, hapo awali aliambia BBC, hii ilitokea kwa sababu ukandamizaji wa mfumo wa ulinzi wa anga haukuzingatiwa katika mipango ya kijeshi ya Urusi na Vikosi vya anga vya Urusi havikujiandaa kwa mafanikio yake.

"Urusi kimsingi iliendelea kujiandaa kwa vita na adui kama kambi ya NATO. Na kambi ya NATO haina mfumo wa ulinzi wa anga ardhini na inategemea nguvu za anga. Mfumo mkuu wa ulinzi wa anga wa NATO ni wapiganaji," alisisitiza.

Haitoshi

Usambazaji wa silaha za Magharibi kwa Ukraine ulianza hata kabla ya uvamizi wa Urusi Februari 24, lakini mwanzoni mwa vita waliongeza kwa wingi.

Mfadhili mkuu wa vifaa pamoja na msaada wa kifedha ni USA. Tangu Februari 24, kiasi cha msaada wa Marekani kwa Ukraine kimefikia zaidi ya dola bilioni 6.92. Na ikiwa itahesabiwa tangu mwanzo wa 2021, basi Marekani imetumia zaidi ya dola bilioni 7.62 kwa msaada wa usalama kwa Kyiv.

Marekani ilitoa zaidi ya 1,400 Stinger MANPADS, zaidi ya mifumo 6,500 ya kukinga mizinga na zaidi ya vitengo 20,000 vya silaha nyingine za kukinga mizinga. Ni 126 M777 tu bunduki za kurushia makombora na zaidi ya robo ya mamilioni ya makombora zilihamishiwa Ukraine kutoka USA.

Hata hivyo, hii haikuongoeza ukubwa Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine katika idadi ya silaha dhidi ya jeshi la Urusi.

Mwanzoni mwa Juni, baada ya kundi kubwa la wapiganaji kuwasili Ukraine na kuanza kutumika kikamilifu mstari wa mbele, gazeti la Independent liligundua kuwa faida ya mizinga mikuwa ya jeshi la Urusi huko Ukraine katika vikosi vya jeshi ni 20 kwa moja, na gharama ya makombora ni 40 kwa moja

Mnamo Juni 13, katika mahojiano na BBC, Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine Valery Zaluzhny alisema kuwa nguvu ya moto ya Urusi ni kubwa mara 10 kuliko ya Ukraine.

Wakati huo huo, mshauri wa mkuu wa ofisi ya Rais wa Ukraine, Mykhailo Podolyak, alisema ili kukomesha mashambulizi ya Urusi, Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine vinahitaji vitengo elfu kadhaa vya silaha nzito, howitzers 1,000 za milimita 155, caliber 300 RSZV, Mizinga 500, vitengo 2,000 vya magari ya kivita, drone 1000.

Kile ambacho huwezi kuona kwa macho yako

Kwa kuwa Mykhailo Podolyak alitaja takwimu hizi, Ukraine imepokea shehena nyingi za kijeshi, lakini, angalau katika vyanzo vya wazi, hakuna ilipotajwa idadi inayokaribia takwimu ambazo Podolyak alionyesha.

Maneno kuhusu vyanzo vya wazi sio utaratibu. Oleksiy Danilov, Katibu wa Baraza la Usalama la Kitaifa na Ulinzi la Ukraine alisema katika mahojiano na Liga.net mnamo Juni 18 kwamba "nchi nyingi zinauliza kutotangaza silaha za kijeshi ambazo wanahamisha kwetu."

Kulingana na wataalam wa kijeshi, ni ngumu sana kwa vikosi vya siri vya Jeshi katika ulimwengu wa kisasa. Lakini inawezekana.

"Ikiwa tunazungumza juu ya ukweli kwamba walianza kutoa hata kabla ya kuanza kwa uhasama, ambazo ni, silaha binafsi, basi zinaweza kutolewa kwa idadi yoyote na kwa siri kabisa. Huwezi kusambaza vifaa vikubwa kwa siri," Oleksandr Khramchikhin aliiambia BBC. .

David Handelman, kwa upande wake, alielezea kwamba kwa kweli "sio majina yote yanaonyeshwa kwa undani katika maelezo yote", hata hivyo, hakuna silaha kali zilizoonekana mbele ambazo hazijaonekana hapo awali kwenye ripoti za vyombo vya habari. Hakatai kuwa utoaji uliofichwa unaweza kufanyika katika maeneo ambayo ni vigumu kufuatilia baadaye.

Mara nyingi haiwezekani kuamua kiasi cha misaada ya kijeshi. Nchi nyingi husaidia, kwa mfano, kifedha au kutoa uwezo wa kutengeneza magari ya kivita.

Hata hivyo, habari kuhusu vifaa vipya vya silaha kwa Ukraine inaonekana karibu kila siku.

Silaha kutoka sehemu mbalimbali

Msaada wa kijeshi wa kigeni kuja Ukraine kutoka vyanzo mbalimbali. Kwanza, kutoka kwa maghala ya vikosi vya jeshi. Hiyo ni, serikali fulani inatoa au kuuza silaha kwa Kyiv ambazo tayari ziko kwenye maghala yake ya jeshi.

