Wanaume wengi Kenya wanakubali kufunga mirija ya mbegu za uzazi-Vasektomi
Na Grace Kuria
BBC News

Chanzo cha picha, AFP/SONNY TUMBELAKAAFP/SONNY TUMBELAKA
Wanaume wengi nchini Kenya wameanza kuvutiwa na upasuaji wa kufunga mirija ya mbengu za uzazi,Vasektomi. Haya ni kwa mujibu wa Marie Stopes Kenya.
“Tumepokea maombi mengi kutoka kwa wanaume. Walakini, hatuwezi kufichua nambari hiyo kwa sababu ya usiri wa mteja.
Shirika hilo la kutoa huduma za Uzazi wa Mpango na Afya ya Uzazi wa Jinsia (SRH) inasema kuongezeka kwa hamu ya kutaka maelezo kunatokana na uelewa zaidi ambao umesababisha upatikanaji na matumizi ya huduma hizi.
"Kwa ujumla, Wakenya wamefahamu kuhusu majukumu sawa ya kijinsia na haja ya kuwa na mawasiliano zaidi kati ya wanandoa, hivyo basi hitaji la wanaume kuwa mawakala wa mabadiliko kwa kuwa washirika wa kuunga mkono katika safari ya kujamiiana na uzazi ya wenzi wao. Tunazidi kuona wanaume wakichukua huduma za SRH” Mkurugenzi Marie Stopes Kenya Inviolata Wanyama alisema.
Daniel mwenye umri wa miaka 39 (sio jina lake halisi) alifanyiwa upasuaji wa vasektomi siku ya Jumamosi, tarehe 15 Oktoba 2022.
"Uamuzi wangu ulifanywa baada ya kuzaliwa kwa mtoto wangu wa tatu. Ilitubidi kutafuta njia bora zaidi (ya kupanga uzazi). Mke wangu alikuwa amejifungua mara 3 kupitia upasuaji , na sikuwa tayari kuhatarisha maisha yake…. Niliamua kwa nini nisimsaidie, kwa sababu wakati mwingine tunaomba sana kutoka kwa wanawake." Daniel alisema.
Kulingana naye, ufahamu zaidi juu ya Vasektomi unahitaji kufanywa, kwani hata katika baadhi ya ziara ambazo yeye na mke wake walifanya kutafuta huduma katika kliniki mbalimbali za familia, baadhi ya matabibu walimkataa kwa maswali kama: “ni kwa ajili yako? Je, umeoa? Kwa nini ungependa Vasektomi? Ni mke wako ndiye anayepaswa kusimamia uzazi wa mpango."

Chanzo cha picha, Getty Images
Hata hivyo aliendelea mbele kutaka huduma hiyo na anasema hajapata madhara yoyote tangu afanyiwe utaratibu huo
Kabla ya Siku ya Utoaji Vasetomi Duniani mwaka huu tarehe 18 Novemba, Marie Stopes Kenya itakuwa ikitoa huduma za Vasektomi bila malipo.
Vasektomi, kulingana na Huduma ya Kitaifa ya Afya (NHS) ni ‘utaratibu wa upasuaji wa kukata au kuziba mirija inayobeba mbegu za kiume ili kuzuia mimba kabisa.’
Hata hivyo inaweza kutenduliwa, ingawa mafanikio (ya kubatilishwa) hayahakikishiwi kila wakati.
"Ikiwa ubadilishaji utafanywa ndani ya miaka 10 ya vasektomi yako, kiwango cha mafanikio ni karibu 55%. Hii inashuka hadi 25% ikiwa mabadiliko yako yatafanywa zaidi ya miaka 10 baaday















