Vita nchini Ukraine: Je, Ukraine imevunja ngome za ulinzi mkali za Urusi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Majenerali wa Ukraine wanasema "wamevunja" safu ya kwanza ya ulinzi ya Urusi katika eneo la kusini.
Tumetathmini ni umbali gani majeshi ya Ukraine yamepiga hatua na kuna dalili gani za mafanikio zaidi kwenye mstari wa mbele.

Ukraine ilianza mashambulizi yake makubwa mapema mwezi Juni ili kuvirudisha nyuma vikosi vya Urusi kutoka katika ardhi waliyoiteka. Ilishambulia kwa pointi tatu kwenye mstari wa mbele wa maili 600-na zaidi (965km).
Eneo la kusini-mashariki mwa jiji la Zaporizhzhia ndilo muhimu zaidi kimkakati.
Kupiga hatua katika mwelekeo huu kuelekea Bahari ya Azov, ikiwa kutafanikiwa, kunaweza kukata njia za usambazaji za Urusi zinazounganisha jiji la Urusi la Rostov-on-Don na Crimea.
Hakujakuwa na maendeleo mengi katika eneo hili, isipokuwa kwa eneo karibu na vijiji vya Robotyne na Verbove katika eneo la Zaporizhzhia, kama inavyoonekana kuangaziwa kwenye ramani iliyo hapo juu.
Ikiwa Ukraine inaweza kukata njia hii kuu ya ugavi basi Urusi itapata yote lakini haiwezekani kudumisha ngome yake kubwa ya kijeshi huko Crimea ambayo ilitwaa mwaka wa 2014 .
Licha ya vizuizi vikubwa, sasa kuna uthibitisho wa kuonekana kwa wanajeshi wa Ukraine wamevunja miundo ya ulinzi ya Urusi kwenye eneo la kusini.
Tumethibitisha video tisa za mitandao ya kijamii kwenye mstari wa mbele karibu na Verbove.

Video nne kati ya hizo zinaonyesha vikosi vya Ukraine vikivunja ulinzi wa Urusi kaskazini mwa Verbove.
Walakini, uvamizi huu sio kwamba Ukraine imeweza kuchukua udhibiti wa eneo hilo.
Kufikia sasa imekuwa tu askari wa miguu wa Kiukreni wakipitia, na hatuoni safu za kivita za Ukraine zikimiminika, zikitumia mwanya na kushikilia ardhi iliyochukuliwa.
Ni nini kinachozuia Ukraine kusonga mbele kwa kasi?
Moscow iliona shambulio hili la kukabiliana likija muda mrefu uliopita na imetumia miezi kadhaa kujenga ulinzi wa kutisha zaidi duniani.

Chanzo cha picha, BBC/DARREN CONWAY
Sehemu kubwa zenye mabomu yaliyotegwa ardhini zimepunguza kasi ya Ukraine
Sehemu hizi zimejaa sana, katika baadhi ya maeneo hadi maeneo tano yenye mabomu yaliyowekwa katika mita ya mraba.
Jaribio la kwanza la Ukraine kuwatimua wanajeshi wa Urusi mwezi Juni liliisha haraka bila mafanikio, huku silaha zake za kisasa, zilizotolewa na nchi za Magharibi zikilemaa na kuungua.
Kyiv tangu wakati huo ililazimika kuondoa mabomu yabrdhini kutumia wanajeshi waliokuwa kwa miguu, mara nyingi usiku na wakati mwingine chini ya mashambulizi Kwa hivyo kusababisha hatua chache kupigwa hadi sasa.
Vifaru vya Ukraine na magari ya kivita yako katika hatari ya kushambuliwa na mabomu ya ardhini ya Urusi, ndege zisizo na rubani na makombora ya kukinga vifaru - kama ilivyo kwenye video moja iliyochambuliwa na BBC Verify ambayo inaonyesha kifaru cha Challenger 2 kilichotolewa na Uingereza kikishambuliwa karibu na Robotyne.
Je, ni nini kinachofuata kwa ajili ya kukabiliana na Ukraine?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Tatizo ambalo Waukraine wanalo sasa," anasema Dk Marina Miron katika Idara ya Mafunzo ya Vita ya Chuo cha King's London, "ni kupata nafasi kubwa ya kutosha kupata askari zaidi."
Wakati huo huo Urusi imekuwa ikisonga mbele katika uimarishaji, na uwanja huu wa vita una nguvu, unaendelea, na Urusi bado inaweza kubadilisha mafanikio ya Ukraine.
Tumeweka kijiografia video ya ndege zisizo na rubani za Urusi ambayo inaunga mkono ripoti kwamba vikosi vyake vya anga, VDV, vimesambaa karibu na mji wa Verbove - hatua inayolenga kuziba mapengo yoyote yaliyotokana na mashambulizi ya Ukraine.
"Vikosi vya Kiukreni vinaendelea kukabiliwa na upinzani kutoka kwa vikosi vya Urusi kwenye uwanja wa vita," anasema Kateryna Stepanenko, mchambuzi wa Urusi katika taasisi yenye makao yake makuu London, RUSI.
"Pamoja na moto wa mizinga, mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na miundo ya ulinzi ya Urusi - Vikosi vya Urusi pia vinatumia sana hatua za kivita za kielektroniki ambazo zinalenga kuzuia mawimbi ya Ukraine na matumizi ya ndege zisizo na rubani."

Chanzo cha picha, Reuters
Vikosi vya Urusi vimechoka na pengine kukata tamaa baada ya kudumu kwa miezi mitatu ya mashambulizi makali, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya masafa marefu ambayo yanalenga njia zao za usambazaji.
Ikiwa Ukraine inaweza kuvunja ulinzi uliosalia wa Urusi na kufika hadi mji wa Tokmak basi hii italeta njia za reli na barabara za Russia kwa Crimea ndani ya safu yake ya mizinga.
Ikiwa wanaweza kufanya hivyo, basi mashambulizi haya ya kukabiliana yanawezakupata mafanikio .
Huenda visisitishe vita, ambavyo huenda vikaendelea hadi mwaka 2024 na pengine zaidi - lakini vitadhoofisha sana juhudi za vita vya Moscow na kuiweka Ukraine katika nafasi nzuri wakati mazungumzo ya amani yatakapoanza.
Lakini kwa Kyiv, muda unayoyoma. Msimu wa mvua utawasili baada ya wiki chache, na kugeuza barabara kuwa matope na kuzuia hatua zaidi.
Zaidi ya hayo kuna sintofahamu ya uchaguzi wa urais wa Marekani, ambapo ushindi wa Republican unaweza kushuhudia uungwaji mkono wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine ukipungua kwa kiasi kikubwa.
Rais Putin anajua anahitaji kuvumilia hadi wakati huo. Wananchi wa Ukraine wanajua inabidi kufanikisha mashambulio yao kwa kasi