Hii inapunguza sana usambazaji, anabainisha Oleksandr Khramchikhin: "Kwa kadiri ninavyoweza kuelewa, si jambo la kweli kwa Magharibi kutoa [silaha] zaidi, na yenyewe isiachwe bila silaha hata kidogo."

Pili, ukosefu wa silaha zilizotumwa kwa Ukraine kutoka nchi wafadhili zinaweza kulipwa na nchi za tatu.

Hii ilitarajiwa, kwa mfano, huko Poland, ambayo iliipa Ukraine mizinga 240 ya zamani ya Soviet T-72. Kwa upande wake, inatarajia kupokea idadi fulani za Wamagharibi, lakini hadi sasa mazungumzo na Berlin hayajasababisha chochote. Warsaw pia inatarajia kupokea mizinga kutoka Marekani ndani ya mfumo wa sheria ya Kukodisha kwa Mkopo.

Hatimaye, njia moja zaidi ni ununuzi wa silaha, mpya au za zamani. Mwezi Juni, Kyiv ilinunua vitengo 60 vya kujiendesha vya Krab kutoka Poland na hii ilikuwa amri kamili ya kijeshi, tofauti na bunduki 18 zinazojiendesha zenyewe ambazo zilipewa Kyiv bila malipo.

Walakini, mikataba kamili kama hiyo kawaida huchukua muda kukamilika kwani mara nyingi silaha lazima ziagizwe kutoka kwa viwandani.

Je, kukodisha-kukopesha kutasaidiaje?

Kulingana na Oleksiy Danilov, Ukraine inasubiri sheria ya Kukodisha ya mkopo iliyotiwa saini na Rais wa Marekani Joe Biden Mei 9, 2022 kuanza kutumika.

"Kuna utaratibu, kukopesha-kukodisha bado hakujaanza. Inaweza kuwa Julai-Agosti labda Septemba. Kuna mambo mengi hapa. Unapaswa kuelewa kwamba dunia sio kubwa. Kila mtu. anajua nani ana nini nchini . Upatikanaji wa silaha, vifaa vya uzalishaji wao, risasi," alisema katika mahojiano Juni 18.

Sheria ya Kukodisha kwa Kukopesha yenyewe haiamui usambazaji wa silaha mahususi. Hati hii inarahisisha sana utaratibu mgumu zaidi wa ununuzi wa silaha nchini Marekani, kuruhusu kukodisha silaha kwa Ukraine na nchi nyingine za Ulaya Mashariki.

Kwa mfano, bila sheria, vifaa vilivyokodishwa lazima virudishwe Marekani ndani ya miaka mitano na kufidiwa uharibifu wowote. Sheria ya Kukopesha-Kukodisha inafuta kizuizi hiki.

Pia inamruhusu rais wa Marekani kutoripoti kwa Bunge la Congress kuhusu uchaguzi wa silaha ambazo zinaweza kukodishwa kwa Ukraine katika hali ya dharura.

Mwishoni mwa Mei, Bunge la Marekani pia liliidhinisha kifurushi cha msaada ambacho hakijawahi kufanywa kwa Ukraine cha karibu dola bilioni 40. Zaidi ya kiasi hiki kitaenda kuandaa jeshi la Kiukreni.

Kwa hivyo, Washington, kwa upande mmoja, imerahisisha utaratibu wa usafirishaji wa silaha kwenda Kyiv na kwa upande mwingine iliunga mkono msaada huu kwa mali.

Hata hivyo, wataalam wa kijeshi waliohojiwa na BBC wana shaka kuwa kukodisha-kukopesha na usaidizi wa kifedha unaweza kubadilisha hali katika mzozo huo.

Kulingana na Oleksandr Khramchikhin, usambazaji wa silaha kutoka viwandani unaweza kuwa mgumu na ukweli kwamba sekta ya ulinzi ya Magharibi haikuundwa tena kutengeneza silaha kwa ajili ya mzozo mkubwa kama huo.

"Silaha mpya ni ghali sana na ni vigumu kuzalisha. Hadi sasa sioni dalili zozote kwamba nchi za Magharibi zinakwenda vitani kusambaza [silaha] kutoka viwandani," anasema.

Na kulingana na David Handelman, kwa hali yoyote, usambazaji wa silaha unategemea utayari wa wanasiasa: "Inategemea uamuzi wa kisiasa wa White House. Kimsingi, hata kwa zile zilizopo, iliwezekana kutoa zaidi ya kile kilichotolewa, lakini kila kitu kinategemea uamuzi wa kisiasa."

Ni kiasi gani na kwa kiasi gani kitawasilishwa kwa Ukraine baada ya Kukopeha-Kukodisha kufanya kazi, hakuna mtaalam anayeweza kutabiri, lakini hadi sasa awamu ya silaha mpya mara nyingi hazizidi vitengo vichache, ingawa huko Kyiv wangependa kupokea makumi au hata mamia.

Hili ndilo lililotokea kwa mifumo ya zima moto ya HIMARS salvo, ambayo vitengo tisa pekee ndiyo vimewasilishwa kwa Ukraine hadi sasa.