Ni kwanini Denmark inahifadhi karibu ubongo 10,000 kwenye akiba yake?

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika chumba cha chini cha gorofa la Chuo kikuu cha south Denmark , moja ya vyuo vikuu vukubwa zaidi nchini humo, kuna safu na safu za maelfu ya rafu zenye vikapu vyeupe. Katika kila kikapu kuna ubongo wa binadamu. Kuna jumla ya ubongo 9,479.
Ubongo huo ulitolewa wakati wa upasuaji waliofanyiwa wagonjwa waliofariki kutokana na magonjwa ya kiakili katika taasisi za magonjwa ya akili kote nchini humo kwa kipindi cha miongo minne , hadi kufika miaka ya 1980.
Inakadiriwa kuwa ndio hifadhi kubwa zaidi ya ubongo kuliko kwingineko duniani.
Hatahivyo, ubongo huo ulihifadhiwa bila idhini ya wagonjwa au ndugu zao wa karibu, na hivyo kuibua mjadala mrefu wa kitaifa kurusu la kufanya kuhusu kiasi hicho cha viungo hivyo muhimu vya binadamu.
Hatimaye, katika miaka ya 1990, Baraza la Denmark la Maadili lilibaini kuwa tishu zinaweza kutumiwa kwa ajili ya utafiti wa kisayansi na ni katika mantiki hii kwamba hifadhi ya ubongo ya Chuo kikuu katika jiji la inafanya kazi katika Odense.
Baadhi ya wataalamu wanasema kuwa kwa miaka kadhaa, akiba hiyo ilisaidia katika utafiti wa magonjwa mengi, mkiwemo maradhi ya ubongo ya dementia na msongo wa mawazo. Lakini uwepo wake pia ni unyanyapaa dhidi ya magonjwa ya kiakili na ukosefu wa haki za kibinadamu kwa ajili ya wagonjwa.
Uhifadhi wa maelezo ya kina

Chanzo cha picha, Getty Images
Uhifadhi wa maelezo ya kina
Ukusanyaji ulianza mwaka 1945, baada ya Vita Kuu ya II ya Dunia , huku ubongo ukitolewa kutoka kwa wagonjwa wenye magonjwa ya kiakili waliofariki katika hospitali tofauti za maeneo ya nchi ya Denmark.
Mwanzoni , ubongo ulitunzwa katika katika hospitali ya magonjwa ya akili ya Risskov iliyopo Aarhaus, ambako wapasuaji wa hospitali ya ubongo walifanyia kazi.
Baada ya kufanya uchunguzi, madaktari waliondoa kiungo hicho kutoka kwenye maiti kabla ya kuuzika katika makaburi yaliyokuwa karibu, waliupima, na kuandika maelezo marefu kuhusu hali ya ubongo.
"Maelezo yote ya ubongo huu yametunzwa vyema sana," Martin Wirenfeldt Nielsen, daktari wa ubongo na mkurugenzi wa sasa wa hifadhi ya ubongo katika Chuo kikuu cha Southern Denmark, Odense, aliiambia BBC.
Swali la maadili

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa miaka mitano, Dkt Nielsen amekuwa mkurugenzi wa hifadhi ya ubongo. Ingawa alikuwa na uelewa kuhusiana na mchakato wa kuhifadhi ubongo, hakujua uzito wake. "Nilipoiona kwa mara ya kwanza nilishangaa kwakweli."
Wengi wa wagonjwa walikuwa katika hospitali za kiakili katika kipindi kikubwa cha maisha yao, kwa hiyo zaidi ya maelezo ya ziada taarifa za daktari wa upasuaji wa ubongo, pia kuna historia ya matibabu ya karibu nusu ya wagonjwa ambao walitolewa ubongo.
"Ni taarifa za kina, tunaweza kuonyesha kazi nyingi ambazo madaktari walimfanyia mgonjwa wakati ule, pamoja na kuwa na ubongo wake sasa' ," Nielsen alisema.
Swali la maadili
Kwa miaka mitano, Dkt Nielsen amekuwa mkurugenzi wa hifadhi ya ubongo. Ingawa alikuwa na uelewa kuhusiana na mchakato wa kuhifadhi ubongo, hakujua uzito wake. "Nilipoiona kwa mara ya kwanza nilishangaa kwakweli."
Ingawa uwepo wake haukuwa ni siri, na ulikuwa ukipekiwa tetesi tu wa nyaka fulani, ukusanyaji huu wa viungo vya binadamu halikuwa jambo lililotiliwa maanani na serikali ya Denmark, hadi mpango wa usafirishaji wa wa kuvipeleka katika chuo kikuu cha Odense ulipofichua mengi kuhusu hifadhi hii.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Knud Kristensen alikuwa rais wa Shirikisho la kitaifa la Afya ya akili nchini Denmark wakati wa mzozo uliopelekea kufichuliwa kwa uwepo wa hifadhi ya ubongo.
Mjadala mkubwa wa umma uliibuka kuhusu jinsi maadili ya uhifadhi wa masalia hayo ya binadamu na namna miili hiyo ilivyoshughulikiwa na kuhusu haki za wagonjwa kwa kuhusika kwa makundi ya wanasiasa, ya kidini nay a kisayansi.
Watu wa Denmark walikabiliwa na suala la kijamii ambalo waliliweka kando: ugonjwa wa akili.
"Kulikuwa na unyanyapaa wa aina hiyo unaozingira ugonjwa wa akili ambao hakuna mtu ambaye alikuwa na kaka, dada, baba au mama katika wodi ya magonjwa ya akili aliuzungumzia," alisema Knud Kristensen, rais wa zamani wa shirikisho la kitaifa kwa ajili ya afya ya akili SIND.
"Wakati ule, wagonjwa walilazwa maisha yao yote. Hapakuwa na tiba ya ugonjwa wao, kwahiyo waliishi pale, labda wakifanya kazi katika bustani, jikoni au kazi nyingine zozote. Walifariki pale na kuzikwa katika makaburi kutoka hospitalini," aliiambia BBC Mundo.
Waginjwa wa akili walikuwa na haki chache sana. Waliweza kupata matibabu kwa ajili ya ugonjwa fulani bila aina yoyote ya idhini.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika miaka ya 1930 na 1940, uchunguzi wa damu ulikuwa ni mchakato ambao ulifanywa bila idhini ya wagonjwa au familia zao.
Leo inachukuliwa kama ukatili na kukosa ubinadamu.















