Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Barcelona kuamua mustakabali wa Rashford

Marcus Rashford akiichezea klabu ya Barcelona

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marcus Rashford alijiunga na Barcelona kwa mkopo mwezi Julai mwaka jana kutoka United
Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester United haitaweza kumzuia mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford mwenye umri wa miaka 28 kusalia Barcelona ikiwa klabu hiyo ya Uhispania itatoa euro milioni 30), chini ya masharti ya mkataba wake wa mkopo. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Juventus imefanya uchunguzi kuhusu Beto wa Everton, lakini The Toffees wanasita kumruhusu mshambuliaji huyo wa Guinea-Bissau, 28, kuondoka kwa sababu ni mmoja wa washambuliaji wawili waandamizi kikosini. (Sportsport)

Juventus inakaribia kumsajili mshambuliaji wa Manchester City, Justin Oboavwoduo, 19. (Sky Sports Italia - kwa Kiitaliano)

Tottenham, Leeds United na Sunderland wanamfuatilia mshambuliaji wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 19, Endrick, ambaye yuko Lyon kwa mkopo. (Fichajes)

Celtic imekataa ofa ya pauni milioni 14 kutoka kwa Nottingham Forest kwa kiungo wa kati wa Ubelgiji Arne Engels, 22. (Mail)

Liverpool inavutiwa na beki wa pembeni wa Inter Milan na Uholanzi Denzel Dumfries, 29. (Fabrizio Romano)

Fulham wamefikia makubaliano na PSV Eindhoven kumsajili mshambuliaji wa Marekani Ricardo Pepi, 23, lakini hatua hiyo inategemea kupatikana kwa mbadala wake. (Sun)

Kiungo wa kati wa Liverpool na Hungary Dominik Szoboszlai, 25, anasema mustakabali wake hauko mikononi mwake huku mazungumzo yakiendelea kuhusu kandarasi mpya. (Athletic - usajili unahitajika)

Wachezaji wa Inter Milan wakishangilia bao dhdi ya klabu ya Empoli wakati wa mechi ya Serie A

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wachezaji wa Inter Milan wakishangilia bao dhdi ya klabu ya Empoli wakati wa mechi ya Serie A

Chelsea inamfuatilia mlinzi wa Nantes Mfaransa Tylel Tati, 18. (L'Equipe)

Leicester City na Birmingham City ni miongoni mwa klabu sita ambazo zimewasiliana na Newcastle United kuhusu beki wa Uingereza Jamaal Lascelles mwenye umri wa miaka 32. (Sky Sports)

Brighton inajadiliana na Marseille kuhusu kurejea kwa kiungo wa Denmark anayewachezea kwa mkopo Matt O'Riley mwenye umri wa miaka 25. (Athletic - Usajili unahitajika)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi