Tetesi za soka Ulaya Jumatano 05.06.2024

TH

Chanzo cha picha, PA Media

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anataka kumsajili winga wa Ukraine Viktor Tsygankov, Chelsea wanatazamia kuwapiku The Gunners kumsajili Benjamin Sesko na West Ham wanamsaka Aleix Garcia.

Arsenal wanamtazama winga wa Girona mwenye umri wa miaka 26 kutoka Ukraine Viktor Tsygankov, ambaye pia anasakwa na AC Milan . (Sport - kwa Kihispania)

Chelsea wana imani kuwa wanaweza kushindana na Arsenal katika harakati za kumsajili mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko kutoka RB Leipzig, 21 . (Standard),

Manchester United wana nia ya kumsajili beki wa Everton na England Jarrad Branthwaite, 21, huku wakitafuta kuimarisha safu yao ya ulinzi. Beki wa Juventus na Brazil Gleison Bremer, 27, na mlinzi wa Nice na Ufaransa Jean-Clair Todibo, 24, pia wanalengwa. (Football Insider)

TH

Chanzo cha picha, PA Media

Manchester United iko tayari kufanya mazungumzo na winga wa Uingereza Jadon Sancho, 24, kabla ya kuamua kuhusu mustakabali wake. Sancho aliisaidia Borussia Dortmund kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kujiunga nayo kwa mkopo kufuatia kutofautiana na mkufunzi wa United Erik ten Hag. (ESPN)

West Ham wanajaribu kuzuia jaribio la Bayer Leverkusen kumsajili kiungo wa kati wa Girona na Uhispania Aleix Garcia, 26. (Guardian).

The Hammers pia wanataka kumsajili winga wa Vitoria Guimaraes na Ureno Jota Silva, 24. (Teamtalk)

Tottenham wako tayari kumtaka Djed Spence, 23, kujiunga na Genoa kwa mkataba wa kudumu baada ya beki huyo wa Uingereza kufanikiwa kwa mkopo katika klabu hiyo ya Italia. (Fabrizio Romano)

Mkufunzi wa zamani wa Newcastle na West Ham Alan Pardew, 62, anasema amevutiwa na kazi ya kuinoa Burnley(Talksport)

Beki wa Fulham Muingereza Tosin Adarabioyo, 26, amefanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kuhamia Chelsea(Mail)

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambulizi wa Roma mwenye umri wa miaka 30 na Argentina Paulo Dybala yuko tayari kuhamia Ligi ya Premia msimu huu. (Sky Sports)

Klabu ya League One Birmingham City imefanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Chelsea na Everton Frank Lampard kuhusu kuwa meneja wao mpya. Lampard pia amezungumza na klabu ya Championship Burnley kuhusu nafasi hiyo baada ya kuondoka kwa Vincent Kompany kwenda Bayern Munich. (Football Insider)

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, 51, anasakwa na klabu ya Uturuki ya Besiktas. Solskjaer hajafanikiwa kupata kazi ya ukocha tangu alipoondoka United Novemba 2021. (Mirror)

Nahodha wa Real Madrid aliyeshinda taji la mabingwa ulaya Nacho, 34, atakutana na klabu hiyo kujadili mustakabali wake. Mkataba wa beki huyo wa Uhispania unamalizika msimu huu wa joto(The Athletic)

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah